Part 02:KIVULI CHA YAJAYO

 Kabla haujasoma ujumbe huu,itapendeza ukisoma sehemu ya kwanza ya hili somo linaitwa KIVULI CHA YAJAYO.

Unaweza kulisoma kabla ya hii part 02 ili tuweze kupata ujumbe uliokamilika zaidi.


Kwanza nimalizie somo lililopita kwa kitu kimoja.

  Ufalme wa MUNGU(wokovu) utashuka kwetu pale tu kwanza tukikubali udhaifu na kuhitaji msaada.udhaifu ni Sheria ya torati.ko kamwe hatutastahili agano la wokovu kama hatujakubali kufuata Sheria ya MUNGU kwanza na kushindwa...(Tunajifunza zaidi)


Luka 17:20-21

Tunaona kuwa ufalme wa MUNGU ulikuwa katika Israel kwanza kutokana na uwepo wa torati(Sheria). ufalme inamaanisha utawala ko inamaanisha kwamba ukianza kujitahidi kuzifuata Sheria za MUNGU Kuna dalili kwamba unatawaliwa na MUNGU.ko inamaanisha kwamba lazima tuzifuate Sheria za MUNGU kwanza hapo ndipo ufalme(utawala) wa MUNGU utakuwa kwetu.


Mathayo 21:43 lakini YESU anakuja kusema Tena kwamba ufalme wa MUNGU utaondolewa kwenu kwa kuwa hamzai matunda ya kifalme na watapewa watu wengine..hii ni ole!!.(Tutaendelea zaidi)


       ko hapo tunakuja kujifunza kuwa Sheria ndiyo inayoshusha ufalme wa mbinguni rohoni mwetu lakini neema ndiyo inayosababisha ufalme wa MUNGU kuzama matunda maishani mwetu. Ko tunaona kidogo kuwa kwa Nini biblia Ina maagano yote mawili japooja ni kuukuu lakini yote yapo kwa kuwa yote Bado ya afanya kazi katika wokovu wetu.na MUNGU anayatumia yote katika kutufanya sisi kuwa watumishi wake.

Turudi nyumba kidogo  Luka 8:18. Ili upate wokovu lazima uwe na Sheria kwanza.la sivyo wokovu haukustahili.

      kwa kuwa utimilifu wa wokovu inaundwa katika udhaifu wa Sheria,yaani hakuna neema pasipo Sheria ndo maana adamu na Hawa walipewa neema alafu na Sheria kwani Sheria Ile ndo iliyopima uaminifu wao kwa MUNGU....


Kama nilivyozungumza kwenye masomo yaliyopita kuhusu habari za Sheria na neema..basi hata Leo naendelea lengo ni kuwafanya watumishi wa MUNGU wajue kuwa MUNGU ni nani na wanaabudu Nini na kwa Nini vitu Fulani vipo hivi..sio kwa ajili ya mashindano na dini nyingine,, hapana!! Ni kwa ajili ya kufanya ibada halisi ya roho na kweli na sio kuabudu MUNGU asiyejulikana.maana kama tunashindwa kuelezea ukweli wa imani yetu ambayo hakika ni ya kweli.ni sawa na kuabudu MUNGU asiyejulikana.matendo 17:23. Basi Paulo akaanza kuwajulisha kuwa wanayemwabudu ni MUNGU wa namna Gani..nami najaribu ili hatimaye MUNGU ajulikane na ajidhiririshe kwa watu wote kwa uweza wote katika jina la YESU Kristo na kwa uweza wa ROHO MTAKATIFU maana MUNGU hujidhirihisha kwa waliomtambua tu, ulimwengu haukumjua basi tumjue ajidhiririshe kwetu atufanye kuwa wana.amenπŸ™πŸ™πŸ™....

       you know why I am saying that!! Because we believe correctly.haina haja ya kumtetea MUNGU.kwa kuwa tupo sahihi neno linasema yeye atatutetea.











UBATIZO

Ubatizo ni ishara ya kufa na kufufuka kwa YESU Kristo.ni uwakilishi wa kazi na huduma ya YESU Kristo.

#ubatizo ni ishara ya kwamba Sasa YESU anakufa(unapozama kwenye maji) na kufufuka(unapoibuka kwenye maji).kufa na kufufuka kwa YESU Kristo kunamaanisha kwamba wewe Sasa umeokolewa na YESU kwa kuwa kwa ishara ya ubatizo inaashiria kuokoka kwako..

#marko 1:4.. tunaona ya kuwa yohana alitokea katika nyika akibatiza ubatizo wa toba liletalo ondoleo la dhambi.Yohana alianza kubatiza kabla YESU hajadhihirishwa.

Pia mitume walikaa katika siku ya pentekoste wakaomba,basi ROHO akajidhirihisha kwa ishara,ishara zinamthibitisha MUNGU kwetu Wala sio kwamba sisi tunamthibitisha MUNGU kwa ishara zake,ikiwa hivyo ni laana hiyo.na ndo maana adui anatupata sana kwa kuwa tunatafuta ishara akati kwa Sheria ishara zinatutafuta sisi na zinaambatana na sisi

   YESU alipozaliwa ishara iliyoonekana ni nyota,pia malaika wakashuka kwa wachungaji wale wa makondeni,pia bikira kuzaa mtoto

Alipokufa YESU ishara ikafuatana kwamba jua likatiwa Giza,tetemeko likawepo nchini,makaburi  ya watakatifu yakafunuka,ishara ikamthibitisha YESU.

          basi na sisi kwamba tumeokoka ishara yetu ni ubatizo......

       kila jambo la MUNGU analolifanya kwenye maisha yetu linaanza na ishara!! Kama tulivyojifunza kuwa torati ilikuwa ishara ya wokovu//pia Israel walikuwa ishara ya wakristo wa leo.basi ubatizo wa yohana ulikuwa ni ishara ya ubatizo wa YESU ambao ndio wa ROHO MTAKATIFU.

     basi kama umeokoka ili ukidhi viwango vya kuitwa mtu aliyeokoka basi jambo la kwanza ni kuitimiza ishara ya ubatizo(ubatizo wa yohana) baada ya hapo ndipo utakuwa na vigezo kamili vya kupokea ubatizo wenyewe  kabisa ambao ni wa ROHO mtakatifu.


             ubatizo ni ishara ya kukubali gharama za kuwa wanafunzi  wa YESU.

YESU alifanya wanafunzi kumi na wawili akawabatiza kwa ishara kuwa Sasa ni wanafunzi wake mathayo 28:19 walipobatizwa ndipo walipoitwa wanafunzi wa YESU.kwa hiyo hata sisi tutaitwa wanafunzi wa YESU kama tumebatizwa ubatizo kama YESU alivyo batizwa Marko 10:38-39.YESU alibatizwa ubatizo wa maji mengi basi na sisi tubatizwe hivyo hivyo kwa kuwa yeye mwenyewe alisema tutaweza,kunywa kikombe anyweacho yeye na kubatizwa kama alivyobatizwa yeye.basi walipobatizwa ndipo walipokuwa wanafunzi halali wa YESU basi na sisi tukibatizwa Ina maanishwa kuwa sisi ni wanafunzi wa YESU na tuna haki ya kuitwa wanafunzi wake YESU.

         lakini tukiangalia kwa makini tunaona YESU alisema mtakinywea na ubatizo mtabatizwa.ina maana Bado walikuwa hawajabatizwa na Bado walikuwa hawajanywa kikombe anyweacho yeye.

        Walikuwa wanafunzi wake YESU lakini kwenye warumi 8:14 aongozwaye na ROHO huyo ndiye mwana wa MUNGU..kuongozwa na ROHO ni ubatizo mtu anayeongozwa na ROHO wa MUNGU.huyo amebatizwa kama YESU alivyobatizwa.YESU alijidhihirisha kama mwana wa MUNGU kwa kuwa aliongozwa na ROHO wa MUNGU.aliishi kwa ROHO,alienenda katika roho mapepo walitoka kwa nguvu ya ROHO,mathayo 12:28.ko ubatizo uliokuwa umebaki kwa wanafunzi ndio uliowahamisha wanafunzi kutoka wanafunzi mpaka Wana,kutoka Sheria mpaka neema .

    ni kujazwa nguvu kwa ROHO MTAKATIFU na kwa moto nasi tutaitwa Wana wa MUNGU.katika kufanya kazi kama Wana basi tunapata haki ya kukinywa kikombe alichokunywa YESU basi tunakuwa watumishi wa MUNGU.

Conclusion: ubatizo ni kukubali gharama ya kuifanya kazi ya MUNGU.Roho mtakatifu anajidhihirisha kwa mtu mmoja tu ambaye ana uwezo wa kumdhihirisha katika ulimwengu.mtu anapokuwa na kiu ya kumtumikia MUNGU na kuifanya kazi ya MUNGU asilimia 100  roho mtakatifu atashuka kwake..

       alishuka siku ya pentekoste walikusanyika pamoja pamoja na vitisho vyote kutoka kwa wayahudi kwamba asiwepo wa kumtumikia MUNGU..walitawanyika ila walipokaa pamoja na kuishinda hofu ya mauti na kifo kutokana na upinzani wa wayahudi.wakaipinga serikali kwa ajili ya  upendo na utii kwa maneno ya YESU Kristo.hapo tu walionyesha kiu kuwa wapo tayari na matunda ya kiu Yao ikawa ni kupokea nguvu.

Utapewa ahadi lakini lazima ukidhi viwango na vigezo vya kupokea ahadi..kwa hiyo kiu anayosema kuiunda ili roho mtakatifu ajifunue ni kuwa tayari kuchukua gharama na Nia ya kuifuata Sheria.

Sisi tunahitaji nguvu ya ROHO kwa ajili ya Nini?? Peleka hoja yenye nguvu kwa BABA wa mbinguni...(Ninakumbuka maneno ya pastor)




          je unastahili kuitimiza ishara hii ya wokovu?

      Mathayo 3:7..wale mafarisayo wakaja ili wabatizwe.ila hawakuustahili ubatizo ule..yohana akawaambia je mnahisi mwaweza kuikimbia ghadhabu Ile inayokuja kwamba mbatizwe wakati Bado ninyi ni uzao wa nyoka?.

Lazima uyajue mema na mabaya,halafu kigezo Cha kuhalalisha ubatizo ni kwamba unaamua kuyachagua na kunia mema tu.kama unajua mabaya na mema afu hujaamua kuacha mabaya Ina maana Bado hujabatizwa kihalali wewe ni haramu.ni mkristo haramu.

       ko ubatizo ni tendo linaashiria maana kuu sana za rohoni.ni ishara inayohalalisha kujikana kwako na kijithibitisha na kuthibitishwa kwamba wewe ni mtu wa MUNGU.kwa kuwa kweli umeamua kubadilika.yaani umeamini mambo ya YESU tunapata haki ya kubatizwa alafu unaokoka.wengine tunakuwa hatujaamini(kwa matendo na utakatifu na kujikana) afu tunabatizwa hapo kipengele Cha kuokoka ni kigumu haijalishi tumeipitia ishara ya ubatizo Bado tunakuwa hatujakidhi.

        maana tukibatizwa tukaendelea kutenda dhambi ishara inakuwa na sisi lakini inakuwa ni ishara mfu kama ishara ya Yona,yaani ishara IPO ila inakuwa imekufa.tukibadilika tunaifufua ishara upya ko ishara inakuwa halali kabisa.ni kutiana moyo ili tuendelee kukua zaidi na zaidi.but as more we don't know a last minute!! Better to tune ourselves right after babtism!!. ni thawabu kubwa mno.


     ni sawa na kunywa maji ya uzima ila upo hai kimwili Yale yatapita tu kwa mkojo.mpaka mwili ufe ili utunze maji ya uzima yatakayokufanya  usifanye dhambi Tena(ni mfano tu wa maelezo hapo juuπŸ‘†.






Some hint!!

      wagalatia 6:7 apandacho mtu ndicho atakachovuna.wale mafarisayo walikuwa na matunda maovu kwani Sheria tu hawakuifwata wakafuata maagizo ya wanadamu wakatunga wakapotosha Sheria ya MUNGU wakawapotosha watu wa MUNGU kwa Sheria hiyo Marko 7:6-12...Hawa walikuwa na matunda mabaya ni nyoka Hawa....yohana aliwaambiaje?? Zaeni matunda yapasayo toba.. mathayo 3:8..palipo na kitu pataongezewa Bali pasipo na kitu hata kidhaniwacho  kuwepo kitanyang'anywa Luka 19:26.

      hii Inamaanisha ili uitimize haki yote jambo la kwanza lazima uwe na haki.kubatizwa ni kuitimiza haki yote mathayo 3:15. Ili upngezewe haki basi lazima uwe na haki.

Hapa tunajifunza kuwa kumbe ishara ya ubatizo inatuongezea na inatupa haki ya kuitwa watu wa MUNGU kwelikweli kwa kuwa tunamsikiliza baba yetu.

Sasa wale mafarisayo walikuwa na shida Moja tu kwamba walitaka waitimize Haki yote wakati huo mioyoni mwao walikuwa hawana hata haki.walikuwa waovu kabisa ko wangejaribu kubatizwa tu wangevuna laana kwa kuwa wanapanda laana.

    hata na sisi tunapojihudhurisha karibu na MUNGU tukiwa wachafu tunajitengenezea laana katika maisha yetu wenyewe na tutakataliwa hakika kwa kuwa tunaujua ukweli ila tunaukataa.

Jambo la kwanza waliloambiwa ni kwamba waanze kuzaa matunda yapasayo toba,wapande mema wapate mema hapo wataongezewa haki na MUNGU wa mbinguni. Mwenye haki atazidi kupata haki kutoka kwa MUNGU Bali asiye na haki hata aliyonayo atanyang'anywa.ko njoo kwa MUNGU kwa utakatifu kwa kuwa ukichanganya uovu na wema hata ule wema ulionao utanyang'anywa ndo maana tunasema kwa MUNGU ukikosa kimoja unakosa vyote..

    basi watu wa MUNGU tujue umuhimu wa kunyenyekea na kujishusha mbele zake kushuka na kutubu na kutetemeka mbele za MUNGU kwani MUNGU huwaangalia watu kama hao isaya 66:2.

###let' s continue na somoπŸ™πŸ™πŸ™.




ubatizo wa maji ni Sheria ya MUNGU ambayo Kila mtu anapaswa kuitimiza kama ameokoka na amejaliwa kusikia neno hili la MUNGU.

     petro alipoenda kwa kornelio alipokuwa akiongea habari za YESU kwa wale watu wale watu wakabatizwa kwa nguvu ya ROHO mtakatifu kabla hata hawajabatizwa kwa maji(ni neema ya MUNGU kwa watu wale) lakini Hilo jambo halikumfanya Petro(mtumishi wa MUNGU) awape uhalali wale watu kwamba wapo tayari,, matendo 10:44-48.akauliza"nani azuie Hawa watu wasibatizwe!!" Kwa Nini aliuliza hivyo kwa kuwa MUNGU wa mbinguni anatukuzwa pale tunapoitii Sheria yake kwa usahihi inavyopasa..basi ubatizo ni Sheria na yohana alikuwa ndiye Musa wa Sheria hiyo..basi upungufu wa Sheria hiyo unatilizwa katika nguvu ya neema mpya ambayo ni unatizo wa ROHO MTAKATIFU.


MEZA YA BWANA.

     meza ya BWANA pia ni lazima ifanyike ishara kwanza ya kumkumbuka YESU alichofanya ule usiku wa pasaka maana ishara ni muhuri ya neema yenyewe 1 korinto 11:24-25,luka 22:15-20. Ko ukumbusho huo wa ishara kwa kula mfano wa divai(kinywaji) na mkate(chakula) ni kwamba tumeula mwili wake ambao inamaanisha ni uzima kwetu,hii ishara tunaifanya mara baada ya kuongezeka kanisa tunaishuriki wote ili ifungue njia ya rohoni kabisa kwamba neno lake YESU (tunalofundishwa) ambalo ni chakula cha uzima lizae uzima na lijae na nguvu mno ya kubadilisha maisha yetu ko kula meza ya BWANA ni kufungua njia ya watu kulitendea kazi neno la MUNGU ili wapate uzima ulio ndani ya YESU.NA kwakuwa tumeshafungua mhuri kwa ishara takatifu hii basi tutaanza kumwona YESU kwenye maneno yake yote kwa kupitia watumishi wake wote hatimaye tunakuwa watakatifu.




    kwa kuwa neema ya MUNGU inakamilishwa na upungufu wa Sheria..na tunaishi katika neema kwa kupitia sheria.na ndio maana tunapojifunza tunazungumza Sheria za MUNGU ambazo ndizo zitathibitisha kuwa tupo kwenye neema kweli kweli.

    ndo maana tunasema ili umwone YESU usitende dhambi kwani dhambi imefunuliwa na sheria warumi 7:7.

        ina maana kwamba tukisipofuata Sheria hatupo kwenye neema.maana ili uikute neema lazima uanze na Sheria kwa kuwa utimilifu wa neema unaonekana kwanza mahali palipo na msingi wa udhaifu wa Sheria warumi 8:2

    kama nilivyosema kwenye masomo yaliyopita kwamba hiyo ni mojawapo ya sababu kwamba YESU alishuka Israel. kwa kuwa nyumba(wokovu) inajengwa katika msingi ambao ni Sheria ya MUNGU.. mathayo 7:24.neno la MUNGU ni Sheria ko asikiaye maneno ya MUNGU na kuyafanya(kutenda Sheria ya MUNGU) atakuwa amejenga nyumba(wokovu) katika msingi imara(Sheria ambayo ndiyo neno la MUNGU) (tukirejea somo Lile la mwamba,msingi,nyumba) ambayo yalimaanisha MUNGU baba, YESU Kristo,roho mtakatifu).hapo tunakuja kuona maadamu tunamwamini MUNGU wa mbinguni (tunajenga katika mwamba) basi uimara wa wokovu wetu hautokani na uzuri wa nyumba Bali unatokana na uimara wa msingi(YESU) ambaye ndiye Sheria.(Ambayo Sheria hiyo ni neno la MUNGU...

na ndo maana wapo wengi Wana wokovu unaojithibitisha kwa watu kwamba wapo ni watu wa MUNGU lakini wakati huo wamekataliwa kwa kuwa  hawana msingi imara (hawajajizatiti kulitendea kazi neno la MUNGU ambalo ni Sheria) basi mvua ikinyesha na mawimbi yakiupiga huo wokovu wao wanaanguka mara!!..hata sisi tunaanguka mara nyingi kwa kuwa hatuna misingi ya neno katika maisha yetu ko tunamkosea MUNGU kwa Hilo.

     1 yohana 5:9 kupitia somo Hilo tunakuja kujua ni nini maana ya utatu mtakatifu,MUNGU mmoja tu katika udhihirisho wa namna tatu.(research somo la kuweza kulitendea kazi neno la MUNGU)

hint==pasipo YESU Kristo mwanadamu anakuwa chini ya Sheria..Ina maana hautakuwa na wokovu.kama ilivyo pasipo msingi hapana nyumba..kama tunataka kuwa juu ya Sheria basi kwanza kunakuwa na kipengele Cha kumkiri YESU na kumwamini(imani pasipo matendo imekufa) alafu tukabatizwa(ishara na uhalisia ambao ndio roho mtakatifu) basi hapo Moja kwa Moja ndipo tunakuwa na haki ya kusema tumeokoka Marko 16:16.




##SABATO..

Kabla ya yote nilisema maadamu tunayo Nuru na mwili basi kivuli lazima kionekane.

na kwa kuwa sisi tunautambua mwili(kristo) basi ili tujue kuwa tuna nuru tuangalie tuone kivuli je tunacho?


Mambo ya Walawi 25:8 Nawe utajihesabia Sabato saba za miaka, maana, miaka saba mara saba; zitakuwa ni siku za Sabato saba za miaka kwenu, maana miaka arobaini na kenda. Hii ni sabato ya kwanza kabisa kwa wana wa israeli.mwaka wa hamsini uliitwa mwaka wa yubile yaani mwaka wa maachilio yaani mwaka wa uhuru kwa watumishi na uhuru wa watu.


    ya kwanza kabisa ilikuwa ni sabato baada ya siku sita kufanya kazi basi siku ya saba ni siku ya pumziko kamili na kutaniko takatifu lilifanyika katika hema ya kukutania,wengine wanapumzika kazi tu hawampi siku BWANA,pumziko alilolotaka BWANA ni kukaa katika nyumba yake.


Siku hizo sita sio tu kwenye kazi yako bali fanya kazi zako ikiwemo na kazi alizokupa BWANA nyingi mno pamoja na za kwako ila siku ya saba ni siku ya mapumziko ya kazi zako na kufanya ya MUNGU tu(kukaa uweponi mwa MUNGU tu!!.


Mwaka wa sita wana wa Israel walilima walivuna mazao ya miaka mitatu kabisa,mwaka wa sita,wa saba(mwaka wa sabato),mwaka wa kwanza tena wakati wanaanza kulima upya.huo ulikuwa ni muujiza na baraka za MUNGU kwa wana wa Israel sasa inashangaza sisi kweru hatumtafuti MUNGU kwanza ndo maana hatuzidishiwi baraka za MUNGU kamwe mathayo 6:32-33.


Jambo la muhimu la kulinoti ni kwamba katika kivuli siku ya saba ilikuwa ni siku ya sabato.

Ile ilikuwa siyo sabato kamili japo siku ya saba hata sasa tunaisimamia(jumapili hadi jumapili kwa sisi wengine jumatatu hadi jumatatu,jumamosi hadi jumamosi, ijumaa hadi ijumaa nk) hizo ni siku za saba maana BWANA MUNGU alipumzika na akaibariki siku ya saba kabla haijakuwepo sabato yaani mwanzo kabisa.mwanzo 2:2-3

Hakuibariki jumapili wala jumamosi wala ijumaa bali aliibariki siku ya saba inamaaanisha kama ishara ya yeye bwana MUNGU kupumzika baada ya uumbaji akawapa sabato Israel siku ya saba kama kivuli cha sabato yetu sisi ambayo ni wokovu(kuokolewa mbali na dhambi), ebrania 4:9-11.na hii ndio starehe yetu kwa kuwa tulikuwa tunatumikishwa sasa sasa tumepumzishwa mbali na dhambi na si mbali na kazi kama kivuli kilivyokuwa. 


Kuna wengine wana siku ya saba ila hawana sabato wameshika siku na sheria tu,hawana utimilifu wa sheria ambao ni YESU,

Kuna siku ya saba afu kuna sabato.mara ya kwanza katika kivuli siku ya saba ilikuwa ndiyo sabato, kutoka 20:10-11.

Lakini kwetu sisi(agano jipya) tuna siku ya saba afu tuna sabato.sabato haikuwa siku,ila siku ya saba ni siku,ila kutokana na amri ya MUNGU siku ya saba ikawa SABATO.


Maana ya sabato ni pumziko na starehe,ko kwa kuwa MUNGU katika siku ya saba alipumzika na kustarehe ina maana ilikuwa ni sabato kwake.kwani alitoka kufanya kazi.


Pumziko ina maana ni kutoka kufanya kazi ndipo unapumzika baada ya kuchoka.naye MUNGU alipomaliza kazi yote ya uumbaji akapumzika na kustarehe na kufurahia alivyoviumba.



Mwili ni kuvuli cha roho kama ilivyo kwamba torati ni kivuli cha kristo.ko mwanzo MUNGU aliyadhihirisha mambo ya rohoni kimwili(moto kushuka,bahari kutawanyika,sabato,vyakula etc) lakini sasa MUNGU anayadhihirisha mambo ya rohoni kiroho.

#kama ilivyo kwamba ili mwanadamu awe roho kamili(ya kwenda kwenye hukumu ya MUNGU Aidha jehanum au mbinguni, inabidi afe mwili.afe ndipo aende rohoni.ndivyo ambavyo MUNGU aliuumba mwili(kivuli),(utawala wa Sheria!!) Ili mwili uishi,ufe pamoja na YESU Kristo pale msalabani ili mwanadamu aanze kumwona MUNGU kiroho na si kimwili tena.

(Ko agano la kale ni njia ya kufikia agano jipya)

#ili umwone MUNGU rohoni ni lazima ufe mwili wako wa zamani wa sheria na kujilazimisha na kinachouua mwili ni Kristo mwokozi anayedhihirika katika pendo.

Kwani mwisho wa mwili ni kifo na baada ya kifo roho ya mwanadamu ndiyo inaenda hukumuni,vivyo hivyo sheria ni mwili ambao inabidi ufe(kupitia YESU Kristo) ili mwanadamu aingie kwenye neema ya YESU Kristo na ROHO MTAKATIFU.

Ndio maana kuna utofauti wa ishara za MUNGU kati ya agano la kale na agano jipya.agano jipya tunatamka kwa jina la YESU Kristo Aliye roho,wakati huo agano la kale walitumia uponyaji wa ishara za kimwili kama kutumbukia majini(naamani na Elisha),kumlalia mtoto kiungo kwa kiungo ili afufuke (eliya na mwanamke mjane),kutumbukiza mti ili shoka lielee(elisha na wana wa manabii,kupiga mwamba ili yatoke maji(musa na Wana wa Israel),ni ishara za kimwili hizo za kumdhihirisha MUNGU, lakini sisi tuna ishara za kiroho za kumdhihirisha MUNGU ambayo ni jina la YESU Kristo tu kupitia nguvu ya ROHO MTAKATIFU!!


Ko ukiona kuna watumishi wanaotumia ishara za kimwili kama maji,mafuta(eti kama daudi alivyosimikwa),keki,chakula,soda,kitambaa,pete,na vyote.ujue kwamba siyo MUNGU aponyaye hapo,kwani kwa sasa MUNGU hatupo kwenye vitu au mtu binafsi bali kila mmoja ana mamlaka na anahusika kwenye uponyaji na miujiza ndo maana hata YESU alipo taka kumponya mtu alitaka imani ya mtu huyo(akasema imani Yako imekuponya),zamani walifanya tu bila hata ya watu kuamini.kwa mfano wana wa Israel hawakumwamini MUNGU ila MUNGU alijidhihirisha kwao .sasa ukisipomwamini YESU huna namna ya kupokea vitu vya thamani kutoka kwake.

     tumepewa jina moja tu nalo ni jina la YESU  matendo 4:12.

Kuomba na kuombea kwa jina la YESU,kuwa na upako wa YESU tu na siyo mafuta wala ishara wala nguo.

     note: uponyaji wa YESU unamfuata mtu mwenye muunganiko nao,ndo maana walimgusa wengi kwenye nguo,ila yule aliyetokwa na damu ndiye aliye pata uponyaji kwa kuwa alikuwa na imani ya kupokea muujiza,wakati huo wengine walikuwa na imani ya kumwona YESU tu 

Je umemwona YESU,umepokea muujiza kutoka kwa YESU?! Jiulize upate jibu ndugu yangu.


Kama ni uponyaji wa ishara (kama ule wa agano la kale)(kama yesu alivyopaka tope kwa macho mtu akaona) ni ufunuo wa kipekee sana wa emergency ambao MUNGU anautumia kujidhihirisha, wakipekee mno,ni unatokana na mawasiliano imara ya ndani kati ya mtu na MUNGU.kwa mfano mdo 5:15,mdo 19:11-12, hiyo ni miujiza kupita kawaida inayotokea kwa ishara za kimwili,lakini matendo ikasema ni miujiza kupita kawaida kupitia jina la YESU na inafanyika kwa kusudi maalumu la MUNGU mwenyewe na si mapenzi ya mtu,kwani ile miujiza ilimshangaza hadi paulo akamtukuza MUNGU kwa yaajabu hayo sasa saivi ile aina ya udhihirisho wa MUNGU wa ajabu, shetani anajaribu kuwafunga watu macho ili matendo ya ajabu ya MUNGU yaonekane ni ya kawaida,kwa mtu aliye macho miujiza ya MUNGU ni dhahiri na ya shetani ni dhahiri.hata adui aige vipi miujiza yake haifikii utukufu unaoletwa na miujiza ya MUNGU inayofanyika ikamshangaza hata inayofanyika kupitia yeye(mtumishi wake) sasa adui anafanya mambo ya mafuta na ishara kama ndo utaratibu wa uponyaji wakati kwa MUNGU uponyaji si jambo la aina moja,kama YESU alivyoppnya watu tofauti kwa aina tofauti.

     pastor alitoa mfano mzuri naweza kuutumia "mkoma alisema ukitaka waweza kunitakasa YESU akasema "nataka takasika"😁 luka 5:12-13,marko 1:40.

Akamshangaza mkoma.kwamba jinsi unavyohitaji YESU anafanya zaidi.


MUNGU anaponya katika namna itakayo mshangaza mtumishi wake na mponywaji.

Muujiza wa MUNGU unatokea kutokana na mazingira ya mwombaji na mwombewaji(hata ukiomba mwenyewe ukachukua nafasi hizi zote mbili)

Sasa eti unaenda kwa manabii unajua kabisa et ntaponaje eti kwa mafuta na maji ya upako.

Au kwa jinsi ulivyomzoea pastor wako na MUNGU wako unaenda ushamuwekea mpaka kwamba nikiombewa nikinywa na dawa ntapona polepole sawasawa na dawa(hapo imekuponya dawa na sio MUNGU) ndo maana hautashangazwa, ila utajishangaza na kumshukuru MUNGU kwa yote na sio kwa jambo alilokutendea(hiyo ni imani haba na tena ni imani nusu),au unaenda kuombewa unatarajia uponyaji wa baada ya wiki,mwezi au mwaka kutokana na ukubwa wa tatizo lako, MUNGU anakushangaa na shetani anakushangaa maana mamlaka ya kusimamisha milima na kuhamisha unayo mwenyewe na sio pastor au any mtumishi.

       yule Aliye tokwa na damu kwa miaka mingi aliweka imani kwamba atakapogusa pindo la YESU atapona akapona wewe unaamini nini unapomwendea YESU peke yako(hii ndo nzuri zaidi) au unapomuendea mtumishi wa MUNGU(nyongeza hii)

Kumbuka YESU alipofika mahali hawamwamini hakufanya miujiza mingi huko mathayo 13:54-58.

Wanamjaji YESU na kumkadiria na kumuwekea mipaka,hata na sisi tunapomuwekea YESU mipaka hafanyi miujiza mingi atafanya michache kweli,tutakuwa wa kawaida tu kama tulivyoleo.

Miujiza ilifanyika kama nyongeza ya neno,lakini wengine wengi wanasafiri na kutenda miujiza ili kuweka brand yao yaani watu wawaone wao ila wasimuone MUNGU.

YESU alipomfufua lazaro watu walimtukuza MUNGU kwa kuwa miujiza ni sehemu ya huruma za MUNGU,sasa inashangaza kwamba sasa miujiza inatumika kama biashara na brand za mikutano,ko watu wanakuja wamejiandaa kuona miujiza ya YESU na si kumuona YESU yaani kimekuwa kizazi cha ishara,kimelaaniwa.

MWAMBIE YESU KRISTO AKUSHANGAZE KWA MIUJIZA YAKE.!!!!....


,.,.,.,...,.........,.,.,.,.,.,.,...,..,.,..........,.,.,.,.,.,.,.,...,,.,.,..,,..,,.,.,.,.,..,.



Tuendelee na somo kuhusu SABATO sasa...

Je wewe una sabato? Naam YESU Kristo ndiye BWANA wa SABATO.marko 2:23-28.

Yeye ndiye BWANA halisi la pumziko (pumziko la kupumzishwa na dhambi).

#mafarisayo walichanganganya walidhani kwamba mwanadamu aliumbwa ili apumzike kazi na vyote vya mwilini siku ya saba(yaani sabato) kumbe pumziko lilikuja kwa ajili ya mwanadamu baada ya mwanadamu kutumikishwa na shetani. sasa anapewa sabato ili awe huru.

Walidhani sabato ni siku ya kuacha vyote kwa ajili ya BWANA kumbe sabato ni maisha ya mtu aliyeokoka.


Lakini kuna siku ya saba ambayo hiyo inapasa iwe ni ya BWANA maana siku ya saba ilikuwepo mara tu baada ya MUNGU kuiumba mbingu na nchi.hiyo ni lazima mwanadamu aitoe kwa ajili ya BWANA  kwa kukusanyika hemani ni ishara ya BWANA kustarehe baada ta kuiumba mbingu na nchi.

Kustarehe kwenye siku ya saba kuna maanisha kuwa huru kutoka kwa kazi zako binafsi(za utaratibu wa maisha za faida yako). labda kufanya kazi njema za emergency kama punda kutumbukia siku ya saba,mtoto kupotea,kupika,kula na kazi njema tofauti na utumwa wa mali(uumbaji) na cha muhimu zaidi kujitoa kwenda kwenye hekalu la MUNGU kumwabudu kumshukuru kwa ajili ya starehe aliyowapa.ko siku ya saba inaadhimisha wokovu wa thamani.


Je ni ipi warumi 14:5-6 siku zote ni sawa(hii ndiyo nguvu) tofauti na wengine wafanyao tofauti kati ya siku na siku(dhaifu,) ko kana tuna nguvu basi tusimdharau asiyeadhimisha kama sisi kwa kuwa naye aiadhimisha kwa MUNGU.ko kujihesabia haki kutokana na makosa ya wengine huo ni ufarisayo pure,sisi tuwe mfano kwa kuwapenda wote ili nao watambue udhaifu wao kupitia nguvu yetu na sio hukumu yetu kwao.je wana sabato ya Sheria na sabato ta neema? Wengine wanayo yote na katika udhaifu huo wanatiwa nguvu kwelikweli kwa kuwa wanaashiria kumheshimu MUNGU sana kimwili na kiroho.japo umakini unahitajika kwa kuwa wanatembea katika udhaifu ni kwamba shetani ana uwezo mkubwa wa kuwaangusha kwa matakwa yake mwenyewe na kuwapooza kupitia udhaifu wao wa imani.ndo maana kwa mfano wasabato wanakumbwa na hali ya kuwa mwilini zaidi kuliko kuwepo rohoni kutokana na kujihesabia haki kwao na hukumu yao japo wapo kwenye udhaifu mkubwa.ila wakiushinda huo kwa kutambua SABATO na siku ya saba.watavishwa nguvu mno ko tuwaombee sana wenzetu.

Barikiwa sana!!!!!


CHAKULA NA VINYWAJI.

hiki ni kipengele cha mwisho naweza nikamalizia.

Warumi 14:17.

Je wewe mtumishi wa MUNGU unaelewa nini kuhusu hapa zaidi?


Naweza kuongeza warumi 3:20 na wagalatia 4:24 kwa ajili kujifunza zaidi.

MUNGU NA AKUSAIDIE UPATE UELEWA WA KWELI ZAIDI KWENYE KIPENGELE HIKI.

      My name:Amani Ernest kyamba

         SOGH TEAM 

          Let's do GOD'S work together.




Comments

Popular posts from this blog

A.Kuweza kulitendea kazi neno la MUNGU

Je kwa nini namna ile?

Mwamuzi(short notes)