Part 02:kugeuza nia

 Ndugu msomaji,

Kabla hujaendelea na masomo haya, ningependa kusema jambo moja kutoka moyoni.

Kama kuna sehemu yoyote katika maandishi yangu imeonekana kuwa kali kupita kiasi, ya kuhukumu, au isiyotoa nafasi ya kuelewana vizuri — naomba unisamehe. Kusudi langu halijawahi kuwa kuumiza, kushusha, au kujiona bora kuliko wengine.

Ninachoandika kinatokana na kiu ya kumtafuta MUNGU kwa undani na kushirikisha wengine yale ninayojifunza katika safari hiyo. Hata hivyo, bado niko safarini kama wewe — najifunza, nakua, na kurekebishwa kila siku.

Naomba usichukue maneno yangu kama hukumu juu yako, bali uyapokee kama mwaliko wa kutafakari, kuchunguza, na kumtafuta MUNGU kwa kina zaidi.

Kilicho muhimu zaidi si mimi, bali ni ukweli wa MUNGU unaotufikisha kwenye uzima.

Karibu tuendelee kujifunza pamoja, kwa unyenyekevu na upendo.

— Amani Ernest Kyamba
SOGH TEAM





Hosea 4:6

              Wana wa Israel walikuwa na sheria ya MUNGU,na walikuwa na ujuzi nayo.lakini pamoja na kuijua sheria,bado waliangamia kwa kukosa maarifa.

        Maarifa ni nini basi?,ni namna sahihi ya kuutumia ujuzi ulio nao,ni hali ya mtu kutambua thamani ya ujuzi.

        Watu wengi wamekuwa wanajua mambo mengi sana ya rohoni na mwilini,lakini kwa kukosa maarifa wanajikuta wanapotezwa na ujuzi walionao.ni heri wasingekuwa wanajua,maana kujua kwao kunawapoteza badala ya kuwasaidia.

       Neno linasema kuwa siku za mwisho maarifa yataongezeka!! Daniel 12:4.tungetegemea kuwa kutokana na kuongezeka kwa maarifa basi nguvu ya MUNGU ingeongezeka!!.

        MUNGU aliwapa adamu na hawa neno.lakini adui naye akaja akajaribu kutumia neno la MUNGU kupandikiza maarifa maovu kwa adamu na Hawa.

         Kutambua thamani ya ujuzi ulionao ndio tunaita maarifa,sasa adamu na eva hawakutambua thamani ya ujuzi waliopewa na MUNGU kuwa wasile mti wa utambuzi wa mema na mabaya.walichukulia rahisi tu,ndio maana tunasema walikosa maarifa kwani hawakutambua uzito wa maneno na uzito wa anayewataarifu habari za mti ule.

       Hata sasa watu wanakosa maarifa wanashindwa kutambua uzito wa habari za wokovu,uzito wa neno la MUNGU,uzito wa siku za mwisho.

        Hakuna mwanadamu ambaye Hana maarifa duniani hapa,lakini ukichagua maarifa ya Kiroho,unayafisha ya mwilini automatically.na ukiyachagua maarifa ya kimwili unayafisha ya kiroho automatically.

     Wagalatia 5:16 inasema ukienenda kwa roho hutayatimiza ya mwili,na ukienenda kwa mwili hutayatimiza ya roho.

Katika siku za sasa maarifa ya kiroho yameongezeka sana,na pia maarifa ya kimwili yameongezeka sana.je wewe unaenenda kwa maarifa gani?.

      Maarifa yanaambatana na uwekezaji.je wewe umewekeza wapi?

     Uwekezaji ni mbinu pekee inayotuwezesha kupata ujuzi.hata katika elimu za mashuleni,lazima mtu awekeze gharama (mda,Mali,shughuli za utafutaji mali) ili aupate ujuzi kikamilifu.ukikamilika kupata ujuzi unaingia katika Hali mpya ya kuubadili ujuzi kuwa maarifa.

       Wengi sana wanashindwa hapo,wanaishia kuwa wajuzi/wajuaji tu lakini si wahusika wa Yale waliyojifunza.

Katika hizi siku za mwisho maarifa ya MUNGU yameongezeka sana,lakini kwa kuwa watu wameridhika na ujuaji(wamelima ila wamesahau kulinda shamba,basi Adui anakuja usiku anapanda magugu katika shamba mathayo 13:25-30).

    Wanalima shamba kwa umakini ila wanasahau kuwa Kuna adui,kwa hiyo wanalala.sasa adui anakuja kupanda magugu.

     Watu wengi sana huwa wanaanza kwa lengo zuri,lakini mwisho unakuwa mbaya,kwa sababu katika njia njema wanayopita wanajisahau(balance ya ubinadamu kwenye kazi ya MUNGU haijakaa sawa),wakijisahau wanamwacha shetani apande maarifa yake kwenye jambo zuri kabisa.ko nje wazuri ndani wabaya kabisa kama ilivyo kuwa shamba ni shamba kwa mwonekano,ila ukiangalia ndani unakuta magugu ni mengi sana kuliko mazao.na kwa namna hiyo magugu huyasonga mazao mpaka mazao yakafa kabisa mathayo 23:25.

       Yesu akasema basi farisayo kipofu safisha kwanza ndani ili nje nayo ipate kuwa safi.kwa kuwa MUNGU hashawishwi kwa na unachojua,bali anashawishika kwamba je unakitambuaje unachokijua?,unakithaminije,unakionaje?.

     Ebrania 2:3 je tutapataje kupona tukisipoujali?,maandiko hayajasema kuujua,bali maandiko yanasema kuujali.

    Yohana 1:9-12 inasema alikuwako ulimwenguni,ila ulimwengu haukumtambua.watu walimjua ila hawakumtambua kama masihi.wao walimjua kama mwana wa seremala.mathayo 13:55.

      Hata sasa watu wengi wanamjua YESU kama nabii,na mwalimu,ni vizuri.lakini tatizo linapokuja ni kwamba hawamtambui kama kuhani wa upatanisho kati ya wanadamu na MUNGU.waebrania 9:22-28.

     Wengi Wana ujuzi wa kumjua YESU,lakini maarifa ya kuona yaliyofichika nyuma ya YESU hawayaoni.ndo maana hawathamini ukuu wake,kazi yake,huduma yake,na mamlaka yake,kwa sababu wanamchukulia kama walimu na watu wengine mashuhuri.

     Hii ni ajabu sana!!.tunasema Yale ya mababa zetu yamewekwa kuwa kama funzo kwetu ,ili tuwe na nuru katika hatua zetu kwa sasa.lakini pamoja na mafunzo yote tunayoyapata na tunapowashangaa mababa zetu,tunajua kabisa,lakini kwa kua tunajua mengi shetani ndo anakuja kupanda magugu mengi katika mashamba yetu,kwa sababu tuna mambo ya thamani,ila hatujui thamani yake,kwa hiyo tunalala! Adui anafurahi sana hapa.

        Shetani Hana mawazo yake binafsi,hana umiliki wowote binafsi,lakini anatumia mawazo ya watu kuharibu.hata YESU alipokuwa amefunga siku arobaini mara alipoona njaa ndipo mjaribu akamjia akamwambia ikiwa wewe ni mwana wa MUNGU badili jiwe hili liwe mkate.mathayo 4:1,luka 4:1---

     Akamjaribu pia kwa tamaa ya mali na kiburi.kwa kuwa YESU alikuwa ni mwanadamu,hayo ndiyo mambo ambayo yanamtesa mwanadamu sana(akiwemo na YESU ambaye alikuwa ni mwanadamu kwa wakati huo).lakini YESU alikuwa na maarifa alitambua thamani ya neno la MUNGU,akashinda.

      Kwa hiyo hapo tunajifunza kuwa, kumbe kadiri watu wanavyozidi kujua mengi ndivyo ambavyo upana wa shetani kupanda magugu unaongezeka.ko kadiri ujuzi unavyoongezeka basi na maarifa ya kuutunza ujuzi huo ndivyo yanavyobidi kuongezwa.

     "Vipi kulinda nyumba moja,na kulinda mji au nchi.inahitaji gharama kubwa sana kulinda mji au nchi.sasa adui anapata nafasi namna hii(maasi yameongezeka) kwa sababu,kwa sababu nyingi ni kwamba ulinzi haukidhi mahitaji yanayohitajika.

      Kwa nini maasi yameongezeka,ni kwa sababu ujuzi umekua sana na kusambaa kwa watu wengi Sana,lakini kutokana na ongezeko la ujuzi(shamba) shetani amepata nafasi ya kupanda magugu na mapooza mengi hivyo watu wamekwama na kuwa wanaojua tu,ila si wanaothamini wanachojua.

        Kwa kuwa magugu na ngano vimekua pamoja katika shamba,BWANA shamba akasema yaache magugu na ngano vikue pamoja tu(japo ni jambo la huzuni sana kuwa Kuna ngano zitalemewa na magugu kwa hiyo hazitazaa).lakini bwana shamba akatoa nafasi kuwa Sasa adui amepanda magugu,sasa hebu magugu yathibitishe mbegu bora ni zipi.ili mbegu zitakazozaa katikati ya magugu,zinastahili kuvuna kwani zitakuwa ni uzao imara.

     Kwa nini mimi na wewe tuwe ni mbegu ambazo zitalemewa na magugu,hebu sisi(ngano) tuyalemee na kuyafisha hayo magugu yanayotuzunguka.Bwana shamba atakuja mda wa mavuno atatufurahia na kutupa zawadi ya uzima wa milele,wakati huo magugu na ngano dhaifu(ambazo hazijazaa kabisa hata moja!!) Zitachomwa moto kwa pamoja.

      Ngano ambayo haizai ni sawa na gugu tu(mti usiozaa unaharibu hata ardhi hiyo rutuba ni bora izalishe itunzwe kuliko kukuza mti usio na faida).ko ngano dhaifu zitachomwa moto pamoja na magugu.mti Luka 3:9,mathayo 3:10.


 Kwa nini mimi na wewe tuwe ngano dhaifu??!!,hebu tujipe moyo!! Kwa kuwa kiongozi wetu aliushinda ulimwengu,na sisi tukimfuata tutaushinda ulimwengu yohana 16:33.


Barikiwa sana 

Mwalimu:Amani Ernest Kyamba

soghteam.org 

Let's do GOD'S work together 



      


      

      

      

          

       

     



Comments

Popular posts from this blog

A.Kuweza kulitendea kazi neno la MUNGU

Je kwa nini namna ile?

Mwamuzi(short notes)