Posts

Showing posts from April, 2026

Neno kwa wasomaji

 Ndugu msomaji, Kabla hujaendelea na masomo haya, ningependa kusema jambo moja kutoka moyoni. Kama kuna sehemu yoyote katika maandishi yangu imeonekana kuwa kali kupita kiasi, ya kuhukumu, au isiyotoa nafasi ya kuelewana vizuri — naomba unisamehe. Kusudi langu halijawahi kuwa kuumiza, kushusha, au kujiona bora kuliko wengine. Ninachoandika kinatokana na kiu ya kumtafuta MUNGU kwa undani na kushirikisha wengine yale ninayojifunza katika safari hiyo. Hata hivyo, bado niko safarini kama wewe — najifunza, nakua, na kurekebishwa kila siku. Naomba usichukue maneno yangu kama hukumu juu yako, bali uyapokee kama mwaliko wa kutafakari, kuchunguza, na kumtafuta MUNGU kwa kina zaidi. Kilicho muhimu zaidi si mimi, bali ni ukweli wa MUNGU unaotufikisha kwenye uzima. Karibu tuendelee kujifunza pamoja, kwa unyenyekevu na upendo. — Amani Ernest Kyamba SOGH TEAM

Part 02:kugeuza nia

 Ndugu msomaji, Kabla hujaendelea na masomo haya, ningependa kusema jambo moja kutoka moyoni. Kama kuna sehemu yoyote katika maandishi yangu imeonekana kuwa kali kupita kiasi, ya kuhukumu, au isiyotoa nafasi ya kuelewana vizuri — naomba unisamehe. Kusudi langu halijawahi kuwa kuumiza, kushusha, au kujiona bora kuliko wengine. Ninachoandika kinatokana na kiu ya kumtafuta MUNGU kwa undani na kushirikisha wengine yale ninayojifunza katika safari hiyo. Hata hivyo, bado niko safarini kama wewe — najifunza, nakua, na kurekebishwa kila siku. Naomba usichukue maneno yangu kama hukumu juu yako, bali uyapokee kama mwaliko wa kutafakari, kuchunguza, na kumtafuta MUNGU kwa kina zaidi. Kilicho muhimu zaidi si mimi, bali ni ukweli wa MUNGU unaotufikisha kwenye uzima. Karibu tuendelee kujifunza pamoja, kwa unyenyekevu na upendo. — Amani Ernest Kyamba SOGH TEAM Hosea 4:6               Wana wa Israel walikuwa na sheria ya MUNGU,na walikuwa na ujuzi nayo.la...

Part 01:Kugeuza nia

 Luka 9:62 Mwanzo 19:22 Mtu anayetaka kuenda mbinguni ila anaangalia nyuma anafananishwa na mtu anayetembea kwenda mbele ila macho yake yanaangalia nyuma(yaani anatembea kinyumenyume)       sasa njia Ile ni nyembamba nayo imesonga kuelekea uzimani je mtu akiwa haoni jinsi ilivyosonga atafanikiwa? mathayo 7:14        maana kusonga Ina maana Ile njia Ina mabonde,mashimo,milima,miiba na adha mbalimbali Bila  kugeuza Nia(macho kugeuka uelekeo wa wokovu) tunakuwa ni vipofu ko miiba itatuchoma mashimoni tutatumbukia na mabonde yatakuwa ni kizuizi kwetu mno kwa kuwa Bado Nia hazijageuka(hatujazaliwa mara ya pili).        Wakati tukigeuza nia(kuzaliwa mara ya pili) tutaona tunapopaendea kwa kuwa Nia inaunda imani na imani inaunda tumaini na katika haya lililo kuu ni upendo 1 korinto 3:13. upendo ndiyo kugeuza Nia ninakozungumzia. ukigeuza Nia(ukizaliwa mara ya pili) palipo na bonde patajazwa, palipo kilima patashushwa,palipo kwaru...

Kwa nini unasita kuisikia sauti ya MUNGU?

 hint: MUNGU alimwambia Musa awahesabu Wana wa Israel hesabu 1:2.lakini si kwamba MUNGU alikuwa hajui idadi.wala sio kwamba Musa alikuwa hajui kwamba MUNGU anajua idadi ya Wana wa Israel. MUNGU anajua hata idadi ya nywele, kwenye kichwa Cha Kila mtu hapa duniani mathayo 10:30. Kwa Nini alimwambia Musa ahesabu wale watu.ni kwa Sababu ni MUNGU.anataka kupima utii na uwezo wetu wakulitendea kazi neno lake.ndo maana hata kwenye masomo yaliyopita kumhusu Adam na Hawa jinsi walivyowekewa ule wa ujuzi wa mema na mabaya.ulikuwa ni Sheria inayopima uwezo wa mwanadamu kulitii na kulisikiliza neno la MUNGU.        ili kwamba endapo wakiitii Sheria(wangesikiliza neno la MUNGU) basi wangekuwa na Uhuru na ukamilifu siku zote lakini pale tu walipokula ilimaanisha Sheria Ile ikawapinga ikawazuia.          Tukisoma vizuri tunakuja kugundua kuwa adamu na Hawa Wala hawakujua kwa Nini MUNGU aliwaambia wasile Lile tunda.lakini kwa kuwa ilikuwa ni neno la MUN...