Mwamuzi(short notes)
3. Nani amekufanya mwamuzi kwetu?
20 Jan 2025
Nani amekufanya mwamuzi kwetu?//ijue thamani ya mwamuzi.
Kutoka 2:14.
Kwa Nini mwamuzi akati wamezoea utumwa.mwamuzi alikuja kwa lengo la kuonyesha Nia ya kuwasaidia lakini wao wanamshangaa na kumwona kama anajipendekeza. #MUNGU wa mbinguni amewavusha Israel kwenda nchi ya ahadi, lakini Wana wa Israel wanamshangaa Musa na MUNGU kwamba kwa Nini wamewatoa misri, kwa kuwa shida ya misri waliiona kuwa ni Raha. #na sisi utumwa wa dhambi tunauona ni Uhuru na uzuri kwetu.
Mfano mwingine:
1 samweli 23:1-13.
Daudi aliwaokoa keila kutoka katika mikono ya wafilisti, lakini keila walikuwa wanaenda kumsaliti Daudi kwa kuwa hawakutambua thamani ya mwamuzi.
YESU Kristo ni mwamuzi!! Unaijua thamani yake?
Kuudharau wokovu ni dalili tosha kuwa. Harutambui thamani ya mwamuzi(YESU kristo)
Tutapataje kupona tusipoujali wokovu mkuu namna hii.
Wao waliijua thamani,kwa nini sisi tusiijue? Tunapaswa kuijua,ili tusije tukakataliwa japo tulikuwa kanisani na wokovu ulikuwa wetu.
Tafakari!! Chukua hatua
Comments
Post a Comment