Msamaha wa kweli


MSAMAHA WA KWELI NI UPI?

​4/02/2026

This is a SOGH 

Amani Ernest kyamba


​#Nikizungumzia msamaha ni jambo ambalo Kila mmoja analifahamu kwa namna moja ama nyingine. basi najua Kila mtu ni mtu wa kusamehe, lakini je una msamaha wa kweli?. Kama husamehi hutasamehewa na MUNGU. asiyesamehe amelaaniwa na hukumu haitamwacha.

​#Mathayo 6:12-15 msamaha wa MUNGU unathibitishwa kwanza na msamaha tunaowasamehe wengine. #Luka 6:38 kwa kuwa tupimavyo ndivyo itakavyopasa kupimiwa. ko tunatubu sana mbele za MUNGU lakini wakati mwingi haiitwi toba ya kweli kwa kuwa hata sisi hatuna msamaha wa kweli kwenye maisha yetu. kama tuna msamaha wa manung'uniko basi hata MUNGU atatusamehe vivyohivyo. kama tuna msamaha wa kusamehe afu kupoteza imani na mtu huyo aliyetukosea ni kwamba hata sisi tunapoteza imani kwa MUNGU wetu wa mbinguni ko hatutakuwa wa ajabu, kwa kuwa hatustahili kusamehewa.

​Je? Msamaha wa kweli ni upi? Anaouhitaji MUNGU? Ngoja tukumbushane. #this is a SOGH Amani Ernest Kyamba.

​#jana nilikuwa naongea na kaka mkuu kuhusu mambo Fulani mazuri mengi, nikajifunza mambo mengi kuhusu msamaha wa kweli. #kutendewa kosa ni kama kuumizwa kidonda kikubwa mno. #wanadamu wengi tuna maana Moja ya kusamehe kwamba tumesamehe ila hatuwezi kusahau.

​##kabla ya yote nachozungumzia sio msamaha wa mataifa, nazungumzia msamaha halisi wa mtu aliyeokoka. kwamba yeye msamaha wake inabidi uwaje?. #ni msamaha wa kiroho, ni msamaha wa muujiza, ni msamaha usiopimika, ni msamaha wa ajabu mno.

​#kwanza kabisa tujifunze kuhusu msamaha wa wanadamu waliopewa wanadamu. naufananisha na kidonda, mtu ameumia, akiwa ameumia anatarajia kupona, kidonda kikiwa kidogo mara nyingi katika mwili hata kovu huwa linapotea. #lakini kidonda kikiwa kikubwa asilimia kubwa kovu linabaki maisha yote japo limepona.

​#kwa maisha ya kawaida ukienda jeshini au kwenye vyombo vya usalama hutaruhusiwa kuingia kama unakovu kubwa. kwa kuwa jeshini shughuli kama kushinda kwenye maji na kwenye tope na Hali ngumu zinaweza kuelekea kovu lirejee kutoa maumivu na kuwa kidonda kikubwa vilevile. #ko ukiwa umesamehe alafu ukapona ukaacha kovu ni kwamba unaacha uwezekano wa jambo Hilo gumu kurejea Tena kukudhuru.

​#ko wakati mwingi tunalalamika kwamba mbona Mimi mambo ya makwazo yapo kwangu hivi. ni wengi wanalalamika lakini suala ni Moja kwamba maadamu upo kwenye maji (watu wanaokuzunguka) kile kidonda lazima kibaki kidonda hivyo. ko utajikuta una mfululizo wa mambo ya kukwaza mno Kila siku kwa kuwa msamaha wako si wa kweli. #huo ni msamaha wa kimwili, ni msamaha wa Sheria, ni msamaha wa duniani kwa mataifa, ni msamaha wa laana ndo maana unafanya maisha Yako yawe tabu kila siku haijalishi umesamehe watu wangapi. kwa kuwa ni msamaha wa mataifa huo.

​##this is a SOGH Amani Ernest Kyamba. #je msamaha wa mtu aliyeokoka ni upi (msamaha wa kweli?). #tusome 2 falme 5:1-15.

​Naamani alikuwa ni jemedari wa jeshi la shamu na alikuwa na shida ya ukoma (msamaha). kwa kuwa ukoma ulikuwa ni ugonjwa mkubwa sana kipindi kile ulitegemewa kufanya madhara makubwa kwa naamani kwenye mwili wake kwani ukoma ni ugonjwa unakula vidole, mikono, na VIUNGO. Kwa kupona kwake ni kwamba angekatwa sehemu zilizoathirika kwa ukoma ili abaki safi ila abaki kilema.

​#hiyo ilikuwa ni njia ya kimwili ya kibinadamu ya kuutibi ugonjwa wa ukoma. je?? Njia ya MUNGU ni ipi. bila shaka unaifahamu. #alipoenda kwa MUNGU (alipookoka) njia ilibadilika. Alienda kutumbukia kwenye mto mchafu ili awe safi. #hata naamani akashangaa anauliza je abana na farpari halikuwa mito mizuri kule shamu, si Bora angeniambia niende huko. au si angenishika na kuniponya Moja kwa Moja ili niwe safi?.

​Kwa Nini kutumbukia kwenye limto lichafu kama jordani (sasa ni kama mto chota mvua za kwanza zilee). #kwa Nini MUNGU alimwambia Elisha kwamba ili naamani asafishike aingie kwenye maji machafu na sio masafi?. maji machafu (ni watu wanaokuzunguka wanaokukwaza Kila siku). lazima ukae nao hapo ndipo utakuwa safi.

​#ko msamaha wa matendo ni msamaha wa kimungu zaidi. kwamba ili uwe safi pasipo kuwa na kovu lolote gharama ni Moja, tu ukae na hao watu waliokusababishia donda kwenye maisha Yako uzame na uogelee humohumo usiwakimbie. kama naamani alikuwa mchafu akazama kwenye mto mchafu akaogelea humo mara saba haijalishi alichelewa kuwa safi hakukata tamaa mpaka alipotoka safi kabisa. #maana uchafu wa maji utauvuta uchafu na udhaifu wako. la!! Angeenda kwenye mto msafi yakini ukoma wake ungeongezeka mara!!. #Kwa kuwa maji masafi yangechukua nafasi safi ya mwili wa naamani ko naamani angekuwa na ukoma mwili mzima endapo angeenda farpari na abana.

​#huo ndio msamaha wa kweli kwa mtu aliyeokoka ni kukaa pahali palepale. mtu akikukwaza na kukuudhi wewe ndo mpende mara zaidi na kumjali kwa namna hiyo utakuwa na nafasi ya kuilinda nafsi ya mtu huyo isipotee. usikubali kupona peke Yako taka na aliyekukwaza apone maana ole IPO kwa akwazaye na anayekwaza. ko usijitoe kwenye ole peke yako. make sure na mwenzako akukwazaye anatoka kwenye hiyo ole. Luka 17:1.

​#ko msamaha wa kweli unakuwa si wa moyoni tu, bali unakuwa wa matendo. #MUNGU wetu alipotusamehe kwa dhambi na makosa yetu (maana yeye ndiye aliye wa kwanza kutusamehe kweli) kwa kutusamehe akatupenda!!. (Ko ukiona unasamehe afu unabaki na chuki na kinyongo sio msamaha huo) . akamtoa mwanaye wa pekee YESU Kristo aje atukomboe.

​#msamaha usio wa kweli unaanza na utaishia na majuto na huzuni. MUNGU aliwasamehe wanadamu kwa kuwaangamiza kwa maji kipindi Cha nuhu ni kwa Sababu alianza na majuto mwanzo 6:6:7. #Alihuzunika na akaweka agano jipya la msamaha wa kweli kwamba Sasa hatampiga Tena mwanadamu kwa mapigo Yale, maadamu Kuna njia ya kubadilisha MTU. hatampiga. akaanza kuandaa njia ya kuwabadilisha wanadamu ambayo ni YESU Kristo, mara tu baada ya gharika.

​#wengine watajiuliza mbona sodoma na gomora walipigwa?. Ni kwa kuwa wao walikuwa hawana namna ya hiyari ya kuwabadilisha kwa kuwa maovu Yao yalifika Hadi juu mbinguni. akawafuta wasiwepo juu ya nchi, akawasahau kabisa.

​#MUNGU wetu anapenda hiyari yaani tunamtumikia kwa moyo wa kupenda kabisa kwa kuwa yeye ni pendo. hataki lazima anataka upendo kwa kuwa yeye ni pendo na Tena ndiye msamaha wa kweli. #ko upendo unaambatana na upatanishi mathayo 5:9. MUNGU alitupenda afu akatupatanisha upatanisho wa milele wa hiyari kupitia mwanaye mwokozi wetu, Emanuel yaani YESU Kristo.

​#ko angalia msamaha wako kwamba je unalenga upatanisho au unalenga uharibifu. be careful msamaha ndio msingi wa toba ya kweli. #neno la mwisho mithali 16:7, MUNGU (wokovu), matendo matakatifu MUNGU atakupa kibali Cha kupatana na wanaoitwa adui au waletao makwazo. kama YESU alivyowaokoa na kuwaponya watoza ushuru na mafarisayo na waovu ambao walifanyika adui za MUNGU na YESU. akawafanya rafiki kwa kuwa alikuwa msafi.

​Utakatifu wako utapatanisha maisha Yako. wenye rehema watapata rehema. kama si mtendaji wa neno huwezi kuwa na msamaha wa kweli. sikiliza na neno la MUNGU. na andiko linaitwa neno pale ukiwa na ROHO MTAKATIFU.

Mungu akubariki sana mtumishi wake wewe.Roho mtakatifu akusaidie ili ufike viwango vya juu zaidi vya msamaha kupitia somo hili.

Amen

​#Tutaendelea kujifunza kwa habari hiyo ya ROHO MTAKATIFU. amen. Blessed you all. # SOGH team. #let's do GOD'S work together. #this is a SOGH # Amani Ernest Kyamba # Kyamba.E.A. 

Comments

Popular posts from this blog

A.Kuweza kulitendea kazi neno la MUNGU

Je kwa nini namna ile?

Mwamuzi(short notes)