Kuweza kulitendea kazi neno la MUNGU
Part 01: Kuujua Mwamba, msingi, nyumba.
Teacher: Amani Ernest kyamba.
From SOGH ministry.
Neno linapotamkwa na mtu linatamkwa kwa lengo la watu kusikiliza. Ndo maana mtu akiwa anaongea peke yake tutamwona ni kichaa kwa Sababu anaongea peke yake bila kuwepo msikilizaji. Basi neno la MUNGU Lina wasikilizaji ambao ndio sisi. Walengwa wakubwa wa neno la MUNGU ni sisi wanadamu. Yeye MUNGU wa mbinguni anatuonya na kutujenga kwamba tujue Cha kufanya kupitia neno ambalo ndilo amri yake. MUNGU wa mbinguni anachohitaji ni sisi kulitendea kazi neno lake. mathayo 7:24-27.
Kutoka katika maneno haya ya YESU Kristo tunajifunza mambo yafuatayo:
Mwamba ni MUNGU Zaburi 78:35, zaburi 89:26. Kutoka katika hii zaburi 89:26 tunaona kuwa mwamba ni MUNGU mwenyewe na pia nyumba ni wokovu tulio nao. Na msingi ni kristo 1 korinto 3:11, mjenzi na fundi wa maisha ya mkristo ni roho mtakatifu.
Unapoamua kuokoka tu pale unakuwa na msingi wa wokovu ambao ni YESU. Sasa wengine wanasema wameokoka ila hawamfuati YESU ko hawana msingi wa wokovu na wanataka waijenge nyumba. Roho mtakatifu atakuja kwa mtu mwenye msingi tu, yaani aliyeunda Nia ya kumfuata YESU Kristo, maana huko ndo kunaitwa kuokoka. Ukishaweka msingi katika Mwamba MUNGU wa mbinguni basi ndipo utahitaji ROHO mtakatifu ambaye atakusaidia kuuumba wokovu yohana 16:13. Hapa inamaanisha kwamba pasipo ROHO mtakatifu tutakuwa hatuna wokovu uliokusudiwa na MUNGU baba.
YESU Kristo alikuja duniani kuuweka msingi wa wokovu katika Mwamba ambao ni MUNGU. Torati kwa mara ya kwanza kabla YESU Kristo hajaja iliwataka wajenge juu ya Mwamba ambao ni MUNGU. Wakajenga wenyewe kwa kuutiisha mwili pasipo msaidizi Wala msingi wakawa na nyumba dhoofu zilizobomoka zenyewe baada ya kumaliza kuzijenga. Na hiyo ndiyo maana mwili uliwatawala na wakawa waasi kwa MUNGU sana maana pale tu upepo na Hali ya hewa ilipobadilika walianguka chini. Wakawa wepesi kupoteza kwenye dhambi. Kumbe hata sisi lazima tujitafiti kwamba je tunaishia kwa kweli au kwa uongo? Kama sivyo inavyotakiwa basi tugeuke na kuamua kuujenga msingi tena...
Hebu tuone jinsi gani tutajenga wokovu katika msingi (YESU). Watu wengi tumebahatika kuujua Mwamba na ndio maana wapo wengi sana (dini nyingi sana zinazojenga kwenye Mwamba ambao ni MUNGU wa mbinguni), lakini shida ni kwamba zinajenga nyumba kwenye Mwamba bila kuweka msingi Wala msaidizi. Huu ni mfano na Wana wa Israel waliokuwa wameijua Sheria tu pasipo YESU Kristo Wala ROHO mtakatifu na ndio maana dini ni nyingi na pia maovu ni mengi sana kwa kuwa hakuna ukamilifu na utimilifu wa njia ya uzima wa kweli.
Hebu tuone ni kwa jinsi gani tutaweka msingi wa wokovu mkuu namna hii:
Kwanza ni kwa kumwamini YESU Kristo kuwa BWANA na mwokozi wa maisha yetu sawa sawa na yohana 3:16, warumi 10:9. Kuamini sio tu kukubaliana au kukubali Bali ni kukubaliana na Yale uliyoyakubali yaani kuweka uhakika kwa yatarajiwayo na kuwafanya yasiyoonekana ila yapo yaonekane ebrania 11:1. Kumwamini YESU Kristo ni pia kuamini kazi zake na maneno yake na njia zake na maono (kazi yake?) yohana 10:38. Kumwamini YESU Kristo ni kukubali kubadilisha mtazamo wa dhambi na kuvaa ule wa haki kama YESU Kristo aliokuwa nao ko ni kukubali gharama za wakovu wa YESU ndiyo msingi wa imani na wokovu tunapaswa kuwa nao. Msingi ni mahali panapotegemewa na nyumba sana kwelikweli maana ukiwa na msingi dhaifu wokovu hautakuwa imara kabisa.
Kwanza fahamu zetu na akili zetu ziwaze kuhusu MUNGU wa mbinguni, tuwe tayari ndani ya mioyo yetu kusikiliza maneno ya YESU Kristo bila kujikwaza au kutoamini (kutoyatendea kazi). Yohana 6:68, akina Petro walikuwa wanaamini na kuwa tayari kusikiliza na kufanya neno lolote kwa ajili ya YESU Kristo, hata kukubali kufa nae yohana 11:16. Huo ndo msingi ambao YESU Kristo alikuwa anataka kuujenga kwa wanafunzi wake. Wakawa tayari sana kweli kwa ajili yake na wakajitahidi kujifunza na kuwa tayari kumsikiliza na wakamjua kuwa Yeye ni nani na wakamheshimu wakamuogopa sawasawa na walivyompokea.
Hi ni hatua itakayomwita msaidizi ambaye ni ROHO MTAKATIFU aje kumbadilisha mtu na kuujenga wokovu. Kwani pamoja na yote, YESU Kristo alijiridhisha nao lakini Bado walihitaji msaidizi wa kuwasaidia kuitimiza Yale waliyokuwa wanawaza na mazuri yote kama kufa kwa ajili yake ndo maana Petro alimkana YESU mbeleni alipotambulika kuwa mwanafunzi wake japo mwanzo alikuwa tayari. Ni wazo zuri ila halikuwa na msaidizi ambaye ndiye ROHO mtakatifu. Ndo maana baada ya kuwa na roho mtakatifu akawa na ujasiri mwingi hata kufa kwa ajili ya YESU Kristo mwokozi wetu. Kwani mwanzoni ulikuwa Bado mda wa nyumba kujengwa Bali walivuviwa ROHO mtakatifu yaani uwepo wa msingi uliashiria uhitaji wa msaidizi wa kujenga nyumba imara ambayo ni wokovu.
Ko msingi ni utayari wa kumtii na kuwaza makubwa na mapenzi ya MUNGU na pia kuwa na msukumo wa kumtumikia yeye. Ko mitume walikuwa na msingi imara kwelikweli ndo maana kazi zao zilikuwa kubwa sana kama ilivyo kwamba msingi ukiwa imara sana tutajenga nyumba kubwa yenye utukufu sana. Wao walimtegemea YESU kwa mioyo yote na walimpenda sana kiasi Cha kufa ndio maana kazi Yao ilikuwa kiasi cha kufa. Je sisi tunamwonaje YESU Kristo, je tunawaza Nini juu ya maagizo yake?, je tunamtegemea kweli YESU, je tupo tayari kuchukua gharama kumfuata YESU? Je Nini Cha kututenga na YESU Kristo maishani mwetu? Haya tujiulize wenyewe kama kweli tuna msingi imara kwamba tukijenga nyumba kwa ROHO mtakatifu shetani hatatutetemesha.
Petro alimpenda na alimwamini YESU Kristo sana kuliko kawaida Hadi akamfata kwenye maji akawa mdadisi kwa YESU Kristo, akawa wa karibu na YESU Kristo hapo ndipo YESU alipojua kuwa Petro alimpenda kuliko mitume wote yohana 21:15. Na pia alimwambia kupitia yeye petro ndipo litajengwa kanisa milango ya kuzimu haitalitetemesha mathayo 16:18 yote ni kwa kuwa Petro alikuwa na msingi imara kuliko mitume wote na alimpenda sana YESU Kristo mwokozi. Zipo dini nyingine zimewekeza imani Yao kwa mitume wasio YESU Kristo mwokozi. Maana ya msingi Ina maana kuwa sisi tunataka kumwona MUNGU kupitia YESU Kristo kama ilivyo kwamba kukiwa na Mwamba mzuri ila msingi mbaya hamna tofauti na watu walipojenga kwenye mchanga (Dunia).
Kwa kuwa Mwamba utaonekana pale tu Kuna msingi imara wa kuubeba wokovu tulionao. Uimara wa YESU Kristo ni kwamba yeye pekee ndiyo njia ya kumwona baba MUNGU Wala hakuna nyingine yohana 14:6. Ko YESU Kristo ndiye njia kwanza yaani kamwe hutaweza kuona uimara wa Mwamba MUNGU pasipo msingi imara (YESU Kristo). Lazima umfuate YESU kikamilifu kwa yote ndipo umuone MUNGU. Sasa hizo dini zingine ziangalie je zinafwata mtume wao mkuu kwa namna yote au Kuna mambo sio makuu ya kufwata, basi sio msingi imara huo. Kama tujuavyo kuwa msingi mzuri unatoka kwenye Mwamba hukohuko. Ona je hao msingi wao ni wa mbinguni au ni mwanadamu aliyeuanzisha?
YESU alitoka mbinguni na ni mwana wa MUNGU wa mbinguni, tena ni neno la MUNGU yohana1:1. Ko kumbe YESU Kristo ndo Msingi pekee wa kumwona MUNGU maishani mwetu. Hakuna wengine maana hao ni Wana asili ya kibinadamu pure kwa mfano akina Musa (wayahudi), Muhammad (Islamic), Gandhi (kwa wahindi na wachina) hayo yote yataitwa mafundisho ya wanadamu. Hawa wote inabidi tuwafanye wamjue YESU Kristo ili juhudi zao za kumuona MUNGU ziwe kweli kwelikweli, la sivyo upotevu upo nao. Na hii ndiyo kazi tuliyopewa na YESU Kristo tuifanye baada ya kumjua yeye.
Sasa tuone kuhusu msaidizi wa kutusaidia kuijenga nyumba (wokovu). Tuna madhaifu mengi sana kwenye maisha yetu ndo maana tunamhitaji ROHO mtakatifu awe na sisi ili atushindie warumi 8:26. Yohana 16:13, roho mtakatifu ndiye anayetuweka kwenye kweli yote ya MUNGU. Yeye ndiye anayetupa usahihi wa kufanya mambo ya kiroho. Maana ya MUNGU yote ni mazuri ila je ni wakati sahihi? Hapo ndipo ROHO mtakatifu atahusika. Tunajifunza kwa sauli ambaye alitaka kumtolea sadaka MUNGU wakati MUNGU alimwambia ateketeze amaleki yote ko hakuitii sauti ya MUNGU na kwa Hilo BWANA akamkataa 1 samweli 15:1-24. Kutoa sadaka ni jambo zuri lakini halikutoka kwa MUNGU kwa wakati huo ko sauli hakuwa na ROHO mtakatifu ko alifeli.
Yeye roho mtakatifu atatufanya kuwa watakatifu kwelikweli kwa kuisikia sauti yake kwamba Nini tufanye. Tunaona kuwa ROHO mtakatifu aliwakanya mitume wasiende baadhi ya miji mitume 16:6. Yeye ndiye anayepanga maisha ya wokovu ya kwetu kwamba madirisha na milango ikaaje? Ni roho huyo. Hata Petro alienda kwa Cornelius kwa kuwa ROHO alisema naye ko hakukurupuka. Ko tusipokuwa na roho mtakatifu tunakuwa wakurupukaji, na tutashindwa hakika hii vita ya utakatifu kwani shetani atatuangusha. Lakini tukiwa naye ROHO mtakatifu tutamshinda shetani hakika kwani tutafanya mambo sahihi kwa mda sahihi. Ko tutakuwa watu sahihi na pia Wana wa MUNGU kwa kuwa nyumba itakayobaki mpaka mwisho na kuvumilia mafuriko ya Dunia ndo itakayookoka.
Haiwezekani pasipo ROHO mtakatifu kujenga na sisi huu wokovu. Wapo wengine hawana msingi imara ila wanataka kujenga nyumba kubwa kuliko uwezo wa msingi. Ole wao kwa kuwa kazi zao (nyumba) zitawaangusha weneywe kwa kiburi, majivuno, dharau kwa kuwa msingi ni dhaifu na hivyo mafuriko na upepo vitaipiga nyumba. Haijalishi wokovu una thamani namna Gani maana hiyo thamani itakuwa haijaundwa na roho mtakatifu, kwa kuwa ROHO mtakatifu anawekeza sawa na msingi tuliounda (atajenga kidogo na kutuachia tujijengee wenyewe hivyo nyumba itakuwa dhaifu kweli kweli). Bado tutashindwa kwa kuwa hatuna msingi. Ko kushinda kwetu na wokovu wenye nguvu utatokana na Mwamba imara, msingi imara, msaidizi imara. Lakini inabidi sisi tumshinde shetani hakika. Naam tutashinda kwa jina la BABA, MWANA, NA ROHO MTAKATIFU, amen!!!!
# A.E.Kyamba.
Mr Sogh.
Comments
Post a Comment