Unalinda?, Unajenga?.
This is a SOGH:Amani Ernest Kyamba
Maana ukisipofanya na MUNGU inakuwa Bure kabisa zaburi 127:1-2.
(Jambo la kwanza kabisa katika kuunda chemichemi ya uzima ndani ya mioyo yetu ni kugeuza Nia zetu ovu na kuhamisha kuwa na Nia safi kabisa..
ili kuujenga wokovu imara kama ilivyoandikwa kwenye mathayo 7:24-26 nafasi kuu ambayo mwanadamu inampasa aifanye ni kujenga na kulinda.
kwanza kabisa tujifunze kutoka kwa Nehemia aliyekuwa anajenga mji wa yerusalemu jambo ambalo lilikuwa ni mapenzi ya MUNGU kwamba ule mji wa yerusalemu ujengwe upya kama jinsi wokovu wetu ilivyo kwamba tukiokoka ya kale yote yapite na hatimaye yawe mapya.
nehemia alikuwa ana lengo Moja tu la kujenga Kuta za yerusalemu akawa ameomba na ruhusa Toka kwa mfalme artashasta ili akaujenge mji wa baba zake.
ni jambo kuu ambalo MUNGU alikuwa analihitaji kutimia kutoka kwa watumishi wake Nehemia na wale hamsini elfu.
basi wale watumishi wa MUNGU wakafika yerusalemu na wakaanza kuujenga mji sawasawa na neno la BWANA.
Lakini Nehemia na wenzake hawakupiga hesabu Moja tu waliyokuwa wameisahau ambayo ni kulinda mji(Cha thamani).wao waliwaza kitu kimoja tu ambacho ni kujenga moyo.mithali 4:23.
moyo ni Nini ni mahali pa utendekeji wa mambo yote ya rohoni.kwa mfano wanaposema kwamba Neno la MUNGU na likae kwa wingi moyoni mwenu,ilo neno ndilo thamani yenyewe ambayo ndiyo inapaswa kulindwa.
sasa inashangaza kwa kweli watu wengine wanasema wameokoka na wanasema wanalinda mioyo Yao akati haina Cha thamani,neno ndilo chemichemi ya uzima bayo inapaswa kulindwa Sasa mwanadamu akiwa Hana utendaji wa upendo wa neema(maana YESU hakuja kuitangua torati Bali kuitimiza, kuitimiza Inaaana ni kuondoa Hali ya kujisukuma na kujilazimisha kunakoletwa kushindwa yaani kutenda usilolipenda na kupenda usilolitenda ambayo hiyo ni Hali ya Sheria, YESU Kristo mwokozi wetu alipokuja alikuja kutupa upendo toka moyoni na sio upendo toka akilini kwamba Sasa tutapenda tulitendalo na tutatenda tulipendalo)) ya neno Ina maana Hana chemichemi ya uzima ko hata akisema anajenga Ina maana i
Unafanya usilolijua na ni kwamba wewe ni kipofu wa rohoni kwa kuwa hujui unalolifanya,unaomba usilolijua na umeokoka lakini wokovu tuliookoka hauujui Wala hauutambui.
ko ukiona hutendi matendo yafananayo na neno la MUNGU ujue hata haja ya kulinda au kuona unajenga ukue havina maana maana unafanya Bure kabisa(unafanya jambo lisilo na malipo).
kama ambavyo huwa nasema kwamba kuweka neno la MUNGU moyoni Ina maana ni kuliingiza neno la MUNGU katika utendaji hapo ndipo tunapoanza kutengeneza jambo la thamani ambalo inapasa ulilinde.
Akina Nehemia wakafika yerusalemu wakiwa na Nia na msukumo mmoja tu kwamba wanataka kujenga mji.hiyo haikutosha kwani hakuna adui alikuja kabla hawajaanza kujenga mji.
Kabla hawajaanza kujenga mji pale walipoweka Nia tu habari zikawafikia wale wapinzani wabaya wale wapinzani walianza walianza kudharau kwa maneno wakiwcheka tu kwamba nyie mtaasi juu ya mfalme artashasta? Nehemia 2:18-19.
hata na sisi tunapoonyesha Nia ya kuujenga mji(wokovu) habari zinafika kwa wabaya ambao ni shetani na mashetani wake,inakuwa imetangazwa vita basi kupitia watu shetani ataanza kuharibu kutuvunja moyo mara tu tunapomwamini YESU Kristo kuwa ni BWANA na mwokozi wa maisha yetu,ataanza kusema je unahisi utamwona MUNGU? Je utaweza kuwa mtakatifu(utakatifu naousemea ni kuwa mtakatifu mbele za MUNGU kwanza ndipo mbele za watu).kejeli nyingi ili uanze kuona kwamba kuokoka ni mbwembwe tu na siasa na kwamba sio jambo la kweli.
nehemia na wenzake walijipa moyo hawakuvunjwa moyo na kejeli hizo.
je wewe katika moyo wako umezishinda kejeli na mitazamo dhaifu ya shetani? Au mpaka Leo una imani dhaifu umeamini nusu afu vingine huamini,unachanganya mawazo Yako na ya MUNGU(be careful, MUNGU yupo juu sana mbinguni na sisi tupo chini sana duniani ko usichanganye imani Yako kwa MUNGU na akili zako za kibinadamu kwa namna yoyote).
kama akina Nehemia wangejaa kwenye mfumo wa hofu na kutojiamini kutokana na vitisho vya akina sanbalati Aidha wangeahirisha au wangejipendekeza kwa akina sanbalati na tobia mwamoni na geshemu mwarabu ili wasiwasemelee kwa mfalme wakati wanajenga yerusalemu(wasingeiamini ruhusa Yao waliyopata kwa mfalme(kama jinsi ambavyo watu hawauamini wokovu mkuu namna hii akati MUNGU ametupa na ni haki yetu ila tunaogopa na kukosa kujiamini kupata mambo makuu ya rohoni)
OLE ukiona kuwa Tangu uokoke hauna uhakika na wokovu wako au thamani unayoijenga na kuilinda ujue kabisa kwamba Bado hujafikia hatua kamili ya wokovu (yaani unajenga Bure unalinda Bure kwa kuwa wasitao hawampendezi MUNGU ebrania 10:38 kwa kuwa imani Yako Ina mashaka basi hauna BWANA kwa kuwa yeye MUNGU hapendezwi na hofu.
Na ujue kwamba hapo Bado hujaanza kujenga wokovu(mahusiano thabiti kati ya MUNGU na mtumishi wake) inamaana umekwama hapo,Sasa ili ujikwamue inabidi upndoe mbali hofu Yako ya kibinadamu kwenye mambo ya MUNGU na uweke hofu ya MUNGU ambayo ni upendo apo utakuwa umeanza kujenga na BWANA na unapojenga kwa kuwa adui ataanza kukujia kwa nguvu na kwa vitendo(si maneno ya kukatisha tamaa) tutaanza kulinda mji na BWANA pia.
anza kuomba MUNGU uame viwango hivyo vya hofu(akina Nehemia walivishinda,wewe umekwama hapo hapo) jiamini kuwa una nafasi na kibali kutoka kwa mfalme wa wafalme yaani Kristo Cha kuitwa mwana kwa kuwa alikufia pale msalabani kwa ajili yako,usitishwe na maneno Wala matendo ya shetani simama kwa njia ya utakatifu na kujitakasa(kulinda mji) na kuimarisha mahusiano thabiti na MUNGU(wokovu)
Blessed 🙏.
walipoanza ndipo wakainuka sanbalati mhoroni na tobia mwamoni na mashehe( kama geshemu mwarabu) na wengi ili kupinga ujenzi ule wa Kuta za yerusalemu( kwa vitendo na si kwa maneno kama mara ya kwanza).
shetani anapokuja ili aibe avunje na kuharibu anachokuja kupima ni Nia je ni kweli imegeuka au ni mbwembwe tu na msisimuko fulani.kwani tukiujenga wokovu kwa misisimuko ni sawa na kujenga nyumba juu ya mchanga(low bearing capacity soil)
Kama wale akina Nehemia waliongazwa na msisimuko tu ilikuwa ni rahisi sana kuvunjwa moyo na akina sanibalati na tobia na mashehe na wengi.
lakini kwa kuwa walikuwa wamegeuza Nia yaani haikujarisha kuwa ni namna Gani ya vitisho ambavyo walipitia walisimama tu kwenye lengo kamili la MUNGU.
moto ndiyo adui,na watu waliookoka bila kugeuza Nia ni kama Kuni tu lakini wakigeuza Nia na kuamua na kujikana wanakuwa dhahabu,kwamba ule moto uunguzao utawang'arisha wao na si kuwachoma na kuwaunguza na kuwapoteza
Akina Nehemia walipotoka kule utumwani hawakupiga hesabu ya upinzani wowote! Wao waliangalia lengo lao tu.
Ndo maana walipovamiwa mara ya kwanza na maadui wale ilikuwa ni kidogo wasombwe na hofu.lakini walipozijua Hila za adui kwa kuwa walikuwa na Nia wakaanza kumpinga shetani,kwa namna gani? Kwa kuwa,kwa Sababu ya uvamizi wa maadui wakasema Sasa tutaanza kujenga huku tumevaa silaha zote za MUNGU baba Nehemia 4:7-23.
Efeso 6:10 maana silaha ndizo zitakazowasaidia kujilinda na uvamizi na kumpiga shetani pale ajapo.
je wewe umevaa silaha hizo? Efeso 6:10
#haya umevaa je unalinda Nini? Maana adui anaangalia Cha thamani,je Cha thamani chako ni kipi? Unachokilinda,kama huna hujue hakika unacholinda ni kitu Bure
cha thamani ni neno litupalo wokovu.
Yohana 1 :1 Ina sema hapo mwanzo kulikuwapo neno naye neno alikuwapo kwa MUNGU Tena alikuwa MUNGU,huyo neno ni YESU ambaye ndiye atupaye wokovu wa thamani ambao adui anataka atunyang'anye hicho Cha thamani sasa sisi tuvae silaha ili tuzishinde Hila za adui kabisa.
neno si Sheria ila neno ni upendo,neno ni kugeuza nia na kumtegemeza BWANA MUNGU tu na kujitoa yote kwa ajili yake,kujikana na kuamua kumfuata na kufuata njia za YESU, kumwamini na kukiri na kudhihirisha kwamba yeye ndiye bwana na mwokozi wa maisha yetu,na kuweka tumaini katika yeye kuhusu mbingu ,hayo ndiyo yanayounda jambo la thamani ndani ya mtu,
Kumbuka:si kutenda mema tu ndiko kutakakokuokoa maana mema pasipo upendo(BWANA)ni sawa na shaba na upatu uvumao 1 korinto 13:1.
Una YESU? Au una matendo mema na kusali tu.
Hakikisha haki Yako inazidi haki ya mafarisayo hapo ti ndipo utaingia mbinguni.
Maana haki ya mafarisayo ni Ile ipatikanayo kwa sheria.bali haki izidiyo haki ya mafarisayo ni Ile ipatikanayo kwa njia ya Imani katika jina la YESU Kristo na kumwamini na kumtegemea yeye.
Ukiwa hivi hautajenga Bure( kujenga bureni kutenda haki pasipo upendo(YESU) na hautalinda Bure (kulinda Bure ni kujivika silaha kulinda jambo lisilo upendo yaani hauna upendo afu unalinda,ni sawa na mtu alindaye manyasi yaotayo popote.
Wokovu ni kuhakikisha kwamba una YESU Kristo ndani Yako na kwamba unaenda mbinguni tu,hiyo ndiyo maana halisi ya wokovu ambao msingi wake mkuu ni UPENDO.
Additional point: ko kumbe tunda la ROHO ni mlinzi tu wa jambo la thamani lililoko ndani ya mtu.sasa wengine wanazania kutenda mema ndio ujenzi wa wokovu! La Bali wokovu ni tofauti ya hivyo kwani msingi wa wokovu ni upendo kama nilivyoandika kwamba I korinto 13:1 kwamba unaweza ukafanya mema yote kama dini zinavyosema lakini kama huna upendo ni Bure,upendo ni neno upendo ni kristo,ukiwa na kristo tu kwa kumkiri na kumwamini kwamba yeye ni BWANA na mwokozi wa maisha yako hakika hapo utakuwa umepata wokovu ambao utaulinda kwa tunda la ROHO.kumkiri na kumwamini Ina maana ni kuingia katika mfumo wa kumpenda kama ilivyo kwamba upendo unafanya umuamini mwenzako umpendaye ko UNAMPENDA YESU na kumtegemea kwa namna ya ajabu na kumtafuta kwa kuomba,kutoa,kufanya kazi yake, kumtafakari mchana na usiku,kulitafakari neno lake na kufanya jambo lolote kwa ajili ya MUNGU huo ndio wokovu, 11na sio kutenda mema tu maana mema ndio mlinzi wa wokovu ulionao.
Ko wokovu si kutenda mema,Bali ni kuwa na mahusiano kamili na MUNGU wa mbinguni.
Ole inapatikana kwenye kitabu Cha zaburi 127;1
Zipo dini na madhehebu mengi duniani yote yanafundisha kutenda mema (kulinda) lakini suala lipo Moja tu,je unalinda Nini Cha thamani?,je ni kwa ajili ya BWANA? Maana wapo wengine wanalinda kitu hakina thamani sasa nani unajilinda naye maana mwizi huja ili avunje na aibe je akivunja kwako anakuja kuchukua Nini(Cha thamani pekee ni uhakika kwamba una mahusiano thabiti na MUNGU na kwamba majina Yako yameandikwa mbinguni )
Ko madhehebu na dini nyingi zinalinda hewa kwa kuwa mema pasipo MUNGU si kitu ni hamna kitu kabisa yaani ni Bure maana si mema yatakayokupeleka mbinguni Bali ni uhusiano na unayemtafuta ambao inalindwa na mema.
kwenye makanisa mengine(sisi mmoja mmoja) tunajenga ila hatulindi Bado hapo ni Bure maana kujenga mahusiano na YESU pasipo utakatifu nayo ni Bure ni upatu uvumao,maana tutajenga kweli lakini adui anakuja ghafla na kuharibu tulichojenga na kutuvunja moyo na tukakata tamaa kabisa,kama ambavyo akina Nehemia almanusura wakate tamaa kwa vitisho vile,mpaka walipoamua kujenga huku wanalinda ndipo wakaamka upya.
ko kwanini tunapata uwepo wa MUNGU kwenye ibada afu tukitoka tunapoteza ni kwakuwa uwepo wa MUNGU na kupokea ya mbinguni ni haki ya Kila mtu haijalishi ni mtumishi wa MUNGU au siyo,lakini kutunza ni kwa watakatifu tu,ko tunapoteza tunavyovipata ibadani kwa Sababu tunajenga afu kwa kuwa hatulindi basi adui anakuja kubomoa mara.ko inakuwa ni mchezo wa Jenga bomoa(ona uwepo wa MUNGU afu poteza)
akati mtu kamili wa MUNGU hamuoni MUNGU ibadani tu Bali anamuona Kila sehemu anayoenda,anapofanya kazi anapolala anapotembea,Kila anachofanya anayona uwepo wa MUNGU yaani kuwa na MUNGU linakuwa si jambo la kushangaa shangaa(kama kupata dhahabu kubwa ukashangaa ukauza ukapata Hela ukatumia zikaisha ukaenda kutafuta nyingine Tena)
Kwa MUNGU hatutashangaa kwa kusema ibada hii Ina uwepo kwa kuwa sisi tuna dhahabu nyingi sana ila tunamshukuru MUNGU kwamba tumeongeza dhahabu mpya kwenye zile tulizonazo,kama lilivyo kusudi kuu la ibada kwamba ni mahali pa kuimarisha zaidi mahusiano yetu na MUNGU,yaani tunayo ila tunaboresha zaidi Sasa wewe ukiwa Kila ibada unaunda upya ujue ni Bure na hakuna faida yoyote hapo.
Zaburi 127:1 inamaanisha kwamba kujenga na BWANA au kulinda mji(wokovu) na BWANA ni kwamba unajenga na huku unalinda hapo ndipo unakuwa na BWANA na hapo ndipo kazi Yako ya ujenzi inakuwa na thamani zaidi ya Yote mbele za MUNGU wa mbinguni.
Barikiwa sana!!
this is a SOGH
Amani Ernest Kyamba.
SOGH team.
let's do GOD'S work together 💪
Comments
Post a Comment