Ole
05 Feb 2025
Ole kwetu sisi watumishi wa MUNGU
nilikutana na watu wabaya wenye utisho porini na yote ni kwa kuwa kwanza nilipanda gari binafsi (nilijitenga na wenzangu waliokuwa kwenye basi mithali 18:1) na wakati huo nilikuwa na begi la thamani mno ambalo ni neno la MUNGU.
Njiani porini nikashangaa begi limedondoka lenyewe kwanza kwa kuwa halikunistahili Mimi kushuka tu kumbe wale wa gari binafsi walikuwa dili moja na wale watu wa porini wanaotisha ambao walibeba visu, na vifaa vikali ili wanitishe.
Begi Lile sikuliona Wala chochote sikuliona nilipoteza neno ila ujuzi wa kupika sikupoteza basi shetani anahitaji ujuzi wangu wa kupika ko akaniambia nikapike chakula (junk) kinachoangamiza na kinachovutia. mimi nikajitambulisha kuwa Mimi ni mtumishi wa MUNGU wakasema kuwa hata wao Wana MUNGU wao, Mimi nikasema ni MUNGU wa mbinguni wakasema hata wao ni hivyohivyo..
Kumbe shetani anaweza akajigeuza kuwa malaika wa nuru ili kukupata wewe ambaye unajua neno la MUNGU kiundani (2 korinto 11:14). shetani anajua jinsi ya kutumia neno na pia anajua udhaifu wako. sasa walijua Mimi ni mpishi ko wakanitengenezea mazingira ya kupika kwao japo sikuwa na neno la MUNGU..
Sasa hapo ndipo nilipoona kuwa unaweza ukawa unahubiri na kuitwa mtumishi lakini unampikia shetani chakula kwa watu wake waone ni chakula kizuri kumbe ni sumu. ndivyo watumishi wengi wanavyofanya, wanahubiri maneno ya shetani badala ya MUNGU.
Nikaona kuwa mazingira ya sasa yamekaa kimitambo zaidi (system) kiasi kwamba hata kama unajijua kuwa wewe ni mtakatifu basi lazima uwe makini na kile unachofanya na pia marafiki unaoambatana nao.
Mwisho nikaona jinsi ambavyo MUNGU anatuonya sisi watumishi wake kuwa tuache michezo na tuwe makini na nyakati hizi tunazoishi. ni heri tuwe moto au baridi kuliko kuwa vuguvugu. eti tunapika chakula Cha MUNGU afu tumboni tuna Cha shetani huo ni mzaha na michanganyo.
Ukiwa vuguvugu adui atakuchezea na Hali Yako ya mwisho itakuwa mbaya zaidi kuliko ya kwanza na utaishi kwa aibu utakufa kwa aibu Luka 11:25-26.
Nini ninataka kusema ni kwamba ukiamua kuwa moto uwe moto (kwa MUNGU), ukiamua kuwa baridi uwe baridi (shetani) kwani ukiwa vuguvugu MUNGU atakutapika ufunuo 3:16 na shetani atakugaragaza na kukupoteza kwa namna mbaya zaidi ko ni heri kwa huduma unayofanya na jinsi umeokoka ili upate ushindi wa mbinguni lazima iamue kuwa mtakatifu kwelikweli hapo mwovu hatakugusa hata kidogo na atakukimbia ukimpinga Yakobo 4:7.
Ukiwa vuguvugu ukimpinga anakufuata kwa kuwa unakuwa umetapikwa na MUNGU na ni kwamba haulindwi na MUNGU. atakugaragaza mwovu. amua ndugu yangu, tuamue na tumtumikie MUNGU wa mbinguni kweli kweli tuwe washindi kweli kweli.
Kwa Nini uanze katika ROHO ukamilishwe katika mwili wagalatia 2:1? Amua sasa!!
A.E.KYAMBA.
Comments
Post a Comment