Msingi imara(short notes)


​1. Kanisa na Msingi Imara

07 Jun 2024

Kanisa na msingi imara.

​Hakuna nyumba inayojengwa pasipo msingi. uimara wa msingi ndio unaoamua uwezo wa nyumba kuhimili mabadiliko ya Hali ya hewa. ina maana kama kanisa linachezewa na shetani Ina maana kuwa kanisa halina msingi imara. makanisa mengi ya Sasa hayana msingi imara wa wokovu, yaani watu Wana sali lakini Wana hila mioyoni mwao, yaani kwaya zina ugomvi, na watu Wana maneno na hila wao kwa wao, watu wengini ni wasengenyaji uwepo wa dhambi katika kanisa unamuondoa MUNGU asiwepo kwenye kanisa Hilo na ndio maana ibada inapoa na watu wanabaki vile vile siku zote kwa Sababu mtu asiye na MUNGU anafananishwana jiwe ndani ya maji linalokaa kwenye maji ila haliruhusu maji kuingia ndani, yaani mwenye dhambi hawezi kumwona MUNGU hata siku Moja mpaka MUNGU atakapogeuza moyo wa mtu huyo uwe wa nyama. uwepo wa dhambi na kukosa utii wa neno la MUNGU kwa watu unaondoa uwepo wa MUNGU kwenye kanisa.

#yoshua 7:1. israeli ni mfano wa kanisa kama Leo hivi tulivyo. kwa Nini dhambi ya akani iliwafanya Israel wote washindwe vita mbele za mji mdogo wa ai? ni kwa Sababu dhambi ya akani ilihusisha vitu vilivyowekwe wakfu, katika nyumba ya BWANA, nyumba ya bwana kwa Sasa wokovu ndio unaotutenga na kutufanya wakfu kwa MUNGU. tunapoichezea neema ya wokovu ambayo tumepewa na MUNGU. ina maana hatuna msingi imara wa kumshinda mwovu. na hapo kanisa halitaweza kufanikiwa kwa Sababu litaonekana kuwa halina utakatifu. akani alikuwa mwisraeli(yaani aliyeokoka) lakini hakutii agano la MUNGU la kuheshimu madhabahu yake. ina maana alikosa utii.

​*ko basi msingi mkuu wa kanisa ni kulisikia na kukubali kulitendea kazi neno la MUNGU wa mbinguni kwa shauku kupitia ROHO MTAKATIFU. mathayo 7:24.

​Amen!!

By Amani Ernest kyamba from SOGH team.

Comments

Popular posts from this blog

Kuweza kulitendea kazi neno la MUNGU

Mwamuzi(short notes)

Je kwa nini namna ile?