Je kwa nini namna ile?
M
Swali: hakukuwa na njia nyingine mbadala ya kutuokoa sisi mpaka YESU afe?
Amani Ernest Kyamba
SOGH Team.
Let's do GOD'S work together.
Njia zilikuwepo nyingi kwa sababu MUNGU ni mtendaji na muweza wa yote. Kwa hiyo MUNGU alitaka atumie njia ile ile ya wokozi sawasawa na njia ya uharibifu. Yaani alitaka/alipanga kumrudisha mwanadamu katika utakatifu sawasawa na njia ambayo mwanadamu aliingia katika upotevu.
Adamu na Eva walipotea kwa kutokutii. YESU akaonyesha njia ya utii katika maisha yaliyozungukwa na kukosa utiifu, Luka 2:52, (akamtii MUNGU na wanadamu). Pamoja na kwamba mwanadamu hakutii na alizama dhambini yeye YESU akampa chaguo mwanadamu, la kukosa utii au kuamua kutii/kufanywa mtiifu. Kwani kupitia yeye mwanadamu akatambulishwa kwamba inawezekana kuwa mtii.
Kutokutii kwa Adamu kulisababisha kifo. Kifo cha YESU kilimpa mwanadamu nafasi ya kumtii na kumtumikia MUNGU. Adamu alikula tunda akafa, YESU alikufa akaishi. Adamu alifukuzwa kwenye urithi wake, YESU anaturudisha kwenye urithi wa mbingu kupitia neema. Adamu na Eva walipoteza thamani, YESU anarudisha thamani kwa kupitia wokovu.
MUNGU alisema tusile damu kwa kuwa ni uhai wa kiumbe (hili ni agano kati ya MUNGU na mwanadamu) Torati 12:23. Ishara ya YESU kumwaga damu msalabani ni ishara ya kurudisha uhai wa kiroho kwa watu waliokosa uhai (wanadamu).
Ilikuwa ni agano na ni sheria kwamba mtu akiuwawa na mtu, damu ya huyo aliyekufa inakaa kwa aliyeua. Mfano Kaini alipomuua Habili, damu ya Habili (mwanadamu) ikawa inamhukumu Kaini mbele za MUNGU. Hivyo MUNGU aliporuhusu mwokozi (mwanaye YESU) kufa, damu ya YESU ikakaa juu ya wanadamu wote.
Msemo "Damu ya YESU inanena mema" ni jambo halisi na ni la kweli. Kwa hakika damu ya YESU Kristo haipo kuhukumu bali kuokoa. Hivyo damu ya YESU inamkumbusha MUNGU habari ya wokovu wake kwetu. Kwa hiyo ukimwamini YESU unashiriki dhambi ya kumuua YESU, kwa hiyo damu ya YESU inakuwa juu yako, kwa hiyo inaanza kunena mema.
Maana mara zote damu ya YESU inanena mema, kwa hiyo inakuwa ni msaada kwako. Ni kama MUNGU alikuwa anajitafutia kisa kwa wanadamu ili awaokoe kutokana na mfumo ambao aliudhihirisha tangu mwanzo wa mwanadamu. Kwa hiyo akaamua kumtoa mwanaye aliye na damu ya pekee isiyolaani bali inayoponya ili ikae juu ya wanadamu siku zote, kuwapatanisha na yeye. Maana damu inamwagika ila inapolia anayesikia ni MUNGU mwenyewe (Mwanzo 4:7-10).
Neno linasema kuwa ukirudi nyuma unamrudisha YESU msalabani tena. Maana ili usamehewe inabidi YESU afe tena, kwa hiyo ni hatia kurudi nyuma mara kwa mara. Maana damu ya YESU ilimwagika mara moja tu kwa ajili ya ondoleo la dhambi. Sasa mbona wewe inamwagika mara sita mara saba? Unakuwa na laana ya kuidharaulisha damu ya mwokozi (unaifanya iwe kama damu ya mafahari na wanyama, wakati yenyewe ni pure holy kuliko damu zote mbinguni na kote).
Be careful!! Adui asije akajiinua ukapotea mazima. Kwa hiyo MUNGU anataka watu wanaotambua damu ya YESU kuwa ina thamani. Na damu ya YESU inaleta wokovu wa thamani. So be careful.
SOGH Team
Let's do GOD'S work together
Blessed
Comments
Post a Comment