Kumpenda MUNGU kwa yote
Hii ni mwendelezo wa somo la "usijidharau"
12 Jan 2025
Kumpenda BWANA YESU kwa vyote. (Part 02 ya usijidharau)
Mathayo 22:37.
Yule mtu YESU akampenda kwa kuwa amezishika amri zake na kwa kweli alikuwa anamtumikia MUNGU.
#yesu akampenda sana mno akatabasamu akafurahi na pia akamwonea huruma.
#akaona upendo wake kwa kweli umewekeza kwenye vyote kasoro Mali zake kwa upendo wake YESU akataka amkamilishe hicho kimoja akamwambia gawa nusu ya Mali zako uwagawie maskini hapo utakuwa kamili yule mtu akaondoka kwa huzuni nyingi kwani alijijuwa kuwa kweli hajakamilika!!.
#hata pale YESU alikuwa anaangalia wanavyotoa sadaka akawa anaupima upendo na sio utajiri ndo uliowafanya wale matajiri wasimwone MUNGU kwa kuwa kutoa kwao kulikuwa ni kwa Sababu ya utukufu wao kwa watu na sio upendo na moyo wa kimungu, ila yule mama mjane alitoa sadaka ya moyo. maana moyo wako ulipo ndipo na sadaka Yako itakapokuwapo mathayo 6:19-21. mama moyo wake ulikuwapo kwa MUNGU ko na sadaka yake ilikuwa kwa MUNGU. matajiri moyo ulikuwa kwa Mali ko walizitolea Mali zao sadaka.
#ila itapendeza sana uwe tajiri na ujitoe kwa vyote kwa pamoja kwa ajili ya MUNGU itakuwa ni thawabu. Zuri sana.
#kati ya 50/100 na 500000/1000000 zote ni nusu ila ni nusu tofauti kwa hiyo kwa MUNGU mbinguni zinaenda sehemu ya upendo yaani nusu, robo na nyingi ndiyo sadaka na sio wingi wa mali. ko utukufu wa Mali ni wa mwanadamu ila sehemu ya upendo ndiyo sadaka kuu.
#Ndo maana 1 korinto 13:1 sadaka bila kuwa na sehemu ya upendo ni Bure.
#kwa mfano akina tajiri kama Elon musk akatoa milion 10 kama sadaka (kwa mfano angekuwa ameokoka) ingekuwa ni sadaka kubwa kwa wanadamu ila haina maana kwa MUNGU kwa kuwa ukisamehewa kidogo lazima upende kidogo na kadharika katika uliyobayo unatoaje?
Jiulize!!
Wengi hatupati karama na huduma kwa kuwa tunapoomba MUNGU anakuja anaangalia ndani ya mioyo yetu anaona tamaa ya heshima na udanganyifu wa kidunia ndio vipaumbele kama ni hivyo Ina maana hatuna upendo mathayo 6:33-34. mungu anaangalia moyo kwa hiyo hatuwezi kumdanganya kwa namna yeyote lle na upendo uliozungumziwa ni ule wa 1 korinto 13:1.
#unafanya kwa ajili ya Nini, wewe ni maskini, tajiri, mtumishi, bosi, mzungu, mwafrika, jiulize unasababu Gani ya moyo?. hiyo ndiyo itamwita MUNGU kwako na sio utajiri na utaratibu wa utofauti wetu. ko usijidharau!!
Blessed!!
This is a SOGH!!
Let's do GOD'S work together
Kyamba.E.A
Mr SOGH.
Comments
Post a Comment