Kuitambua neema(short notes)


24 Sep 2024

Jinsi ya kuulinda utakatifu

​Utakatifu ni usafi kuanzia ndani (mawazo) mpaka nje. yaani mbegu ya mhindi haiwezi kuotesha maharage hivyo kama una mawazo ya kufisha ndani ya akili haijalishi unajizuiaje Bado hujashinda kwa kuwa utakatifu wa kweli unaanzia ndani.

​Unajua kwa Nini Wana wa Israel walishindwa kulifuata Sheria ni kwakuwa walitaka kuwa wazuri lakini chemichemi za mioyo yao zilitoa mambo maovu,, ikijaa chemichemi lazima maovu yatadhihirika na ndio maana tukiishi katika wokovu wa Sheria tunatoa maovu yaani tunaondoa maji ya chemichemi chafu ko yanaanza kujaaa Tena.. mda wote huo tutajiona watakatifu na wenye kumpendeza MUNGU lakini pale tu chemichemi ikijaa uovu unadhihirisha nguvu tukaanguka tena.

Warumi 7:15..

​Je Nini tufanye ili tukamilike katika utakatifu? Ni kwa kufisha chemichemi chafu za asili ya Dunia hii za dhambi kwa kujitoa kikamilifu kwa MUNGU kupitia YESU Warumi 12:1.. kwa kuvuviwa (kuunda kiu ya kuacha dhambi) ambako ndiko kunamwita ROHO MTAKATIFU aliye msaidizi mfishaji wa mambo ya mwili.

​*Sisemi kwamba uliyemkiri YESU Kristo kwamba hauna ROHO,, hapana kabisa.. ukisha mwamini YESU Kristo unakuwa na ROHO mtakatifu tayari. lakini shida inakuwa ni kwamba huyo ROHO mtakatifu hajatukuzwa ndani ya mtu kutokana na kutawaliwa kwa asili.. kutukuzwa kwa ROHO MTAKATIFU ni pale mtu anapoamua kuchukua gharama halisi za kuuishi wokovu. sasa wengi tunaishi maisha ya wokovu bila ya kuchukua gharama kwa kujikana.. mathayo 16:24.

​Kujikana ni kutambua gharama za upendo wa YESU Kristo mwokozi kwa maisha Yako na kuamua na wewe kutambua gharama za kumpata yeye YESU Kristo mwokozi na masihi. na huu ndio upendo... ambao utafanya ROHO MTAKATIFU adhihirishwe kwa ulimwengu asibaki kwako tu.. maana wengi ROHO tunaye ila hatujamtambua kwa kuwa hatumjui na pia hatumfwati. yohana 1:10.. lazima ili watu wa nje wajue kuwa una YESU Kristo kwanza wewe mwenyewe uweze kuithibitisha kwamba una YESU KRISTO.. la sivyo itakuwa ni injili bubu isiyoponya.

​*Wengine wanatamani na wanajua tu kwamba ishara na muujiza ndio udhihirisho wa nguvu za ROHO MTAKATIFU pekee wakati hawajajua kuwa neno la MUNGU linasema ishara zitambatana na waaminio Marko 16:16.

​Ngoja nipafafanue... kabla wanafunzi hawajatimilika katika pendo walikuwa ni waaminio pekee.. walikuwa na ROHO MTAKATIFU ambaye hawamjui..

​*Ndo maana walikuwa na wokovu bubu kwani shetani aliendelea kuwatesa na kuwatumia mara kwa mara mfano mathayo 16:13-23 Petro alitumiwa na ROHO na pia na shetani kwa wakati tofauti tofauti ni kwa kuwa hakukamilishwa katika pendo (neno).. kwa kuwa Bado alikuwa na chemichemi chafu.. japo aliamini.. na ishara ziliambatana nao luka 9:1.. lakini hawakuwa wamesajiliwa katika mbingu kama wateule mpaka walipoondoa na kuushinda mwili kwa kumtazamia YESU Kristo pekee hapo ndipo wakasajiliwa mbinguni.. ko usidanganyike na miujiza na ishara za wajiitao watumishi akati matunda Yao na ushuhuda wao unamkana MUNGU.. tambua matunda ambayo ni matendo na ROHO wa MUNGU uliye naye atakusaidia katika jina la YESU Kristo katika MUNGU baba.

​Amen!!!

​Tutaendelea zaidi na zaidi polepole mpaka YESU Kristo atupe kibali Cha kuitwa Wana wake katika ROHO warumi 8:14.. kama Kuna sehemu hujaelewa tusihofu!!

​Mwombe MUNGU wa mbinguni aliye tegemeo letu.. na usisite kuniuliza ili tendelee kumwomba MUNGU kwa pamoja kupata majibu ya yote tusiyoyajua katika mfululizo wa masomo haya.. Mimi na wewe tunaweza.. hebu tuamue na kumrudia MUNGU wetu na hakika ataturudia sisi.

BLESSED YOU ALL

​*This is a SOGH..

*A.E.Kyamba

Let's do GOD'S work together...

In holy name of Jesus Christ our saviour. Amen


Comments

Popular posts from this blog

Kuweza kulitendea kazi neno la MUNGU

Mwamuzi(short notes)

Je kwa nini namna ile?