Part 01: imani na akili

 Mwalimu:Amani Ernest Kyamba 

SOGH Team

 


Ni mwendelezo wa maelezo yaliyopo kwenye somo la ubatizo,utatu mtakatifu,na sabato.na hili neno la MUNGU zuri la kiroho kabisa litatusaidia kushinda na kushinda zaidi ya kushinda.katika hili,kama tulivyojifunza kwenye masomo yaliyopita namna ya muunganiko kati ya sheria na neema,sasa tunaenda kujifunza Tena kuhusu akili na imani.

    Karibu sana mtumishi mwenzangu.twende pamoja.


     Kwanza kabisa nitoe ushuhuda unaoambatana na shukrani kubwa sana kwa MUNGU.kwa kuwa mwaka 2024, mwezi wa tatu niliumwa ugonjwa mbaya sana unaitwa malaria 🦟.

      Ulianza kama maumivu ya kichwa ambayo yalianza kama utani, siku ya kwanza nikajipa moyo kwamba nikinywa maji afu nikilala nitapona asubuhi yake.kesho yake ugonjwa ukawa zaidi nikajikaza nikaenda na kazini Tena lakini kichwa kilikuwa kinauma sana,sijawahi umwa kichwa kwa namna ile.

nakumbuka hiyo siku nikalala chumbani hapo kwa pastor maana nilijihisi vibaya ,joto Kali,jasho yaani ni homa mfano wa mtu aliye kwenye sufuria anachemshwa. Basi nikaanza kuomba MUNGU,maana nilianza kuhisi Hali tete.maombi yangu hayakufanya jambo lolote kwenye Ile homa na kama nisingepelekwa hospitalini maybe ningekufa kwa malaria maana ilikuwa ni kama tayari imepanda kichwani(kama ambavyo huwa wanasema).ko malaria ilikuwa imepanda kichwani kweli kweli.nakumbuka nilikuwa naomba kwa MUNGU lakini kwa namna ambayo hata Mimi nilikuwa sisikii nayoomba.

        hatimaye nikapelekwa hospital na nikasaidiwa na watumishi wa MUNGU ma doctors na nurses,nilikimbizwa hospital na wazazi wangu na nililazwa  Hali sijitambui kabisa nakumbuka nilikuwa ni kama sijazimia ni kwamba mwili ulipoteza mahusiano kati yake na mazingira kabisa.japo ni kama nilihisi,maana kama harufu ya bajaji iliyonibena na jinsi nilivyobebwa na machela ya pale hospital.

         first of all ni kwamba namshukuru MUNGU kwa kuwa alinipa kibali Cha Mimi kupona maana kama ningekufa sijui!! Maana 100% nilikuwa Sina kitu kwenda mbinguni, namshukuru MUNGU niliepuka kifo na pia mauti.maana kifo kama ilivyo ada na mauti ni kifo Cha mwenye dhambi.

       ko hata wakati mwingine tuwe tunapeleka hoja yenye nguvu kwa MUNGU kwa kipindi ambacho tunaishi kwa imani ithibitishwayo na matendo (injili na uzima) kwamba MUNGU aweza kuzuia kifo Cha watu wasio haki kabla hawajapata wokovu.luka 2:25-29 maana MUNGU wa mbinguni aliweka ahadi kwa Simeoni kwamba hataona mauti kabla hajamwona YESU maadamu amezishika vizuri njia za MUNGU.

          kumbe na sisi kwa jinsi tulivyo na mamlaka na haki kwa njia ya imani ya matendo(tukiwa tumekazana na MUNGU kweli kweli kumtumikia na kufanya kazi yake kuu) tunaweza mwambia hoja kwamba MUNGU azuie vifo vya wasio haki mahali Fulani tunapaendea ili kama kufa ni haki ya kilicho hai kwa Sasa basi kwa kuwa Kuna kazi inapaswa ifanyike basi hiyo haki isitimie mpaka mtu apate haki ya uzima maana yeye YESU hataki hata mmoja apotee Bali wote wafikilie toba 2 Petro 3:9.

          anahitaji watu wenye hoja kama hizo YESU, na kama ni mapenzi yake hakika atatusikia.kwa hiyo tujitafakari sana na kujichunguza tukumbuke tulipokosea tutubu na kujenga upya maana tukigeuza Nia yeye ataturudia sisi kama alivyosema mlezi(pastor) kwa habari ya Nia kwamba kuokoka ni kugeuza nia.moja baada ya nyingine yaani kufanywa upya Kila siku ko tukiokoka tuna nafasi ya kuokoka Tena na Tena.

      Ko wakati mwingine tunaomba MUNGU azuie ajali na vifo yeye YESU anauliza kwa ajili ya nini? Maana hata akizuia watu wale watakufa kwa mauti tu je tunataka azuie ajali kwa ajili yetu tu au tunawaza kwa ajili ya wengine?.


      basi maombi niliomba kwa imani lakini ili niwe na haki ya kuishi kwa imani lazima niwe na haki.“Imani isiyozaa matendo ya haki hubaki kama ufahamu wa akili tu, bila nguvu ya kiroho.

       Ko imani na (matendo) na haki ni vipengele viwili ambavyo havitengani kwa namna yeyote.kuna mahali nimeandika kuhusu 1 korinto 13: 1 kwamba nijapofanya matendo ya upendo pasipo haki ya kuwa na upendo si kitu chochote nachofanya,.ni BURE..

      kutokana na maelezo hapo juu ni kwamba ili kuishi kwa imani lazima kwanza uwe na haki.na pia haki yangu inapatikana kwa imani,ko vipengele viwili(vitatu) haviwezi kuachana.

     na Mimi nilipokuwa naumwa niliomba kwa imani kabisa  asilimia 100 ila nilipofeli ndo maana sikupokea uponyaji ni kwa Sababu sikuwa na haki  (japo Wakati mwingine Mungu huruhusu hali fulani ili kutufundisha, hata pale tunapokuwa na imani.)kwa kuwa imani ilikuwa hainipi haki ya kumwomba MUNGU na kupata uponyaji.ko imani nayo ila haki Sina ko imani inaitwa akili kwa hapo.kwa sababu wengi wanakiri kuwa na imani lakini ili imani ifanye jambo lolote ni lazima kuwe na haki.haki ni kibali unataka kupona?unastahili kupona?,kwa nini upone,unafanya tendo gani ili imani yako ikuponye?(mwanamke yule aliyevuja damu alimtafuta YESU katika makutano,akasema nikigusa pindo la vazi la YESU nitapona.je wewe umejipangaje.je tatizo lako ni kwa ajili ya utukufu wa MUNGU au ni changamoto za kidunia(walikufa wengi ila lazaro kifo chake kilikuwa ni kwa ajili ya utukufu wa MUNGU)

     “Imani hutoka kwa neno la Mungu; akili hulipokea neno hilo, na haki hulidhihirisha kwa matendo".

   formati ya maisha ya kiroho kama formati ya mtihani) lakini ili uyajibu maswali na Hali halisi lazima, Hadi neno imani litokee kunakuwa na vitu viwili vinavyoungana kuumba imani navyo ni

 akili+haki=imani.

#wengine tutaanza kujiuliza haki ipi Tena akati umesema imani na haki havitengani? 

~je Haki iliyopo hapo kwenye equation(mlinganyo) ni ipi?

~ni Nini maana ya sawasawa(=) kwenye huo mlinganyo?

~maana Kuna wengine Wana haki na Wana akili ila hawana imani akati tumeshasema kuwa akili+haki=imani?

~je neno linalosema mwenye haki wangu ataishi kwa imani lilikuwa Lina maanisha nini ebrania 10:38?

kusitasita kunatokana na Nini kwenye ebrania 10:38? Ni kwa Sababu akili na haki havijaunganishwa kuwa imani Bado

~ulisema ulipokuwa unaumwa kwa kuwa hauna haki basi imani Yako ikawa akili.je akili ni Nini?




      na maswali mengi kama hayo na basi MUNGU atusaidie sana tuyajibu na kuyafikia kwa usahihi nauhakika kwa kuwa akili ndo inayotufanya kuyajua mafumbo ya MUNGU (formati ya maisha ya kiroho kama formati ya mtihani) lakini ili uyajibu maswali na Hali halisi lazima uwe na imani.

Yo!! 👋 👋  Let's go 


#ko mlinganyo sahihi ni upi?

Akili+haki=imani>>>haki ambayo MUNGU anaizungumzia kwamba kwa hiyo basi hatutatengana na imani na tunahesabiwa haki kwa njia na imani.warumi 5:1

##jambo la kwanza ni kwamba ili haki isitenganishwe na imani ni kwamba akili na haki lazima viungane kwa pamoja.

Je akili na haki ni aina Gani? Maana bila shaka wengi tunaweza tukawa tumekwamia hapa.

Twende pamoja.

 One formula:akili inapokea mambo ya rohoni,imani inadhihirisha mambo ya rohoni.


AKILI NI NINI?

       kabla ya yote tunapaswa tujue kwamba MUNGU alipomuumba adamu alimuumba akampa na akili.akili ni kama memory card,ni sehemu ya kutunza mambo yote tunayoyaona na kuyasikia na kujifunza na kuyajua.akili sio kwamba inakuwapo kichwani kwenye ubongo,akili ipo pamoja na pumzi ya MUNGU aliyompulizia adamu ko inamaanisha akili ni uwanda wa kiroho kabisa na sio mwilini.

      inaweza kusemwa IPO kichwani kwenye ubongo ni sawa kabisa kwamba akili na ubongo vina mahusiano.lakini akili yenye mahusiano na ubongo inamwezesha mtu kuishi sawa na taratibu.ndo maana malaria ikipanda kichwani mtu anakuwa kichaa kabisa,ko ni hakika kuwa ubongo ndiyo funguo ya akili,yaani kupitia ubongo akili zetu zinaonekana. Ubongo hauna akili,kwa kuwa akili si jambo la kimwili,ni jambo la kiroho kabisa,ila ubongo ni funguo ya sisi kuonekana akili zetu.

     ubongo unaongoza mwili wa binadamu na shughuli zote zipasavyo na pia ndo udhihirisho wa akili ya mwanadamu.ubongo ni kifaa cha kubebea akili.ko ubongo ukipata shida moja kwa moja akili itakuwa na shida!!.

       akili ni pumzi ya MUNGU iliyomo ndani ya mtu.ndo maana wanyama wote wapo hai ila aliyepuliziwa pumzi ya MUNGU ni mmoja tu ni mwanadamu.ndio maana wanyama Wana ubongo ila hawana akili (Tofauti na mwanadamu aliyeumbwa kwa mfano wa Mungu, wanyama hawakupewa uwezo wa kiroho wa kumtambua Mungu kama mwanadamu)kwa kuwa fahamu zao hazina pumzi ya MUNGU.ni mwanadamu tu aliye na pumzi ya MUNGU.

      na pumzi hiyo ni akili aliyonayo MTU.

       ili kuithibitisha akili ya mwanadamu MUNGU akaweka mti wa ujuzi wa mema na mabaya pale edeni,ule mti ulikuwa unaithibitisha maamuzi ya mwanadamu na akili yake.asili ya akili ni roho(MUNGU).na ndo maana MUNGU alipomwumba mwanadamu tu mwanadamu aliishi katika ROHO akamwona na MUNGU akija kutembea jioni kila siku.akamwona MUNGU akauona na utukufu wake MUNGU kwa kuwa adamu alikuwa ni kiumbe wa mwili katika roho.yeye MUNGU ni ROHO na kwa kuwa akili ya Adamu ni ya rohoni alimwona MUNGU na kumwabudu na kumtumikia katika ROHO.

        lile tunda aliliweka MUNGU mwenyewe.si ajabu yeye anaumba na anafisha anainua juu na anashusha chini 1 samweli 2:7.hafanyi tu.ila anafanya sawasawa na neno lake analotuambia tukikosea anatushusha sawasawa na neno lake na tukipatia anatuinua sawasawa na neno lake.kama alivyomwambia adamu na Hawa kuwa ukila tunda nitakushusha na usipokula likithibitika neno langu utashinda na nitakuinua ila Adam alifeli mwe!!😔.

      maana hatujui vipi ingekuwa kuwa adamu amezaa mtoto kabla hajala tunda yule mtoto angekuwa na pumzi halali ya MUNGU.maybe tunda lilikuwepo kuwajaribu Adam na Hawa kabla hawajazaa, hahaha!! Haya ni maneno yangu na najua kuwa nina roho wa MUNGU ko take it as it.

      ko kama tunavyoumba sumu na pia dawa MUNGU pia alifanya hivyo hivyo kwa mwanadamu ila mwanadamu akachagua sumu.

   akili iliyokuwamo kwa mwanadamu ilikuwa njema.na inapokea mema tu.inawaza mema tu na inatenda mema tu,na pia Ina mema tu.ni akili haina mfano.

#je akili njema ya Adamu ilishindwaje?

Warumi 10:2.walimwabudu MUNGU ila hawakuwa na maarifa.

#maarifa ni neno la MUNGU mithali 2:6 kwa MUNGU hutoka maarifa na ufahamu.

Adamu alimjua MUNGU vizuri sana na alikuwa na neno la MUNGU kamilifu

Tunasema neno linasema watu Wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa.ni kweli.

     maarifa ni kusimama kwenye neno la MUNGU tu ndiyo maarifa.

#kama nilivyosema kuwa akili ni memory card.basi ilitunza yasiyopasa.lazima akili zetu zijue kutambua Nini inapasa kufanyika sawa sawa na mapenzi ya MUNGU.

    shetani alipokuja kwa namna ya nyoka akawaambia habari njema za ule mti mbaya,kufanana na MUNGU kama MUNGU,kujua mema na mabaya,na uzuri wa mti ule.ni mzuri ila kwa ubaya,kama mathayo 7:13-14 kwamba njia yaonekana safi kwa macho lakini mwisho wake ni upotevu.

     maarifa yanatufanya tuone alikoficha shetani anapokuja kutudanganya na kufunga fahamu zetu.adamu na Hawa hawakuona hicho kwa kuwa walisahau neno la MUNGU lisemalo msile wakapumbazwa na uzuri wa mda mfupi wa tunda Lile.

     shetani alijua kabisa Hawa akili zao ni njema ko na yeye akawapa mambo yaliyoonekana mema akawapumbaza.wakashawishika.

     hata na sisi tunaizuia kazi ya MUNGU kwa ushawishi wa shetani kwa mambo Fulani Fulani yanayoonekana mema kwetu lakini mwisho wake ni upotevu.tunarahisisha baadhi ya vipengele vya neno la MUNGU kwa akili zetu zilizopumbazwa tunaishi tu na hatimaye tunapoteeza haki zetu.

     ko shetani akapanda ubaya kwenye akili ya mwanadamu kupitia neno la MUNGU.kwa kuwa MUNGU alisema kwa kweli mtajua mema na mabaya nyie ikawa.

 Maarifa ni namna mtu anavyoumba ulinzi kutokana na kusikia neno la MUNGU.marifa ni juhudi ya mtu kutafuta kisichoonekana katika neno analolisikia.

     Adamu na Hawa walikuwa na neno.lakini halikupandwa kwenye akili zao.ko halikuzaa neno lisilozaa siku zote linashindwa.mazao ya neno ndo yanaitwa MAARIFA.

     ko Ile pumzi ya MUNGU ikawa batili mwanadamu akapoteza haki zake kwa kumsikiliza shetani.

      akapoteza mamlaka kwa wanyama na vyote vya kutawala kwa kuwa tayari pumzi ya MUNGU( mamlaka ya MUNGU) iliondoka kwa adamu.na kwa kumsikiliza shetani mwanadamu akakosa haki mbele za MUNGU.japo akili alibaki nayo(japo ilikuwa akili batili),akafukuzwa bustani ya Eden na makerubi wakalinda mlango wa bustani ili kwamba kwa akili iliyobaki kwa mwanadamu asiweze kula Tena mti wa uzima.

      kwa kuwa mwanadamu alitaka ashindane na MUNGU kama shetani alivyoshindana na MUNGU akashindwa.maana shetani na mwanadamu wote walikuwa wanashindana na MUNGU ili washindwe na anguko lao likawa kubwa na mahali Pao hapakuonekana shetani mbinguni na mwanadamu edeni.

#akili ikawa imepoteza haki palepale mahali Adamu alikula tunda.shetani alikuja kumnyang'anya mwanadamu haki. Ili kwamba imani ya kumwona MUNGU isiwepo kwa mwanadamu.haki ya kumwona MUNGU ikapotea.



AKILI NA IMANI(part 02)


((((((((Hii inamaanisha kwamba ukishindwa kutenda Sheria ambayo ni neno la MUNGU moja kwa moja unakua ni mfano wa nyoka kama yohana alivyowaita mafarisayo wana wa nyoka mathayo 3:7,luka 3:7. 

Mafarisayo waliijua Sheria ila waliipuuza ndiyo maana yohana akawaita "wazao wa nyoka"

#shetani ni nyoka..kwa Sababu kuu mbili

alitoka kwenye ukweli halisi ambao ni kumtumikia MUNGU akatamani ajitumikie(hii ni Sababu ndogo)

Alikuwa mwerevu kuliko hayawani wote wa mwituni akawafanya adamu na Hawa wasikilize neno la MUNGU kwa akili,,ubongo wa mtu aliyeokoka unaishi kwa imani(mwenye haki wangu ataishi kwa imani) pia kwenye mithali 3:5 sio kutegemea akili kumtumikia MUNGU.

MUNGU kwa asili anatupa Uhuru sisi wanadamu,njia mbili uzima na mauti.hata akina adamu walikuwa na njia mbili imani(MUNGU) na akili(shetani) kwa kupitia nyoka na uerevu wake aliokuwa nao shetani akawageuza Adamu na Hawa kuanza matumizi ya akili ambayo ilikuwa na matumizi machache sana(ko hapo tunakuja kuona kumbe shetani anatumia akili zetu kutushawishi maana tukisoma mwanzo 3 :1.inasema nyoka aliumbwa akiwa na akili na uerevu kuliko wote mwituni..

       ko akili za nyoka ndizo zilizomfanya shetani amtumie nyoka.alitumia uerevu wa nyoka kumdanganya mwanadamu na ndiyo maana MUNGU alipokuja pale Ile jioni alimlaani nyoka Moja kwa Moja Wala sio shetani.kwa kuwa kwa kuwa na werevu afu akakubali kutumiwa na shetani kuwadanganya wanadamu wawili.

#ninaweza kuongezea kuwa kutumia akili(bila utaratibu wa nenoni dhambi sawasawa na neno la MUNGU,Daniel 12:4,maarifa na matumizi ya akili yanavyozidi kuongezeka ndivyo dhambi zinavyozidi kuongezeka na kuwa nyingi.huo ni ukweli ambao Kila mtu anaujua.

     “MUNGU anajidhihirisha kwa imani, lakini shetani hutumia akili isiyoongozwa na Roho kumpotosha mwanadamu.”(akapandikiza akili za uasi kwa binadamu ndo maana tunaona watu wanaojihusisha na technology wanatengeneza maroboti ya kike yote ni kuunda dhambi kwa watu ili watu wapotee,Ngono,wizi na uzinzi wa akili.manabii wa uongo wanapotosha wengi kwa kutumia akili kwa kulibadili neno lenye asili ya rohoni kuwa mafanikio yanayopimwa kwa akili akati kwa halisi mambo ya rohoni yanapimwa kwa imani. Wakati mwingine na sisi wenyewe tunakosea kupokea mafundisho kwa kujaribu kuishinda dhambi kwa akili na kujitahidi akati dhambi inaondolewa kwa neema(imani) warumi 3:23-24. Twaweza kuwa sio sisi lakini dini zingine nyingi zinawafunga watu kwenye matumizi ya akili ole wetu tukishindwa kuishi kwa imani na akili..tuwe makini tusije tukapotea.

      sisemi kwamba tusitumie akili na maarifa!! Ila uongozi wa ROHO MTAKATIFU unahitajika kuishi kwa akili na imani..niliwahi kufundisha somo Moja kuwa mambo yote ni mazuri lakini usahihi wa hayo unatoka kwa MUNGU kumbukia kwa habari ya sauli.MUNGU alimwambia aue waameleki wote na vyote vilivyopo ila yeye akamwacha hagagi mfalme pamoja na unono wa amaleki eti kwa ajili ya sadaka ya MUNGU akati wakati huo MUNGU hakutaka sadaka alitaka amaleki wapotee kabisa.sadaka ni jambo zuri ila kuua ndio kulikuwa sahihi kwa mda ule.hii inahitaji uongozi wa ROHO MTAKATIFU.hata Adam alipewa akili kwa ajili ya kuipalilia Eden na kuitunza ila alipoiingizia akili kwenye neno la MUNGU ikawa laana kama ilivyokuwa laana kwa sauli.ndo maana Hawa kwa akili yake akaona anachofanya ni sahihi na kwa vipimo vya akili akatambua mti ule ni mwema kwa macho na kwa kula akajiuliza ni kwanini Hadi MUNGU aliwaambia wale akashangaa akala kwa haki ipatikanayo kwa akili na siyo imani.


        Ko akili tunayo na haki tunaipata kwa njia ya matendo yatokanayo na neno la MUNGU kwa utii na unyenyekevu kwa MUNGU muumba mbingu na nchi.

Ayatendayo hayo ataishi kwa hayo na atahesabiwa haki kwa hayo na ataitwa mwenye haki

Kuomba kujitakasa,kujitenga mbali na dhambi,kukemea dhambi,kupendana na zaidi kujiungamanisha na MUNGU kwa pamoja tukiishi katika hayo  wagalatia 3:12.


     huku ikiongezeka na nafasi ya akili ambayo ni utambuzi  wa maarifa ya neno la MUNGU kwa kupitia ROHO mtakatifu tunakuwa kamilifu katika haki kwa njia ya imani.

      kwa kuwa ROHO mtakatifu aliyevuviwa na YESU anakuja kuondoa kipengele Cha mabaya kwetu.kwa kuwa tumeshatambua Haki zetu zilizopotea basi akili iliyomkosa roho mtakatifu,inarudishiwa ROHO MTAKATIFU ko mamlaka yanarudi upya kwa jina la YESU Kristo..

       tunaishi Tena kama tupo edeni vilevile.kwa kuwa tumetambua haki yetu.


Note: adamu hakutambua Hali MUNGU alimwuliza kwa Nini mmekula Yale matunda? Adamu alilaumu mwanamke tu.kama sisi tunavyolaumu serikali na mfumo wa kiutawala na Dunia ya Sasa tukiwa hatuna jambo lolote la kufanya katika Hali hii tuliyopo. MUNGU alipoona manung'uniko akawafukuza edeni na akaanzisha mpango wa kumfanya mwanadamu atambue haki yake upya kupitia yeye YESU Kristo mwokozi wetu.

      sijui Adam angejibuje ili MUNGU amsamehe palepale? Yeye MUNGU anaona mioyo yetu aliona jinsi Gani moyo wa adamu umejaa manung'uniko na malalamiko ambayo kwa kweli hayawezi kutupa Haki yeyote maishani mwetu.bali kujikana na kuamua kumfuata YESU Kristo mwokozi wetu na maisha yetu.


Ko pale maandiko ya MUNGU Linasema kwamba Neno la MUNGU na like kwa wingi ndani ya mioyo yenu.moyo Ina maana ni akili yenye haki(imani). Ko na haki inapatikana kwa kulitendea kazi neno la MUNGU.ko like kwa wingi inamaanisha ni kulitendea kazi neno la MUNGU kisawasawa.maana likiwa halina utekelezaji Ina maana lipo kwenye akili.

       kwa mfano walevi na wazinzi dhambi hizo zipo mioyoni mwao ndo maana wanajipa haki kwa wayatendayo.

      maandiko ni yakiwa akilini,lakini yataitwa neno kwa kuwa yapo mioyoni.maana moyo ni utendaji.ndo maana tunasema wazungu Wana akili nyingi,ni kwa kuwa wanatendea kazi walivyonavyo.basi Sasa sisi tuliookoka imani yetu nyingi itaonekanaje? Kama si kwa haki? Ko tutende matendo yathibitishayo imani zetu.

  yakae mioyoni na si akilini.yaani yatendewe kazi maneno ya MUNGU kama inavyotakiwa.

#jiulize ndugu yangu je neno la MUNGU lipo mioyoni?

Lisemalo :1 thesalonike 5;17

:Kutoka 20:1.....(Mheshimu MUNGU kupitia wazazi wako) Kwa mambo yaliyo chini ya wazazi wako fanya.ila kwa mambo ambayo mzazi anakimbilia ila ni amri ya MUNGU kwa wakati huo acha,mtii MUNGU kwanza.

Weka mioyoni maana imani ni moyoni na sio akilini.

"Mathayo 17:14-21"

Luka 17:5-6

(pitia vifungu viwili hivyo vinavyoonyesha kuwa MUNGU hampi mtu imani,ila mwanadamu ndo anawekeza imani kwa MUNGU?

Pia vinaweza kukusaidia kwenye maelezo hayo hapo chini.



MAELEZO YA MUHIMU. kutoka somo la "imani na akili".

      Pia wanafunzi walimwambia YESU,,tuongezee imani YESU aliwajibu vile kwa nini? 

~maelezo kidogo ni kwa Sababu walikuwa hawana haki kwa kuwa Bado walikuwa hawana matendo hai.tulijifunza kwamba adamu alipoteza Haki yake.japo akili ilibaki na utambuzi uleule.haki ni mamlaka sahihi aliyonayo mwanadamu.mamlaka hayo yanapatikana pale tu mwanadamu anapomfuata na kumsikiliza MUNGU.

wale mitume walikuwa na uhakika kwa akili zao kwamba wanakemea Pepo kwa jina la YESU.na kwa akili waliamini kweli kweli lakini kipengele walicho miss ni kwamba hawana haki.

    haki anatupa MUNGU pekee, jiulize wewe je una Haki mbele za MUNGU.je unalitendea kazi neno la MUNGU kama inavyotakiwa? Jiulize.

#mathayo 10:1....

Marko 6:7...

YESU aliwapa haki wanafunzi wake maana alijua kuwa tayari kwa yote aliyofanya mbele Yao walikuwa na akili kuhusu kazi zake YESU.maana walizipima kwa akili zao ila walikuwa hawana haki ya kuzifanya.kwa kuwa haki inapatikana kwa matendo.YESU akawapa masharti yaatendo endapo wangevunja Yale basi wangepoteza amri.ko haki Yao pale ilithibitishwa na amri walizopewa na YESU.ndo maana baada ya kazi Ile haki Ile ikapotea wakabaki na akili kwa Yale waliyokuwa wanafanya.

     wakajaribu Tena kwa yule mtu mwenye Pepo lakini haki Yao masharti yalikuwa yamepitwa na wakati ko hawana haki kamili walikuwa na haki ya ofa tu.

    ko ili upate haki lazima uwe na akili

Matendo 19:13-16

Pepo likajibu Paulo namjua lakini nyie ni akina nani?

Wale walikuwa hawana akili Wala haki kwa wanayofanya walikuwa mfano wa watu haramu.hawana haki ko hawawezi kutenda matendo ya imani.

Heri yetu sisi tuna akili maana kuyajua maandiko ni akili basi tutafute kibali Cha haki kwa MUNGU kwa kuyatendea maneno yake kazi hapo tutaishi kwa imani kwelikweli.


Wengi tuna akili kubwa yaani tumepewa kuyajua mambo ya mbinguni(siri za ufalme) lakini matendo yanakana akili ko tunakuwa tuna imani zero.

Ko kadiri tunavyoongeza viwango vya matendo na kumtumikia MUNGU basi matendo ya imani yanakuwa makubwa sana Zaidi na zaidi

Tuna matendo hafifu ya imani kwa kuwa tunatenda kwa udhaifu neno la MUNGU.

Ko imani haba ni kuwa na matendo haba.


Note

“Maandalio ya moyo ni ya mwanadamu, lakini Mungu ndiye anayejaza moyo huo kwa haki. Msukumo wa ndani unaweza kumtafuta Mungu, lakini haki ya kweli ni kazi ya Mungu ndani ya mtu, ambayo baadaye huonekana kwa matendo.”warumi 5:1,mithali 16:1.


Akili inapokea,

Imani inaamini,

Haki inasimamisha,

Matendo yanathibitisha.

Think deeper in holy spirit.

Akili ni lango linalopokea vitu na kuvitunza.mwanadamu akifungua mlango wa moyo(upendo wa ndanj) vile vitu vya akilini huzama moyoni ambapo neno linaenda kuchanganyika na nguvu ya MUNGU ambayo hulipa neno Hilo haki mbele za MUNGU.

  MUNGU huangalia moyo 1 samweli 16:7.anaangalia huko ili aone unaingiza neno lake ili yeye aje,au unaingiza mambo ya Dunia hii ili shetani aje?

Ukiingiza mambo ya MUNGU moyoni,MUNGU atayachunguza na kuyapima ili yakiwa sahihi atoe kibali(haki) ili yaliyoingia yawe imani.

Moyo ni Nia ya ndani inayotambulisha mtu kwa MUNGU au shetani.

Wengi wanafanya mema ila Nia za ndani ni mbaya ko shetani atawapa haki yake wataonekana kwa MUNGU kuwa ni wabaya tu haijalishi wanafanya mema kiasi gani(watu wa namna hiyo ni wanafiki Tena mafarisayo).

Hii inatupa somo la kutenda sawasawa na uhalisia wetu(tusiigize maisha kwani MUNGU hadanganyiki).

       Haki(kibali) ya MUNGU huzaa imani,na imani huthibitisha huthibitisha haki.wapo wengi ambao wana haki ya ndani ila hawajaithibitisha nje.ndo maana ndani wanawaza mengi sana makubwa ila nje halijadhihirika hata moja.haki hiyo anaijua nani?,ni MUNGU peke yake.kwa nini taa yako ikae chini ya pishi? mathayo 5:15. Hakikisha haki imezaa imani inayoweza kuithibitisha haki yako kwa matendo.

Bila Shaka imani na haki ni vipengele vinavyoingiliana sana kwa namna mbili

1.Haki inatokana na imani:pasipo imani hamna haki warumi 5:1

2.mwenye haki wangu ataishi kwa imani ebrania 10:38 ikimaanisha kuwa Kuna wengine ni wenye haki wa MUNGU ila hawaishi kwa imani.japo haki Yao kwa MUNGU ipo.hawa ni ngumu sana kuithibitisha imani Yao kwa watu wengine,yaani wana MUNGU wa peke Yao.

Haki ya pili(inayozaliwa na imani) ni kubwa zaidi lakini ina gharama zaidi ya ile ya kwanza(inayozaa imani) japo wenye zote wataenda mbinguni lakini haki ya pili watakuwa na taji yenye utikufu zaidi.





Blessed!!

#this is a SOGH

# let's do GOD'S work together 💪 

# SOGH team.

#kyamba.E.A.


Comments

Popular posts from this blog

A.Kuweza kulitendea kazi neno la MUNGU

Je kwa nini namna ile?

Mwamuzi(short notes)