PART 01:HATUA ZA UKUAJI
Mwandishi:Amani Ernest kyamba. SOGH Team. MUNGU wa mbinguni alipoanza kuumba mbingu na nchi,dunia ilikuwa ukiwa,tena utupu tena giza lilitanda juu ya vilindi vya maji.MUNGU akaanza somo la uumbaji kwamba yeye awezaye yote angeweza kuijaza Dunia yote kwa siku moja au wakati mmoja tu.angeweza kuumba vyote kwani yeye anaweza vyote.akatoa somo kwetu kwamba katika kujenga,Mda ni kipengele cha muhimu zaidi. Pia katika technology ya ufundi wa ujenzi wa nyumba.mtu anaweza kuwa na gharama nzima na maandalizi mazuri ya ujenzi,lakini akiwapelekesha mafundi wake wamalize ujenzi mzima wa nyumba kwa wiki moja.inawezekana.lakino asilimia za uimara wa nyumba hiyo unakuwa mdogo sana .na labda yajapotokea mafuriko,pepo,na mabadiliko ya Hali ya hewa,hiyo nyumba itaanguka,au yaweza kuanguka hata kabla haijamaliziwa kujengwa. Yote hiyo inasababishwa na ujenzi kutokuwa na hatua. MUNGU angeweza kuumba wanadam...