Part 01:Kugeuza nia

 Luka 9:62

Mwanzo 19:22

Mtu anayetaka kuenda mbinguni ila anaangalia nyuma anafananishwa na mtu anayetembea kwenda mbele ila macho yake yanaangalia nyuma(yaani anatembea kinyumenyume)


      sasa njia Ile ni nyembamba nayo imesonga kuelekea uzimani je mtu akiwa haoni jinsi ilivyosonga atafanikiwa? mathayo 7:14

       maana kusonga Ina maana Ile njia Ina mabonde,mashimo,milima,miiba na adha mbalimbali

Bila  kugeuza Nia(macho kugeuka uelekeo wa wokovu) tunakuwa ni vipofu ko miiba itatuchoma mashimoni tutatumbukia na mabonde yatakuwa ni kizuizi kwetu mno kwa kuwa Bado Nia hazijageuka(hatujazaliwa mara ya pili).

       Wakati tukigeuza nia(kuzaliwa mara ya pili) tutaona tunapopaendea kwa kuwa Nia inaunda imani na imani inaunda tumaini na katika haya lililo kuu ni upendo 1 korinto 3:13.

upendo ndiyo kugeuza Nia ninakozungumzia.

ukigeuza Nia(ukizaliwa mara ya pili) palipo na bonde patajazwa, palipo kilima patashushwa,palipo kwaruza patalainishwa.si kwamba patakuwa pamenyooshwa,au pamelainishwa au pamejazwa Bali tutapita mazingira magumu kama rahisi tu.kwa kuwa upendo wetu kwa MUNGU ni waajabu.luka 3:4-5.

Tujapopita kwenye bonde la uvuli wa mauti hatutaogopa kwa kuwa yeye aliye upande WETU ni mkuu kuliko yote.kwa nini hatutaogopa,ni kwa Sababu macho yanaiona mbingu ile,ko njia ndo hii haijalishi ni njia mbaya sisi hatutaona njia tutaiona mbingu.

      sasa macho yako yakiwa yanaiona dunia  ina maana ukidondoka utasema safari ni ngumu na matumaini yanajengwa na unaona wapi,ukianguka afu unaitamani dunia,itakutengenezea manung'uniko kwamba mbona MUNGU wale wa dunia wanafanikiwa? Afu mimi sifanikiwi?

         unasahau kuwa njia ya dunia ni pana wengine wanaenda wengine wanarudi lakini wote uelekeo wao ni upotevuni,kama ilivyo kwamba wengine wanafanikiwa kwa nguvu za giza(wanaenda )na wengine kwa juhudi zao(wanarudi),lakini wote hatima yao ni upotevuni kama hawajamuamini YESU kristo.

Tukisoma kwenye kitabu Cha mathayo 7:13 inasema habari ya vipengele viwili kwamba kuna lango,afu kuna njia.

       YESU Kristo ndiye njia nyembamba ambayo ndiyo inatufikisha katika kweli na pia uzima yohana 14:6.


        LAKINI HEBU TUJIFUNZE  SIRI MOJA ILIYOFICHIKA INAITWA LANGO/MLANGO

      kabla haujaanza kupita kwenye njia jambo la kwanza ni kufungua mlango.ufunuo wa yohana 3:20.njia(YESU) ipo mlangoni mwako,anatamani ufungue mlango ili aingie kwako,ili pawe na muunganiko kati ya mlango na njia.

      ukisipofungua mlango(nia yaani kujikana na kuamua kumfuata YESU) ina maana mlango haujaungana na njia,bado kuna mahali hamjavaana na YESU Kristo vizuri.

       ko ili uingie katika njia nyembamba ni lazima ufungue mlango mwembamba ndani ya moyo wako(maamuzi kamili ya kujikana na kuamua kumfuata YESU katika njia yake ya utakatifu) hapo ndipo utaingia katika njia nyembamba.

       umeingia katika njia nyembamba? Jiulize ndugu yangu,maana lengo kuu ni kwamba wote tuingie katika uzima ambao ndiye YESU.

Uzima duniani na tena uzima wa milele mbinguni.

Barikiwa sana.

Efeso 4:3-6.



SOGH team.

let's do GOD'S work together 💪.

SOGH A.E.Kyamba

0768441831.




Comments

Popular posts from this blog

A.Kuweza kulitendea kazi neno la MUNGU

Je kwa nini namna ile?

Mwamuzi(short notes)