Usijiulize ulize
hint: MUNGU alimwambia Musa awahesabu Wana wa Israel hesabu 1:2.lakini si kwamba MUNGU alikuwa hajui idadi.wala sio kwamba Musa alikuwa hajui kwamba MUNGU anajua idadi ya Wana wa Israel.
MUNGU anajua hata idadi ya nywele, kwenye kichwa Cha Kila mtu hapa duniani mathayo 10:30.
Kwa Nini alimwambia Musa ahesabu wale watu.ni kwa Sababu ni MUNGU.anataka kupima utii na uwezo wetu wakulitendea kazi neno lake.ndo maana hata kwenye masomo yaliyopita kumhusu Adam na Hawa jinsi walivyowekewa ule wa ujuzi wa mema na mabaya.ulikuwa ni Sheria inayopima uwezo wa mwanadamu kulitii na kulisikiliza neno la MUNGU.
ili kwamba endapo wakiitii Sheria(wangesikiliza neno la MUNGU) basi wangekuwa na Uhuru na ukamilifu siku zote lakini pale tu walipokula ilimaanisha Sheria Ile ikawapinga ikawazuia.
Tukisoma vizuri tunakuja kugundua kuwa adamu na Hawa Wala hawakujua kwa Nini MUNGU aliwaambia wasile Lile tunda.lakini kwa kuwa ilikuwa ni neno la MUNGU ilibidi washike tu.na kutunza Hilo agano la Sheria walilopewa na MUNGU.
sisi Sasa tumekuwa na tabia ya kumuuliza MUNGU kwamba kwa Nini umesema nifanye hivi? Na maswali mengi mno tunamuuliza MUNGU.tunamfanya MUNGU aonekane sio mkamilifu kwetu kwa imani zetu ndogo na ndio maana hatupati kufikia kukamilishwa na yeye.
mwanadamu hajapewa Uhuru na MUNGU wa kumfanya MUNGU amsikilize ila amepewa Uhuru wa kumsikiliza MUNGU tu.na kutenda mambo ambayo yeye MUNGU anataka tufanye.
ili MUNGU akusikilize Cha kwanza ni lazima wewe mwenyewe uanze kumsikiliza yeye.
musa alisema na MUNGU na kuzungumza na MUNGU kama mtu azungumzaye na rafiki yake wa karibu.kutoka 33:1.kilicho mpa kibali Musa Cha kuzungumza na MUNGU kwa namna hiyo ni kwa Sababu Musa aliweka kipaumbele kwanza kumsikiliza MUNGU zaidi bila kuuliza uliza Wala bila kujitetea.
haya hesabu 20:1 Musa akakosea kwa MUNGU na kwa watu wake.ukiendelea mbele unakuja kukuta kuwa ghafla MUNGU alipunguza mawasiliano na ule urahisi wa yeye kuongea na musa.akaanza kumrudisha kwenye ukaribu wa kwanza kabla hawajawa marafiki.
kilichomfaya Musa akosee ni kwa Sababu alizoea neno la MUNGU alalifanya liwe kama neno lake.MUNGU alimwambia kwamba apige mwamba utoe maji afu yeye akapiga mwamba kama yeye ndiye aliyesema.akajifanya MUNGU katikati ya Israel.alijiinua musa.akamkosea MUNGU kwa kuwa Musa alitaka kuchukua utukufu wa MUNGU.
sisi pia tuna ole hii mahali pengi tunapoanza kutumiwa na MUNGU tunaanza kuchukua utukufu wa MUNGU na kujipa wenyewe kwa kujiinua nakusema kam"Mimi ndo niliyefanya haya yote"..Mimi pekee ndiye mtu wa MUNGU njoo kwangu".Mimi ndiye pekee naisikia sauti ya MUNGU"ole!! Kujiinua huleta kiburi na kiburi huleta anguko.be careful!!.
musa alikuwa rafiki wa MUNGU kwa kuwa alimsikiliza MUNGU kwanza ndipo MUNGU Naye akaanza kumsikiliza na yeye Musa kwa mapenzi yake mwenyewe.
inashangaza kwetu sisi tunataka kumpa MUNGU maswali akati huo hakuna tulichofanya chochote Cha kuugusa moyo wake
si Musa aliyemwambia BWANA na kuomba kumuuliza.bali ni MUNGU anayetupa nafasi ya sisi kumuuliza yeye katika mambo ya wokovu wetu.sio sisi kabisa.
tunataka kula kama watu wazima akati sisi ni watoto wadogo ko lazima tutambue Nini inapaswa tufanye katika mda tulionao
alipokosea Musa ndipo hapo hapo nafasi yake ya kufika kanaani ilipotea.
nachojaribu kuzungumza ni kwamba tujitahidi tumwendee MUNGU kama MUNGU sio kama mwanadamu.tukimwendea MUNGU kama mwanadamu tutapotea hakika.
tukimfanya MUNGU aende kwenye mifumo yetu tuliyojiwekea sisi badala ya sisi kwenda kwenye mfumo aliotuwekea sisi hakika tutapotea.
nini Cha kufanya ni kutenda alivyosema MUNGU pasipo kuingiza utashi wetu hata kidogo hapo ndipo MUNGU atatufanya rafiki.
#kutii na kulisikiliza neno lake
Isaya 66:2
Mtu mwenye hofu ya MUNGU ndiye yeye anaye mwangalia.
tusilewe na huduma au Mali tukamfanya MUNGU wa level zetu.musa alikosea mara moja tu akasamehewa ila hakuingia kanaani.ko tutumike kwa kujishusha kwa MUNGU na kumpa utukufu yeye na kumsikiliza na kumpenda na kadiri tunavyoinuliwa ndo tuzidi kushuka zaidi na zaidi hapo kweli tutakuwa rafiki wa MUNGU.tusikilize na kutenda bila kuuliza uliza
SOGH team.
Mwalimu:Amani Ernest Kyamba.
This is a SOGH.
let's do GOD'S work together 💪
Comments
Post a Comment