PART 01:HATUA ZA UKUAJI
Mwandishi:Amani Ernest kyamba.
SOGH Team.
MUNGU wa mbinguni alipoanza kuumba mbingu na nchi,dunia ilikuwa ukiwa,tena utupu tena giza lilitanda juu ya vilindi vya maji.MUNGU akaanza somo la uumbaji kwamba yeye awezaye yote angeweza kuijaza Dunia yote kwa siku moja au wakati mmoja tu.angeweza kuumba vyote kwani yeye anaweza vyote.akatoa somo kwetu kwamba katika kujenga,Mda ni kipengele cha muhimu zaidi.
Pia katika technology ya ufundi wa ujenzi wa nyumba.mtu anaweza kuwa na gharama nzima na maandalizi mazuri ya ujenzi,lakini akiwapelekesha mafundi wake wamalize ujenzi mzima wa nyumba kwa wiki moja.inawezekana.lakino asilimia za uimara wa nyumba hiyo unakuwa mdogo sana .na labda yajapotokea mafuriko,pepo,na mabadiliko ya Hali ya hewa,hiyo nyumba itaanguka,au yaweza kuanguka hata kabla haijamaliziwa kujengwa. Yote hiyo inasababishwa na ujenzi kutokuwa na hatua.
MUNGU angeweza kuumba wanadamu wote aliowahitaji endapo angehitaji kama alivyoumba malaika wengi.lakini akaanza na wawili akawaumba,akawaambia zaeni mkaongezeke mkaijaze dunia.akaumba wanyama wawili wawili na akatamka neno "zaeni".alianza na wawili kwani alitoa funzo kuwa kuanza na wanadamu wawili ingekuwa rahisi kutengeneza kizazi Chenye utashi kumhusu yeye MUNGU.kizazi kinachoelewa ni nini thamani ya ukuaji.
MUNGU alimchagua Ibrahim kwa ajili ya wokovu wa ulimwengu.angeweza kuanza na watu wengi lakini alianza na mmoja ili msingi wa wokovu uwe imara,mpaka waebrania ikasema tutapataje kupona tusipoujali wokovu mkuu namna hii? Ebrania 2:3.ko MUNGU alianza mpango wa wokovu kupitia mtu mmoja na sio wengi.MUNGU anaanza katika upungufu anakamilika katika ukamilifu.
Nyumba iliyojengwa kwa hatua ni ngumu kuiangusha kwa kuwa ikijengwa kwa hatua itabomolewa kwa hatua.lakini ikijengwa kwa mara moja ibomolewa mara moja hivyohivyo.ko wokovu ni hatua nyingi sana.hakuna awezaye kuuvuruga wokovu huu mkuu namna hii.
Katika kipindi cha nuhu,MUNGU angeweza kuwatenga nuhu na familia yake na wanyama wote wawili kwa namna nyingine zaidi ya Safina.kwa namna bora zidi kwa akili zetu za kibinadamu,labda angewaondoa duniani kwa mda etc.lakini akaanza kuwekeza kwa mtumishi wake,nuhu kuijenga Safina kwa miaka Mia na ishirini 120.lengo ni kutoa nafasi kwa watu kuujua mpango wake.watu wale wakapuuza wakamtukana nuhu na kumkejeli badala ya kutafakari na kutubu,dunia ikamezwa na maji,uhai wa waovu ukapotezwa.MUNGU ni mwaminifu sana,kamwe hawezi kufanya jambo pasipo kuwataarifu wanadamu.
YESU kristo kabla hajazaliwa duniani,manabii walitabiri na watu walijiandaa kumpokea messiah. Maandalizi hayo yote yaliandaa njia ya YESU kuifanya kazi yake vyema.vipi ingekuwaje endapo YESU angekuja pasipo kutabiriwa kwa mda mrefu?,au angewahi mara baada ya gharika?.au angekuja kabla yohana mbatizaji hajaja(mtu aitengenezaye njia ya BWANA isaya 40:3,mathayo 3:3,luka 3:4)?.isingekuwa na utukufu kwani kabla ya YESU kuja MUNGU alianza kuandaa misingi ya mda mrefu ambayo ni sheria(torati) ili YESU aje kukamilisha pendo.kwani hakuna pendo pasipo Sheria.
YESU kristo alipokuja duniani alikaa mda wa miaka kama thelathini akiwa hajaanza kazi kama mwokozi(mda huo alikuwa ni seremala).m wote huo alikuwa anafanya maandalizi ya huduma kwa kujifunza kunyenyekea,kutii,kumpendeza MUNGU na wanadamu Luka 2:52.alijifunza kutii kama mwanadamu wafilipi 2:8.alijifunza sheria kwa ufasaha wote.alizaliwa kama wanadamu wengine ko ikampasa kukua kama wanadamu wengine.kwa hiyo mpango wa kwanza wa MUNGU ilikuwa no kumfanya YESU kuishi kama mwanadamu asilimia Mia,miaka 30 alikuwa akijifuza kuishi kama wengine kwani alikuwa kama wengine wakati huo.baada ya kuwa mwanadamu asilimia 100,ndipo akaingia kwenye miaka mitatu na nusu ambayo akaanza kazi kama MUNGU. YESU hakujifunza kuwa MUNGU wala hakuhitaji mda wa kujifuza kuwa MUNGU kwani tayari YESU ni MUNGU,ndiyo maana kwa mda mfupi tu alifanya makuu.isingekuwa hivyo basi ingekuwa ni utukufu tofauti.lakini njia hii kamili ilimfanya YESU awe mwanadamu 100% na MUNGU 100% ili YESU awe limbuko la utakatifu duniani,kwani pamoja na YESU kuwa mwanadamu kamili,YESU hakutenda dhambi hata moja maishani mwake.ko watu tusidanganyike kuwa YESU alikuwa na upendeleo tofauti na sisi.kwani kama sisi alikuwa mwanadamu na katika ubinadamu wake akawa MTAKATIFU.je? Hawezi kutufanya na sisi kuwa watakatifu?. ANAWEZA!! NI SISI KUFUNGUA Mioyo yetu TU.
Mfano wa mwisho ni jinsi ukuaji wa mtoto ulivyo.mtoto hawezi kunyonya akiwa tumboni.bali atakula virutubisho vya mama.akizaliwa hawezi kula virutubisho kwenye damu ya mama kwani atanyonya(mwanzo tumboni vilikuja bila kulazimisha ila sasa inabidi anyonye yeye).akifika miezi sita anaweza kula chakula laini na sio vyakula vigumu vya watu wazima huku akichanganya na maziwa.(utegemezi wa mama unapungua).hakuna mtoto wa miezi saba mwenye meno mdomo wote.mtoto hawezi kuzaliwa akiwa anaongea.
Mtoto Atazaliwa,atakaa,atatambaa,atatembea ma kuongea pia,hizo ndizo hatua.na zote zina maana yake katika ukuaji.ukimpa mtoto wa miezi miwili chakula kigumu kinaweza kikamuua pamoja na kwamba ni chakula cha binadamu(si chakula cha binadamu wa umri wake).ko mambo yote mazuri ni MAZURI kufanya ila kwa usahihi unaotokana na MUNGU anavyotaka kufanya,na usahihi huo ndio unaitwa HATUA ZA UKUAJI.
Neno la MUNGU linasema ukisipokuwa mwaminifu Katika mambo madogo hutaweza kuaminiwa katika mambo makubwa.ko msingi wa kutenda makubwa ni mpaka ukamilishwe katika madogo yote mathayo 25:23,luka 16:10.
MUNGU hadhihakiwi,apandacho mtu ndicho atakachovuna,ikimaanisha kuwa kwa MUNGU huwezi kuruka hatua.ni lazima upitie hatua zote ambazo inabidi upitie ili ufike viwango vya juu
Maajabu ni kwamba watu wengi katika wokovu wamekuwa wakitamani hatua za juu wakati huo hatua za chini hawajapiga.hatua za juu za maombi,huduma,utukufu etc.huwezi kufika juu kama hujakamilika chini.
Kwa mfano wote tunatamani kufika mbinguni/kwenda mbinguni lakini njia ya kufikia mbinguni hatutaki kuifuata.basi "tamaa ikiwa mbele mauti inafuata nyuma".ko tamaa ya kufika mbinguni inatufanya tusifike mbinguni bali tufike mautini tena dah!!.
Mtoto mdogo akianza kufanya mambo yawapasayo wakubwa,si jambo zuri kwa kuwa si sahihi.si ajabu sulemani anawasihi binti za yerusalemu kuwa wasiyachochee mapenzi wala kuyaamsha mpaka yatakapoona vyema yenyewe wimbo ulio bora 2:7.kufika mbinguni ni haki yetu lakini je duniani tunaishije?.basi dunia ni ngazi ya kufikia mbinguni.ko ili tufike mbinguni ni lazima tuwe tumepita kwenye ngazi kwa uaminifu.
Tamaa itatufanya tuende bila uangalifu ko tutajikuta tunaanguka badala ya kusimama,tunafeli badala ya kufaulu,tunashindwa/tunashindana badala ya kushinda.maana tunayofanya ni hisia si halisi kwani si haki yetu kuyafanya kwa kuwa hayajawa yetu kwani si yetu.
Hili ni neno la MUNGU ambalo linasisitiza kuthamini hatua uliyopo/unayopita katika wokovu.watu wengi wapo kanisani wanaabudu,ila hawana hatua ya kusonga mbele wameganda tu kwani Hawathamini hatua waliyopo ko wameridhika na walipo kwani hawajui walipo.
Wapo wengine wana hatua ya juu zaidi kuliko hatua zao halali kimaombi,kihuduma,kimaisha etc.wanawaza mambo makubwa wakati madogo yanawashinda.neno linasisitiza uaminifu katika mambo madogo,kwani baraka ya mambo makubwa ni yetu endapo tumeyatimiza mambo madogo
OLE ole.!!;:wapo watu wengi Wana imani kubwa sana ila imekufa,uozo wa imani hiyo ni mkubwa sana ko matendo Yao yananuka zaidi na kukataliwa zaidi kwani miili yao mikubwa imekufa imeoza inanuka.mbu akifa,tembo akifa nani anachafua hali ya hewa zaidi?.ajabu iliyoko rohoni ni kwamba hata marehemu wanakua.kwamba hata mtu aliye na imani mfu bado atakua ko na uozo wake utazidi kuongezeka.kwa hiyo cha msingi ni kwamba kama imani inakuwa hakikisha ipo hai ili ifanye kazi kubwa.maana ukiwa na imani kubwa tena mfu ni kwamba unanuka zaidi rohoni na utaadhibiwa zaidi.ko ni heri zaidi kurekebisha,kuhusu habari hii ya imani
Shetani anamwamini sana MUNGU.yakobo 2:19.imani ya shetani kwa MUNGU ni kubwa sana kuliko imani zote za wanadamu,ila imani yake ni batili(imekufa) ko kufa kwa imani kubwa zaidi ya shetani kunanuka zaidi ya vyote,kiasi ambacho halistahili msamaha,kwani uchafu wake wa mwili mfu wa imani yake unawaambukiza na wengine.wapo watu wengine duniani ni mashetani kwani wameoza wananuka,hadi wanawaozesha wengine.kwa namna wanavyowaozesha wengine ndivyo ambavyo mlango wao wa kufufuka kiimani unakuwa unafungwa zaidi.ko mwanadamu wa namna hii anakuwa jirani kitabia na shetani jambo ambalo linahesabiwa kama KUMKUFURU ROHO mtakatifu ebrania 6:4
#kabla MUNGU hajakuona wewe anaona imani yako kwanza.
,na uhai wa imani ni matendo katika ROHO.
1.KUOMBA
Neno linasisitiza kuomba,kuomba ni msingi wa wokovu.lolote tutakaloomba tutapewa.ROHO mtakatifu hutusaidia katika madhaifu yetu warumi 8:26.mawasiliano yanaongezeka kiwango cha hatua kadiri siku zinavyoendelea.
Hebu nijaribu kuelezea hapa tu,MUNGU aweza kukifunulia zaidi na zaidi ya hapa.:wengi wanaookoka wanatengeneza misingi yao ya kufunga na sio kuomba na wengine kuomba na sio kufunga.ko kumekuwa na wafungaji na kumekuwa na waombaji,lakini wote hawaendi kwenye misingi ya MUNGU.ko hao ni fungafunga(starvers)na ombaomba(beggars).kwa sababu wanafunga na kuomba bila kuwa na hatua.
Wengine wanafunga ila hawaombi,wanajua kufunga ila hawajui kuomba.kufunga ni kwa mwombaji(anayemwomba MUNGU),na sio kuomba ni kwa mfungaji.wengi wanaokoka wanaanza kula vyakula vigumu vya kufunga wakati huo hawajui hata "kwa nini wanaomba",jinsi ya kuomba,haki ya kuomba.kwa hiyo wanakuwa fungafunga na ombaomba kwani chakula kigumu kitaharibu matumbo yao wataanza kuuchoka wokovu ghafla.kwani walikula bila utaratibu.
Mtu anayeokoka au anayepitia hatua halisi ili akue,ili aboreshe mahusiano na YESU inabidi ajifunze kwa nini kuna kuomba?,haki ya kuomba,namna ya kuomba(hata wanafunzi wa YESU walifundishwa mathayo 6:9),imani ya kuomba,vigezo vya kuomba(utakatifu,utii),muda wa kuomba,mambo ya kuombea,wakati wa kuomba,umuhimu wa kuomba wakati huo anaendelea kuomba.kuomba ni jambo dogo ila kufunga ni jambo kubwa.kwa hiyo muumini lazima awe muombaji sana halafu kutokana na mahusiano yake na MUNGU yanayojengeka ndipo anaanza kufunga.kufunga ni haki ya mtu yeyote anayejua thamani ya maombi.mbona watu wanafunga,wanaomba bila kujua thamani ya maombi?
Yaani mwingine anaomba siku ya maombi tu,hajui kuomba ila anakuja kufunga maombi mazito.hii ni hatari sana.inakuwa ni sawa na Bure.lazima mtu ajue hatua za imani ili mawasiliano yaendelee kujengeka na kuboreka.ukianza na makubwa hautapata unachokipata unajikuta unapitwa na wakati katika wokovu, na kuona kuwa hamna uhai katika wokovu kumbe wewe ndo hauna uhai.(hii ni hatari sana, watumishi wenzangu).
2.ROHO MTAKATIFU.
Ishara ya kwanza ya kwamba una ROHO ni kuwa mtakatifu.sasa wengi sio watakatifu ila wananena kwa lugha.kwa hiyo ishara zao ni kunena kwa lugha ila moyoni mwao wana kiburi,majivuno,ufarisayo,dharau,wivu,faraka,ugomvi,unafiki na uovu wa kila namna,hiyo ishara inakuwa ishara mfu(iliyolaaniwa),kwani haina uhai ambao ni utakatifu.
Wengi wanajikita kunena kwa lugha wakati bado hawana matendo safi,basi kinakuwa ni kizazi cha ishara na sio kizazi halisia.
Wale watu wakamfuata YESU kuomba ishara luka 11:29. YESU akasema hiki kizazi cha ishara kitapewa ishara za yona (ishara za zamani),ishara mfi tu.ko hatutaenda mbinguni kwa sababu ya kunena kwa lugha tu.ila tutaenda .mbinguni kwa kuwa na moyo safi.kama ilivyo kuwa kula na kunywa hakutupeleki mbinguni,zaidi ni utakatifu wa moyo,ko tusiwe kizazi cha ishara za rohoni,bali kizazi cha asili ya rohoni.
Wengi Wanalazimisha hatua ya ishara ya kunena,badala ya kulazimisha hatua ya kuanza kutenda mema na kujifunza utii na unyenyekevu ambayo inabidi iwe ya kwanza hiyo nyingine ni zawadi(ofa) ya kiroho kutoka kwa MUNGU.
Mitume walipokea ROHO MTAKATIFU baada ya kukidhi gharama za upendo wao kwa YESU.walipokusanyika kinyume na sheria za wayahudi,wakaishinda hofu ya kifo kwa ajili ya BWANA YESU,wakastahili kuiteka nguvu ya ROHO.sisi tunatakaje kuiteka pasipp nguvu?.MUNGU ni nguvu kwa nguvu.hakuna dhaifu atakayepokea nguvu.dhaifu aliyekiri udhaifu na kuukubali ataishi kwa ishara tu.
Mitume hawakukusanyika ili wanene,walikusanyika kuomba na kutii na kunyenyekea,matendo ya mitume 2:1.ila MUNGU akawashushia ROHO MTAKATIFU na wakanena kwa lugha(wakati wa MUNGU)
Utafuteni ufalme wa MUNGU kwanza na haki yake ndipo hayo mengine mtazidishiwa mathayo 6:33.
3.NENO.
Neno ni chakula yohana 6:31-35.MUNGU ndiye anayeshusha chakula kwetu.anayepokea chakula ni mpishi.kama ambavyo MUNGU alishusha mana ndipo watu wakaokota ili wakapike ilo wale na familia zao,Mpishi naye ni mwanadamu anapika na inabidi ale,wapo wapishi wamekizoelea chakula wanachopika,kwa hiyo wanapika ila hawali wanachopika labda wanakula alichopika mwengine,au wakati mwingine wanakula chakula kingine kabisa,hii si sawa kabisa.wapo watu ni masikini,wanazijua harufu za vyakula vingi sana vya kitajiri japo hawajawahi kula,vyakula vingine wanavijua majina na harufu,japo vingine hawajawahi kuvisikia(ila harufu wanaijua (wanasema hili neno ni la kweli,ila hawalifuati kwa hiyo wamekuwa na pepo la utambuzi ila si watu wanaojengwa na neno).
Harufu haishibishi wala jina la chakula halishibishi,bali kula chakula ndipo kunashibisha.katika mpangilio wa kiroho neno linaanza na kutenda ndipo kujua,kujaribu ndipo kuona malaki 3:10.sasa watu wamegeuza hatua,wanajua kabla hawajajaribu ko wanakuwa wajuaji na sio watendaji.neno Lina mfumo tofauti kwani ndio kiini cha maisha ya kiroho.neno linakataza dhambi na linasapoti mema.usijiulize ulize!! Matendo maovu ni dhahiri na mema ni dhahiri.
Kuna tatizo linaitwa mzio wa vyakula fulani limezuka,sia ajabu hata kipindi cha YESU lilikuwepo yohana 6:50-71.
Watu wanamfuata YESU huku wakiwa wamejipanga kula chakula fulani!!.wanachagua vyakula(neno).wanataka maneno Malaini Malaini,na siyo magumu.wakiambiwa neno gumi wanakwazika na kurudi nyuma.eti neno linawapa mzio.mzio ni udhaifu wa kishetani inabidi tumwombe MUNGU atuponye mizio yetu.
Neno gumu,neno laini yote ni ya kufanyia kazi maana MUNGU amempa mpishi atupikie.
Kuna ole za mpishi pia labda tutaziona kwenye sehemu ya pili ya somo hili,neema ya BWANA ikituwezesha.
4.SADAKA.
Nia safi ndiyo sadaka safi mathayo 6:19.
Si wingi ila ni sehemu ya upendo wako kwake.utatoa kutokana na jinsi unavyompenda MUNGU.
MUNGU hadhihakiwi panda uvune.panda mema uvune mema,ukipanda mali unavuna mali,lakini mbingu utakosa.ko hakikisha unapotoa sadaka ya mali unaitoa si kwa sababu ya tamaa zako mwenyewe,bali kwa sababu ya mapenzi ya MUNGU kwanza.hapo mali zako zitalindwa na kutakaswa.
Kabla ya sadaka za nje,sadaka ya kwanza ni mwili warumi 12:1.hii ndiyo ihalalishayo sadaka zote.
Yohana 21:1 mbingu mpya na nchi mpya zinakuja kufukuza ukale wote.ko ili mwili ufe ni lazima nia yako ya ndani iwe inamwelekea MUNGU,hiyo ndiyo hatua ya kwanza ya sadaka mwili.je wewe matoleo na sadaka zako zinamwelekea MUNGU au zinatafuta utukufu wako?
Barikiwa sana!!.kwa kujifunza pamoja na mimi katika hii sehemu hii ya kwanza.tutaonana sehemu ya pili,kwani hatuwezi kujifunza kikamilifu mara moja,bali tunakumbushana kidogo kidogo tu fellows.MUNGU AWABARIKI NA ATUSAIDIE KATIKA UTENDAJI.
AMEN!!.
mwalimu:Amani Ernest kyamba
SOGH Team
Motto:Let's do GOD'S work together
soghteam.org
Comments
Post a Comment