Madhabahu.(short notes)


10 Aug 2024

Kwa Nini ni muhimu kuhudhuria kanisani/kanisa ni madhabahu, madhabahu sahihi ya MUNGU.

​Kwanza kabisa lazima tujue kuwa ni Nini maana ya madhabahu? Kabla ya yote ngoja tuone madhabahu ya kwanza katika biblia ikijengwa kwa ajili ya nini? Yaani tutambue umuhimu wa madhabahu.

​Ko kumbe madhabahu ndiyo itakayotuunganisha na MUNGU.

​*Madhabahu ya kwanza kabisa katika biblia ilijengwa na nuhu. Katika mwanzo 8:20-23. ukiachana na lle madhabahu ya kwanza ya akina kaini na habili.

​*Nguvu ya madhabahu ilimfanya MUNGU aamue kubadilisha Nia ya kuja kuipiga Dunia kwa mapigo makuu kwa Sababu ya dhambi, yaani baada ya nuhu kutoa sadaka ya kuteketezwa kwa MUNGU kupitia viumbe hai safı vilivyokuwepo ndani ya safina ndipo mahali ambapo BWANA MUNGU aliviongezea thamani viumbe vyote katika Dunia kwa kuanza na mwanadamu wake. ko msamaha wa kwanza wa Dunia wa siku zote ulianza kwa Sababu ya madhabahu.

​*Ko kumbe tunakuja kujua kwamba madhabahu ni sehemu ya upatanisho kati ya MUNGU wa mbinguni na mtu. mambo ya walawi 9:7. yaani hatutapata kuwa safı kama hatujatakaswa kupitia madhabahu. japo Kuna wengine hawajapatana na agano la madhabahu ko si sehemu ya madhabahu ya MUNGU japo wapo na wanaabudu katika madhabahu hiyo.

​*Madhabahu pia ni mahali inatolewa sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya dhambi au agano kwa mfano Ibrahim alimtolea sadaka mwanawe kuwa sadaka ili alithibitishe agano la MUNGU kwake. ili kufikia maagano na MUNGU lazima iwepo sadaka katika madhabahu yake.

​*Ili upate kitu kwa MUNGU basi ni lazima vitu vyako vipungue ili MUNGU wa mbinguni akufanyie mambo makuu. kwa mfano wa sadaka hizo ni maombi pesa na mali, usingizi na mwili warumi 12:1.

​*Pia madhabahu ndiyo mahali penye udhihirisho wa MUNGU kwa mfano madhabahu ya bwana aliyoijenga Eliya ndiyo iliyomdhihirisha MUNGU kwa Wana wa Israel. 1 falme 18:30.

​*Madhabahu ni mahali pekee tunapoliitia tunapoliita jina la BWANA hakuna pengine. mwanzo 12:7-8. bwana anaposema niite nami nitakuitikia, anataka umwite katika madhabahu yake.

​*Wapo watu wengine wanasema hawaoni umuhimu wa kuhudhuria ibada ya MUNGU na wanajipa moyo kumuomba MUNGU walipo hukohuko bila kukusanyika pamoja hao hawana MUNGU kwa kuwa lazima kwanza MUNGU apatikane kwanza kwenye madhabahu ya pamoja ndipo adhiririke kwa madhabahu ndani ya moyo.

​*Ko tunapaikosea madhabahu ya pamoja iliyohalalishwa na MUNGU tunakosa kibali kwa MUNGU wa mbinguni. na Kila kitu tunachofanya au kuomba kunakuwa hakina maana kwa kuwa sisi sio sehemu ya madhabahu ya MUNGU.

​*Zamani zile madhabahu zilifanya kazi kimwili tu kwa Sababu watu walienda kupatanishwa yerusalemu hekaluni pekee na wakaoshwa lakini Sasa madhabahu zote za MUNGU zinaunganishwa kiroho na madhabahu kuu mbinguni ambayo YESU Kristo ndiye sadaka kuu iliyotolewa kutupatanisha sisi.

​*Ko sisi kupitia madhabahu yetu ya pamoja kama Ile ya Israel basi tunapatanishwa kwa pamoja kwa kuwa mahali penye nguvu ya MUNGU panadhirihishwa kwa umoja. basi madhabahu zetu zimewekwa wakfu na MUNGU kwamba ili mradi tumejiungamanisha nazo kupitia agano la madhabahu ambalo ni wokovu na pia kupitia sadaka na mafungu mafungu ya kumi basi mahali popote tulipo tutakuwa madhabahu zetu za ndani zimeungamanika na madhabahu ya kanisa na pia madhabahu kuu ya mbinguni.

JINSI YA KUILINDA MADHABAHU YETU.

​*Kwanza lazima tujue kwanza kwamba madhabahu ya kusanyiko ni kipaumbele kuliko madhabahu ya ndani ya mioyo yetu, yaani kanisa la watu ni kubwa na Lina mamlaka kuliko kanisa katika roho zetu. ko tunapokosea maagano ya madhabahu ya pamoja tunaharibu nguvu ya kanisa. kwa kuwa sadaka za madhabahu zetu za ndani zinafunguliwa na kupata kibali kutoka mbinguni kupitia madhabahu ya pamoja. kumbe kutunza madhabahu ya pamoja ni juhudi inahitajika sana kwa kuwa msingi ni umoja. pia yoshua 6:18.

​*Yoshua 7:1 akani alipokosea kwa kuiba Mali wakfu za madhabahu adhabu iliwapata Hadi wale ambao walikuwa na madhabahu safi za moyoni ndo maana adhabu iliwapata Israel ko hata sisi nasi kama watu tulio na madhabahu Moja kama Wana wa Israel basi tuweke muunganiko na umoja mmoja kwamba Kila mmoja afuatishe agano la madhabahu ya MUNGU ambalo ni wokovu na usafi wa moyo ili tuwe na madhabahu yenye nguvu la sivyo tunakosa nguvu za MUNGU kwakuwa wapo watu wanaovunja maagano.

​*Kwa kugusamali wakfu za madhabahu (maandiko yanoyojenga madhabahu) kwa kuwa msingi wa madhabahu ya kwanza ni torati na msingi wa madhabahu ya Sasa ni YESU Kristo. ko asiwepo miongoni mwetu wa kutukosesha au asiyekuwepo na sisi hapo ndipo tutamwona MUNGU.

Vitu Gani vitafanya kanisa lilaaniwe?

  1. ​Ni kuvunja amri za utakatifu na kufuga maovu.

  1. ​Kuiba fungu la kumi na matoleo na vyote vya rohoni kutalaani maisha yetu yawe chini hiivihivi kiuchumi.

  1. ​Kuchelewa ibada kutafanya MUNGU achelewe kufanya yetu na kdharau mambo yetu kwa kuwa na sisi kimakusudi hatutamvui Nini tunapaswa kufanya.

  1. ​Kukosa au kutotimilika kulifuata agano la wokovu kutasababisha kanisa likose udhihirisho wa nguvu za ROHO mtakatifu na YESU Kristo na BWANA MUNGU.

​*Wapo wengine hawasali Wala hawaendi kanisani ila wanasema na Mimi namwomba MUNGU kivyangu. hapo ni uongo kwa kuwa maombi ya mtu kwa MUNGU lazima yapitie katika madhabahu ya pamoja lengo ni kuweka umoja. sasa ukiwa husali na wenzio wanaounda madhabahu katika kanisa Ina maana wewe hujajiunganisha na bomba kuu au Tanki (madhabahu).

​*Sasa je maji utapata wapi? Hapo Ina maana huna MUNGU ila unajifariji tu kwa kuwa kisima ni MUNGU, Tanki ni madhabahu (kanisa la MUNGU), na pia madhabahu zetu za ndani ni mabomba ya vituo, haya tuone kama Bomba la kituo litatoa maji bila Tanki au kisima??

​God of heaven help and bless your church.........

Comments

Popular posts from this blog

Kuweza kulitendea kazi neno la MUNGU

Mwamuzi(short notes)

Je kwa nini namna ile?