Jumbe kwa makanisa saba
16 Jun 2024
Jumbe Saba kwa makanisa ya leo
By amani Ernest Kyamba.
From SOGH team.
.hapa Cha kwanza tunabidi tujue kuwa kanisa ni hekalu la MUNGU ambalo ndilo sisi. 1 korinto 3:16
*Kumbe huu ujumbe wa makanisa saba haya ni ujumbe wa mtu mmoja mmoja kwanza ndipo itafuata sinagogi maana sinagogi lisilo na mapungufu linajengwa na watu wasio na mapungufu pia. ko kumbe utimilifu wa sinagogi unaanza na sisi wenyewe.
Kitabu Cha ufunuo kilikuwa kinalifumbua kanisa kuujua wakati na mda uliopo na utakaokuja kwamba watu wazijue Siri za rohoni za MUNGU na pia Siri zao zifumbuliwe na watu wajirekebishe.
*Ko tunapozungumzia makanisa saba tunamaanisha mapungufu yaliyopo ndani yetu ambayo yanaweza kutufanya tusifike mbinguni au kusababisha tusione utofauti na upya kwenye maisha yetu ya kimwili na kiroho.
Kanisa la efeso. (kanisa la kwanza) Ufunuo 2:2a
Lilikuwa ni kanisa zuri sana. Lilikuwa na linajitaabisha katika Mambo ya MUNGU kwa maombi na kusoma neno kwani kwa neno liliyatambua mambo maongo ya manabii waongo. pia halikuchukuliana Wala kuyasapoti mambo mabaya ufunuo 2:2b. Kwa mfano wapo watu makanisani wanaoyapa kibali mambo yenye roho za shetani ndani yake kwa mfano nyimbo za kidunia ambazo zina mipango mibaya ya kidunia ya kuwafanya watu wajione wenyeji wa Dunia hii yaani wamsahau MUNGU wao na kuyapa mambo ya Dunia kipaumbele kuliko MUNGU wa mbinguni. wengine Bado wameshikiria tamaduni zao za asili za kimakabila wakati Wana wokovu ndani Yao. wengine kupitia simu zao wanasapoti mambo machafu ya duniani kupitia mitandao ya kijamii. Haya ni mapungufu yatazuia mengi ya rohoni maishani mwetu, wakati huo na mengine mengi warumi 1:32. Ni dhambi kujichanganya na maovu ya Dunia hii au kuisapoti kazi za mwovu, pia kwa mfano kuisapoti kazi za watumishi wa uongo.
*Tena kanisa la efeso lilikuwa na subira na uvumilivu katika Hali zote za Dunia likiingojea ahadi ya MUNGU. maana yake ni imani na matendo ya kumtegemea MUNGU. je sisi viwango vyetu vya kumtegemea MUNGU vipoje je tuna imani inayochagua? kwamba MUNGU anaweza hili na hawezi hili? Maana ya aina hii ya imani ni imani haba. je tunavumilia katika yote bila kumlaumu MUNGU?. Ufunuo 2:1.
Lakini efeso liliyashinda haya yote kwa kumtafuta MUNGU kwa bidii sana na likawa vizuri katika yote.
Japo Bado halikuwa limekamilika. je Nini kilikuwa kinawarudisha nyuma efeso pamoja na yote hayo? Na utimilifu na utumishi wote huo?
*Jambo Moja liliwafanya waonekane hawajatimia kwa. MUNGU wa mbinguni. ni kwa Sababu waliuacha upendo (matendo) wa kwanza kwa kutotubu dhambi zao. Sio kwamba kweli walikuwa hawafanyi kabisa Yale matendo ya kwanza. hapana waliendelea kufanya lakini matendo Yao hayakuwa na thamani Tena kwani kulikuwa na dhambi hawajaitubu yaani waliizoea dhambi fulani. huku wakiendelea kumtumikia MUNGU. yeye MUNGU anataka utakatifu mkamilifu. ko ni lazima tuwe safi kwelikweli. ufunuo 2:4-5.
*Toba ya kweli ilitaka wakumbuke wanapoanguka watubu kwamba Kuna baadhi ya mambo ni dhambi ila walikuwa wanafanya kama sio dhambi ko YESU Kristo alitaka wajichunguze alafu waombe toba na kuiacha hiyo dhambi na hiyo ndiyo toba ya kweli kutubu na kuiacha. sasa saivi watu wanatubu huku wanaendelea kufanya dhambi hizohizo kwa kujua au kutokujua kama waefeso bas YESU Kristo anataka tujue tunachoomba MUNGU atusamehe na kukiacha kwelikweli hapo tutakuwa tumemwita YESU Kristo awe ndani yetu na tutakuwa huru kwelikweli. na hapo tutaona NGUVU ya ROHO mtakatifu maishani mwetu kwa kuwa roho mtakatifu anashuka kwa watu wenye Nia na kiu ya kuwa sio wenye mazoea ya utakatifu. Basi wewe unda kiu na kubali gharama za kuutunza utakatifu afu aje msaidizi wa kukusaidia kwenye lengo safi la kimungu ambaye ndiye ROHO mtakatifu. yohana 14:16 maana mtu hawezi kusaidiwa asipoonesha uhitaji wa kusaidiwa. basi onesha kiu ya kuwa mtakatifu kwa kuwa mtu wa kujichunguza upoje mbele za BWANA ili naye bwana kusamehe na kuondoa dhambi zako. tena Mtu mwenye upendo wa kweli na MUNGU ni mtu mwenye kujichunguza na kuangalia wapi anamkosea MUNGU na kutubu kwa hayo yote Tena kuyaacha.
Tukishinda kuwa watu wa toba ya kweli tutaustahili mti wa uzima yaani uhai yaani utakatifu ufunuo. 2:7.
kanisa la pili(smirna) ufunuo 2:8
hili ni kanisa zuri sana la kiroho na hii ndiyo namna MUNGU anataka mtu wa kiroho awe. kuipata neema hii ya wokovu ni gharama kwakuwa tunakuwa tumejinasua kwenye makucha ya shetani. hicho kitu mwovu hapendi ko ataendelea kututafuta sana na kwa gharama zaidi ilo ni jambo la kwanza kulitambua 1 Petro 5:8 unasema shetani anatusaka nasi tupo kwenye himaya yake ivyo kama yeye anavyochukua gharama kubwa kututafuta atumeze basi na sisi tuongeze gharama ya kumkimbia na kumtafuta MUNGU haijarishi tutapitia.
(Umasikini wa rohoni ndio utajiri kwa Sababu uhitaji wa kitu ndo unaotupa hamu na mbinu za kukipata ko lazima tuwe masikini wa rohoni kwa kumuhitaji MUNGU sana maishani mwetu). dhiki, manyanyaso, kutengwa, kuchukiwa, kuwekwa gerezani, kutukanwa, kudharauliwa, pia labda na miili yetu inatupinga kufanya mambo ya MUNGU na mambo mengi sana ya Dunia kuchukua gharama na kupiga hesabu ndio jambo la muhimu na msingi zaidi. ufunuo 2:9-11.
YESU Kristo alisema mtu anayetaka kumfuata lazima ajikane mwenyewe kwa yote kwenye safari ya wokovu. mathayo 16:24, Marko 8:34, Luka 9:23. *Wokovu n gharama basi lazima tukubali gharama hizo Luka 14:28. Yaani kisiwepo kitu Cha kututenga na upendo wa mwokozi YESU, warumi 8:35.
Tuvumilie na kushinda tutavikwa taji Naam tutapata taji ya uzima yaani ikipimwa kwa moto itang'ara kwa Sababu tuliutunza ushuhuda na wokovu kwa kuhimili yote shetani anayoyaleta kwetu. wafilipi 3:14. Kumbe Kuna mede imeandaliwa kwa ajili yetu Naam taji ya uzima tukikaza mwendo wa kitakatifu.
Kanisa la tatu (pergamo)
ufunuo 2:12
Ufunuo 2:13 mahali ambapo pergamo ilikuwepo palikuwa ni mahali palipo ni kiti Cha Enzi Cha shetani, kwamba ni mahali ambapo pana mamlaka kubwa ya shetani ye ye lengo la kutaka kuwarudisha nyuma watumishi wa MUNGU pia kuwaua.
Jinsi gani shetani anaonesha mamlaka kwamba kiti chake Cha Enzi kipo sehemu tupo, ni pale anapohuisha hofu miongoni mwa watumishi wa MUNGU kwa kuamsha watu wenye roho za Giza waje kuwapiga na kuwaua watu wenye imani. lengo ni kwamba waliookoka waogope kukiri wokovu na hapo ndipo mwanzo wa maanguko na kuiacha wokovu.
Lakini kanisa la pergamo halikurudi nyuma hata baada ya shetani kuwashambulia kupitia hofu kwamba hata antipa shahidi mwaminifu wa MUNGU akauliwa na huyo akatumiwa kama njia ya kulitishia kanisa lakini watu wa pergamo hawakurudi nyuma. je sisi hofu itatutenga na Kristo? Umasikini utatutenga na Kristo, njaa, kiu manyanyaso je nikipi kitutenge sisi? warumi 8:35. Haya pergamo walimshika MUNGU sana na kuitetea imani hata katika misukosuko.
Bwana akauona umahiri wao, lakini kwa ajili ya hayo akawaonyesha udhaifu wao ili wawe wapya kwelikweli, lakini wapi walipungukiwa ni kwa Sababu waliyaruhusu mafundisho kinyume na neno la MUNGU kuingia ndani Yao haya ndiyo mafundisho potofu, haya ndiyo mafundisho ma matendo yenye lengo la kukosesha watu wa MUNGU duniani alafu pia wasifike mbinguni. watu wengine wanakuwa wanikolai kwa kuwadanganya watu na kuwapoteza wasimwone YESU Kristo Bali waonekane wao tu mfano manabii wa uongo ambao wamechakachua watu wengi wasimuone MUNGU halisi wakati wapo kwenye mafundisho halisi yote no kwa Sababu imani Yao imepotoshwa na wanikolai.
Pia wanikolai (maajenti wa Giza) wanaweza kuwapo makanisani kusababisha kukosekana kwa umoja ambao ndio msingi mkuu wa wokovu kwa kupitia maamuzi mabaya, huduma mbaya, Hawa ni mbwa mwitu. wanataka kuriharibu kanisa kwa kulikosesha umoja wa kiroho.
YESU anataka Kila mtu ajichunguze je maisha yake yanakosesha wengine wasimuone YESU? Baada ya hapo kutubu kabla YESU Kristo hajatupambanisha na neno lake tunashindwa na kuanguka. bwana hataki hata mmoja apotee.
*Tukizuia matengano na uharibifu ndani yetu tutaistahili mana iliyofichwa ya Siri yaani upendo na umoja na nguvu ya kumshinda shetani. maana mana ya kwanza haikuwafanya waisraeli kushinda na kufika kanaani kwa kuwa pamoja na kula Bado walimnung'unikia MUNGU. maana huko kunaondoa Hali ya imani Moja, basi lazima tushinde. Umoja anao utaka YESU Kristo ni zaidi ya upamoja kwamba tuwe na imani Moja, MUNGU mmoja, lengo Moja naam wokovu wa aina Moja kwakuwa hatuna mwingine. efeso 4:3-6
kanisa la nne (thiatira).
ni kanisa lililokuwa hai kwenye mambo ya MUNGU lenye upendo, matendo, Imani, na huduma na subira na kukua kiroho Kila siku. lakini udhaifu wa kanisa hili ilikuwa ni kumridhia na kumpa nafasi yezebeli (aliye mpotoshaji na mharibifu wa kazi ya MUNGU maana yezebeli aliwapotosha Israel waabudu baali wa jua lakini ili Israel ibadilike MUNGU alimuangamiza yezebeli. kumbe ilituwe watakatifu lazima tukubali kuondoa roho chafu ndani yetu na watu wabaya wasiotaka kutubu kama akani Alivyolichafua kanisa la Israel. basi kanisa tujitenge na kuweka bayana utofauti na pia kuithibitisha imani yetu. watu wamjue yezebeli/akani na kumjua MUNGU na kuamua, maana wapotoshaji na wapotezaji Wana hukumu Yao wasipotubu. basi YESU Kristo amesema kuwa tushike tulichonacho kwa kuwa kina thamani sana bila kujitwika mzigo mwingine maana vita ni juu ya BWANA. ufunuo 2:24-25.
Kanisa la Tano (sardi)
ufunuo 3:1
Ni watu wenye jina la kuwa hai ila wamekufa kama soma la pastor linalosema(mkristo asiyekuwa na Kristo na mkristo mwenye Kristo ndani yake) asiye na Kristo ila ni mkristo ni maiti za kiroho maana thamani ya kiumbe inatokana na uhai ndani yake. sardi walikuwa aina za maiti kwa kuwa walikuwa hawana uhai wa kiroho yaani uhalisia wa wokovu. kwa Nini walikufa ni kwa Sababu wanafuata mafundisho ya wanadamu Wala sio neno ndo maana anawaambia wayarudie waliyoyapokea na kuyasikia wakazane kwa hayo ili wawe hai tena. yaani uhai unakuja kwa kulitendea neno la MUNGU kazi. sio kutunga Sheria kiongozi kinyume na MUNGU. YESU KRISTO anataka msingi mkuu wa wokovu wetu uwe ni neno la MUNGU ambalo ni biblia na sio maagizo ya wanadamu kuwa njia zetu isaya 29:13. tukilifuata neno kama kiongozi mkuu tutaistahili kuvaa mavazi meupe na kuandikwa kwenye kitabu Cha Uzima yaani tutaonekana watakatifu kweli mbele za Ufunuo 3:4-5.
Kanisa la sita (filadelfia)
ufunuo 3:7
*Ni kanisa lenye nguvu kidogo linaendana na watu wa sasa. wana nguvu kidogo. kwa Nini kwa Sababu Kuna udhihirisho mdogo wa nguvu za MUNGU. roho wa udhihirisho ni ROHO mtakatifu na neno na maombi ndio vitaongeza nguvu ya kuishi na wokovu. pamoja na nguvu kidogo Bado BWANA anatupenda. YESU Kristo sio kwamba aliridhika na kanisa Hilo Bali na kwamba alilipenda kanisa Hilo kwa kuwa Bado lilishika neno lake na neno la subira yake.
Kwa hili kanisa lazima tujue namna MUNGU anavyowekeza sawa na imani zetu na utayari wetu. basi lazima tuamue ni kiasi Gani tunataka roho awekeze ndani yetu. kwa kuwa BWANA anatupenda jinsi tulivyo. Kwa mfano kwa masomo Fulani kwamba yohana alikuwa na roho ya eliya kwa kuwa halikuwa na mtu mwenye wivu na kazi ya MUNGU kama eliya ndo maana kazi ikarudi upya kama yohana basi lazima tujue kuwa BWANA anavitafuta vyombo vizuri sana basi tukubali kutumika kama vyombo vizuri. lasivyo tutafeli sisi lakini MUNGU yeye hawezi kufeli. atainua wengine kama alivyomuinua eliya mpya(yohana) Basi omba na wewe uwe mtumishi kamili wa MUNGU amen...
Kanisa la Saba(laodikia)
ufunuo 3:14
Kanisa vuguvugu ufunuo 3:15 halina maamuzi kamili kwa MUNGU lipo na kwa shetani lipo. yeye BWANA hataki vuguvugu ko hutapika watu hao BWANA anataka maamuzi kamili na sahihi. tukipoa Moja kwa Moja hatuna MUNGU. ni kanisa lenye tamaa ya Mali tu, lisilo tayari kumtumikia MUNGU kwa vyote lililokuwa navyo. ufunuo 3:17. lazima tukubali mwili, roho vyote viwekeze mbinguni ufunuo 3:18 kwa kumtumikia MUNGU kwelikweli basi tunakuwa tunapata Mali za mbinguni. basi tutubi kwa kutokumtumikia MUNGU kikamilifu na kukubali kukamilika ufunuo 3:19. tuisikilize sauti ya MUNGU na kujitoa kikamilifu naye MUNGU atatushindia. tutarithi pamoja naye. yesu akamaliza mwishoni kuwa yupo mlangoni anavisha hodi kumbe watu wenye uvuguvugu hayupo YESU Kristo ndani Yao ko lazima tukubali na kuamua kununua dhahabu ambayo ni wokovu kutoka kwa MUNGU mkuu wa mbinguni..
MUNGU ....alibariki... neno... lake. .amen.
Comments
Post a Comment