Kwa nini umeokoka?

04/02/2026

Kwa nn umeokoka?/mtazamo wako ndio unaokuvuta!!

Fellow SOGH Amani Ernest Kyamba

​Je ni kwa Sababu unaikimbia dhambi au ni kwa Sababu unataka umwone MUNGU..ukimwona MUNGU Moja kwa Moja utakuwa umeikimbia dhambi. watu wengi wanaokoka ili kuikimbia dhambi jambo ambalo linamweka MUNGU nafasi ya pili kwenye maisha Yao kwa kuwa wanataka kuikimbia dhambi ili kwa hivyo wamwone MUNGU. akati wokovu dhamira yake kuu ni kumwona MUNGU. kwa kuwa kumwona MUNGU na kumtafuta ndiko kuishinda na kuwa mtakatifu. ukisema kuokoka ni kuikimbia dhambi ambayo ni asili Yako kwa kweli hauwezi wewe peke Yako kwa kuwa ni asili ya mwili kurudi mavumbini, yaani kutenda dhambi kwa kuwa ukiweka dhamira kwa mtazamo wa chini basi lazima huo mtazamo ukurudishe chini.

​YESU alisema aliye wa juu huwaza yaliyo ya juu na hufikiri yaliyo ya juu tu wakolosai 3:2. Usiwe motivated na ulikotoka Bali kuwa motivated na ulipo na unaokwenda kwenye maisha ya kiroho na mwilini pia, maana MUNGU peke yake ni WA tangu milele, Leo, na hata milele ebrania 13:8. lakini mwanadamu ni WA Leo tu na anapoona kesho, anapopatarajia tu sio alipotoka na hiyo ndiyo imani.

Fellow SOGH Amani Ernest Kyamba.

​Paulo mwenyewe anatufundisha kuwa anaendelea kupambana Leo (present) kwa kuwa Kuna mede imewekwa kwa ajili yake wafilipi 3:14. Hakusema kwamba ni kwa Sababu anaikimbia jehanum au dhambi Bali ni kwa ajili ya safari ya mbinguni. Hata mke wa lutu alikuwa nguzo ya chumvi kwa kuwa alitaka kuona ni jinsi gani ameokoka na jinsi gani wengine wanaangamia pale sodoma na gomora. yaani ujilinganishe na walio chini ni kosa na huko ndipo Kuna leta dhambi ya kiburi na kujiinua kwa kuwa utajiona upo juu na kwa kweli upo juu ko utaanguka na kuwa nguzo ya chumvi ghafla.

​Kwa habar za Lucifer aliyekuwa malaika mbinguni yeye aliona kuwa ni mkuu kuliko malaika wengine wengi walio chini yake ndo akajona mkubwa akasahau habari ya kuangalia juu ili ajifunze kushuka. na ndiyo maana alishindwa na akatupwa chini sawa na mke wa lutu alivyogeuka kuwa nguzo ya chumvi kwamba aliganda palepale. ndiyo maana hata sisi wakati mwingine tunabaki tulivyo kwa kuwa tumekuwa watu wa kujilinganisha sana na watu tunaowadhani kuwa ni wa chini bila kuangalia je MUNGU anasemaje.

​Njia nyembamba na imesonga kwamba mtu hataruhisiwa hata kugeuka nyumba kuona alipotoka Bali ataangalia anapokwenda tu macho mbele maono. Mbele, fahamu mbele, ROHO mbele imani mbele Kila kitu mbele. Basi jifunze kuona mbele tu maana ukiangalia asili basi ni kwamba asili uliyoipa kuwa asili ikutawale basi hakika itakutawala. asili Yako na maono Yako na matarajio Yako na sehemu ya kujilinganisha iwe ni mbinguni tu Wala sio vya Dunia ujilinganishe navyo maana dunia ni Giza na mbingu ni nuru ko huwezi kujiita mtakatifu kwa kujilinganisha na Giza (watu wa duniani) Bali angalia kwa scan ya mbingu ikuonyeshe udhaifu ili uendelee kufanya upyaa maana Giza linadanganya ila Nuru inaweka wazi.

​Hata nyimbo za kujilinganisha na waovu na wachawi hazifai kwa watumishi wa MUNGU mara oooohh!! Wachawi hawatuwezi, mara ukahaba sijui ma free mason ushoga na siasa na uchafu wote wa dunia visiwe vya kujipimisha MUNGU wako Bali MUNGU yeye mwenyewe ndo akupime. hapo utainuka utakuwa mtu wa juu na mtumishi wa MUNGU kwelikweli na hapo ww ni Nuru kamili ya ulimwengu. Imba, au hubiri kuhusu mambo yaliyo juu si yaliyo chini hapo utawafanya watu wajue wokovu unapimwa na MUNGU mwenyewe Wala sio dhambi Wala sio maisha Wala sio ugumu Wala mambo ya chini ko lazima tujue kuwa mambo ya juu hayapimwi wala kudhihirika kwa mifano ya chini Bali ni juu huko huko tumuachie YESU afanye kazi yake sio tufanye tumpe adhihirishe hapana!! Hiyo haitafaa.

​Wokovu ni wa rohoni basi tuuishi katika namna ya roho hapo tu ndipo itakuwa sahihi.. ufunguo wa imani zetu ufuguke tufungue milango ya rohoni na ishara za kutoka kwa BWANA YESU mwenyewe Wala sio ishara tulizozihalalisha wenyewe ambazo ni za kibinadamu, Bali ishara zetu ziwe za MUNGU hapo tutaonekana kama mbegu ya MUNGU iliyojitenga na iliyotakaswa.

Fellow SOGH Amani Ernest Kyamba.

​Hao manabii wa uongo wanapotosha wengi akati wenye usahihi tupo na sisi tumeshindwa kuithibitisha kweli ya MUNGU kwa kuwa wao wanawafanya watu waangalie na wajilinganishe na ya chini..na sisi tunataka tuende ka ma wao basi YESU hafuati ya chini basi ili adhiririke tumuachie ajidhiririshe mwenyewe yeye aliye wa juu watu wamjue kwa injili ya juu maono ya juu macho ya juu tusimchukue YESU wa juu kumleta chini hiyo haitafaa kabisa na hapo tunamkosea MUNGU.

​Afu pia ni sawa na wewe upande juu sana kwenye mnara Fulani, inakupasa iangalie ulipo na juu tu maana juu hakutakupa kitete lakini ukigeuka kuangalia chini basi lazima kutakuvita udondokee huko. Wakati mwingine BWANA MUNGU anatuzuilia kupanda juu sana kwa kuwa anajua tutaangalia chini ko anguko letu litakuwa kubwa, kwakuwa tupo chini chini na Bado tutaangalia chini, tunawaza yaliyo chini, MUNGU hawezi kutuamini kwa mambo ya juu kama ni hivyo.

​Tunaogopa wachawi, free mason, na shetani baada ya kumuogopa MUNGU, tukiogopa uovu utatuvuta uovu tuwe waovu, tukimuogopa MUNGU basi MUNGU atatuvuta tuwe wake kabisa. Ko hata wokovu wetu ukiwa kwenye misingi ya kuikimbia dhambi na kuogopa maovu lazima tutavutwa na wokovu huo ambao ni wokovu wa Musa kwa kuwa wokovu wa Musa uliwafanya watu waichukie dhambi lakini washindwe kuacha, lakini wokovu wa YESU unatufanya sisi tumtafute MUNGU afu tuikimbie dhambi. roho mtakatifu anaondoa hofu ya mabaya analeta hofu ya MUNGU.

​Afu pia tunajifunza kuwa kwa Nini yakobo alibarikiwa.ni kwa Sababu alifanya vita na MUNGU. lakini adui anapotukamatia ni kwamba anatakatupambane naye?? Ukipambana na aliyeshindwa sio chochote. pambana na MUNGU ambaye ni mshindi wa yote na aliye juu. ushinde uuteke ufalme wa MUNGU maana ufalme wa MUNGU unavamiwa na kutekwa na wenye nguvu Sasa itashangaza sisi eti tunataka tuiteke Dunia na shetani../ je utofauti wetu upo wapi?. ili MUNGU atutumie katika udhihirisho wa tofauti basi ni lazima na sisi tuwe wa tofauti hapo tutamdhihirisha MUNGU maishani mwetu kwa watu wengine.

​Shetani hujigeuza kuwa kama malaika wa Nuru lakini Nuru yake ni Giza Bado ko na sisi tukienda sawa na mitazamo ya manabii wa uongo Ina maana Nuru yetu inakuwa na giza. akati Nuru ya YESU Giza halikuwa na nafasi kwake.. let's look light🕯 🕯 not mixing light with darkness.. this is a word of GOD!!

​Kuokoka sio kuacha mambo yanayoitwa dhambi Bali kuokoka ni kuamua kumfuata MUNGU na kumpendeza MUNGU kupitia haki 1 wakorinto 13:1. kwani pia wapo wanaotenda mema zaidi ya sisi lakini hayajapata kibali Cha kuonekana kwa MUNGU kwa kuwa hawajaokoka Sasa MUNGU mwenye wivu anasema haki yetu isipo zidi haki ya mafarisayo hatitaurithi kwa kuwa upendo wa MUNGU ni wokovu katika njia ya YESU Kristo kwa matendo katika neno na utakatifu hapo ndio haki itakapohesabiwa kwa imani. maana wengine Wana haki ila Hawana imani yenye matendo ko haki Yao haionekani mbele za MUNGU..ko kuwa na haki mbele za MUNGU ni kuwa na uwezo wa kumthibitisha MUNGU mbele za watu. matendo bila usahihi wa imani ni kwamba hayapo ko watu tunapookoka jambo la kwanza ni kuithibitisha imani kama ilivyo kwa kuwa wema na usafi na huruma na kusaidia vyote vikiwa vimefungamanishwa na YESU Kristo mwenyewe,na roho mtakatifu ndani yetu.

​Kuokoka ni kuamua kumpenda na kufanya jambo lolote kama kazi ya MUNGU. kutojionyesha kwa watu bali kujionyesha kwa MUNGU kwa kuwa unaonekana kwake. ukisipo onekana kwa MUNGU Ina maana umejionyesha kwa watu jambo ambalo sio zuri kwa maisha yetu. Kuokoka Ina maana ni kumpenda MUNGU na kujitoa kwa MUNGU kuliko yote Sasa sisi Bado upendo haujatimia yaani kumweka MUNGU mbele kwanza Wala sio miujiza yake Wala Uhuru wake. maana wapo waliomfuata YESU kwa ajili ya mikate YESU hakuwahesabu kuwa ni watu wake. wengine sisi tunamfuata MUNGU kwa ajili ya kuacha pombe,uzinzi,kupona magonjwa,kupata Fulani kitu,YESU hawezi kutuonekania kama ndo yaliyotuleta. lazima Cha kutuleta kiwe ni uzima wake watu waokoke kwa ajili ya kuirithi mbingu na kumwona YESU. maana upendo wa mtu na matendo yanatafuta mema si kwamba yanakimbia mabaya. kwani kuyatafuta mema ni kuyakimbia mabaya.ila kuyakimbia mabaya inaweza ikawa sio kuyatafuta mema.

​Ukijilinganisha na unaowaona ni wa chini Yako ni kwamba tumekubali wewe kuwa juu na ukakubali wale uwaonao kuwa chini wabaki chini hivyo inakupasa kiburi na kujiona wa thamani na kuwachukia walio chini badala ya kuangalia juu ili umpe thamani unayemwendea. kama mke wa lutu angeangalia mbele Ina maana alikuwa anaangalia wokovu wake tu,lakini kuangalia nyuma tu kuona adhabu ilivyo ni kosa kwa kuwa huo ni upande wa MUNGU mwenyewe Wala sio mwanadamu. si haki yako kuwahukumu wengine kwa kujilinganisha nao ila kazi Yako ni kumulika hao wageuke ..amen!!

​Huu pia ni ujumbe mzuri sana kwa wahubiri wa injili ili kwamba injili inapotamkwa/kuhubiri injili iwajenge watu kuona ya juu tu Wala sio ya Dunia kwa kuwa ukimtumikia MUNGU kwanza hayo mengine tutazidishiwa..basi injili ilenge mambo ya ufalme tu afu ayo mengine ni ziada tu. ni zawadi ya MUNGU hiyo.. Wokovu ni asili ya kuokoka roho za watu..ila ziada ya wokovu ni faida kwa mwili basi watu waokoke wakitegemea mambo ya mbinguni tu..kwanza ..wasije kuwa wanaokoka wanataka Mali, uponyaji wa magonjwa, uzima,na faida za mwili hiyo ni kinyume na Sheria za wokovu kwamba lengo kuu liwe mambo ya rohoni kwanza mathayo 6:33.

​Blessed you all in the name of Jesus Christ amen!!

A.E.kyamba from SOGH team.


Comments

Popular posts from this blog

Kuweza kulitendea kazi neno la MUNGU

Mwamuzi(short notes)

Je kwa nini namna ile?