Part 01:KIVULI CHA YAJAYO

 My name:Amani Ernest Kyamba 

SOGH Team 

Let's do GOD'S work together 

Kwenye Lile somo lililopita la "KWA NINI UMEOKOKA" tulizungumzia watu waliopambana na ya chini wakashindwa basi nilibakisha mfano mmoja wa mtu aliyeshindana na Nuru akaishinda yakobo alipambana na MUNGU wa mbinguni aliposhinda akapata baraka kubwa kuliko wote duniani.mshinde MUNGU uteke ufalme wake maana ufalme wa MUNGU unapatikana kwa nguvu na kuuteka.

Na siyo kuwa na lengo la kushindana na ulimwengu.maana YESU alishinda ulimwengu sio kwa kushindana nao Bali kwa kutoa mfano wa kujitoa kikamilifu mbele za MUNGU.ndipo akaishinda.


part 01:

PALIPO NA UDHAIFU PANA NGUVU


Lengo la haya masomo ni kuwafumbua  wakristo waanze kuona mambo ya rohoni kujua walipotoka walipo na wanapokwenda..maana watu wengine wanasema wametoka mbali huku kumbe walipo ndo waliipotoka hapo walipo ukiwa hivyo basi maana yake mtu unakuwa kipofu yaani usiyeona chochote.YESU.kristo anataka tuone, kwamba macho yafumbuke tujue tulipo kwani tusipojua tulipo ni kwamba tupo nuruni sawa, maana asili tuliyo nayo ni ya. Nuru(tumeokoka).lakini macho(fahamu za utambuzi wa rohoni) zimetiwa Giza, basi tunakuwa tupo nuruni ila hatuoni Nuru ko ni Giza pia la shetani..basi YESU yupo hapa kutufungua macho.


 Yohana 9:39-41;YESU akawaambia mafarisayo kwa kuwa alikuja ulimwenguni kuwafanya wasioona waone na wanaoona wasione.watu Gani wanaoona alafu wasione?!,ni wale ambao wapo kwenye Sheria ya MUNGU na Wana uhakika alafu hawaifuati yeye YESU alikuja kuwathibitisha kwamba hawapo sahihi,yaani wanaijua Nuru alafu wakapenda Giza kuliko Nuru, hao atawafumba macho wasiione nuru.maana wameiona Nuru wanaijua ila kwa Sababu zao wakalichagua giza.mpaka waamue kuwa vipofu kwa kuhitaji msaada upya wa YESU ili YESU awafanye waone Nuru wawe wanaona nuruni.ndo maana akawaambia mafarisayo kwa kuwa mwasema mwaona basi dhambi yenu inakaa kwa kuwa mnajua mlipo na kwa makusudi mnaipinga kweli kwa faida ya maisha yenu ya mwilini.


    sisi tupo nuruni ila ni vipofu yeye YESU anataka atufanye tuone Sasa kupitia neno lake.



Kabla ya yote tusone yohana 3:1-8.

Kuokoka kupo kwa aina mbili. na ni lazima uokoke mara ya pili katika ROHO MTAKATIFU hapo itakuwa sawa vizuri kabisa.

Ukiokoka kwa Sheria yaani kwa kumkiri YESU Kristo pekee, Ina maana umekubali kufanyika mteule wa MUNGU kama Wana wa Israel basi mema Yako na mabaya Yako yanakuwa yanajionyesha wazi mbele za MUNGU.yaani umeingia kwenye mfumo wa MUNGU ko unakuwa kama Wana wa Israel walivyokuwa mbele za MUNGU.huu wokovu unakamilishwa katika udhaifu,ni katika kujikana na kujitoa kikamilifu mbele za MUNGU wa mbinguni.na kujitahidi kuomba na kutaka kutakaswa kujifunza neno na kukamilishwa na kuitwa mtu wa MUNGU.ukishaokoka tu kwa kumkiri YESU, ROHO wa MUNGU anashuka ndani yako,lakini huyo ROHO ashukapo atakuwa anakukagua udhaifu wako/kwa kuwa ROHO ni mkaguzi ili akujue na udhaifu.na atakujua pale unapojikana na kujiweka wakfu kwa MUNGU kwa akili,moyo,Mali,fahamu,na vyote ulivyonavyo.akishaona mahali unashindwa na unatamani kushinda basi anaanza kukusaidia ili udhaifu wako ujae nguvu hatimaye uitwe una nguvu ya kushinda.akikusaidia ROHO Ina maana anakuongoza kushinda na hapo ndipo utaitwa _"mwana"!!_.ili uwe mwana lazima tujifunze kabla ya kuwa mwana unakuwa unaitwa mwanafunzi,afu,muumini(aliye amini),afu mfuasi(anayejua ila ajaamini yaani matendo yake hayaendani).


Sasa inashangaza muumini anakuwa hataki kukaguliwa udhaifu kwa pale anavyojitoa na kutaka kukamilishwa kwa jinsi anavyolitendea kazi neno la MUNGU.kwa kuwa mwanafunzi anapimwa kwa mtihani Sasa akiwa anafundishwa afu anafeli mtihani Ina maana Bado hafai kuitwa mwanafunzi.

Ukizaliwa katika ROHO inamaana umezaliwa na MUNGU hautatenda dhambi 1 yohana 3:9,1 yohana 5:18,1 yohana 3:6.Ina maana Sheria imekutambulishia dhambi alafu huitendi dhambi ko unakuwa juu ya Sheria maana asili ya Sheria ni kuvunjwa ukitenda dhambi unakuwa chini ya Sheria maana Sheria ndio inayokuhukumu.ila ukiwa hautendi dhambi hutahukumiwa na Sheria utahukumiwa na YESU mwenyewe kwa kuwa upo kwenye neema na YESU ndiye baba wa neema.mimi namshukuru MUNGU kwa neema hii kwani amenishuhudia hakika kwamba nimekuwa mwana kwani sio mtumwa wa neno(halinifungi halininyimi,halinifanyi nijihisi sipo sawa,sichukii kuyafuata maagizo yake) Sasa nimewekwa huru kupitia neno...haya ni kutokana  na somo la baba pastor kuhusu hatua za kufanyika mtu wa Yaani kuwa huru mbali na dhambi inamaana ni kuondoa upinzani wa asili ambao unatusumbua kwa asili kutokana na sheria.hali inayotupinga warumi 7:6.tunakuwa huru nayo kwa kupitia ROHO kwani hatutajikaza na kuutiisha mwili kwa ukali ili kuishinda dhambi kwa kuwa tayari tutakuwa tumeshinda kabisa.


Udhaifu ni nini basi? Udhaifu ni mfano wa utupu uliopo kwenye kifaa cha kubebea vitu.mfano tanki likiwa halina maji linakuwa na utupu.

          Wapo watu wengine hawana udhaifu(hawana cha kubeba) (wanaishi kwenye neema ya wanadamu kabla ya gharika). Wanafanya linalofanyika,na Wanaona wana haki ya kufanya wanayoyafanya

       Wapo wengine Wana udhaifu mkubwa sana(mfano wa tanki kubwa la maji ambalo halina maji.hawa wakiamua kutafuta nguvu watajaa nguvu kubwa sana.

Wapo wengine wana udhaifu mdogo(vifaa vyao vya kubebea ni kama ndoo na sio tanki) watavuna walicho kipanda kwani MUNGU hadhihakiwi na apandacho mtu ndicho atakachovuna.wengi sana kati yetu tunakuwepo hapa.afu tunalaumu kuwa saivi wokovu umepoa wakati huo wenye makosa ni sisi wenyewe.

       



        Siku zote MUNGU wa mbinguni anatumia viumbe dhaifu ili aviaibishe vinavyojidhani kuwa vina nguvu.1 korinto 1:27. Kwa kuwa ili MUNGU ajitukuze kupitia hivyo lazima pawe na udhaifu kwa kuwa MUNGU anajitukuza katika udhaifu na anajithibitisha katika nguvu.

Ndo maana kipindi Cha gideoni alitaka jeshi la Israel liwe dhaifu ili ajitwalie utukufu yeye mwenyewe.wasiwe watu wa kujitwalia utukufu.huyo ndiye MUNGU wa mbinguni.

#kwa kawaida watu wajidhaniao kuwa na nguvu hawampi MUNGU utukufu Bali hujipa wenyewe.hawamruhusu MUNGU atukuke kwa kuwa tayari Wana nguvu wamejijaza na ni akili zao na ujuzi uliyowasaidia.

      kwa Nini YESU alishuka katika mwili? Kwa kuwa ili awapate walio dhaifu(wanadamu) walioshindwa na dhambi alitwaa udhaifu wetu akawa nao na yeye kwa kuvaa mwili ulioshindwa mathayo 8:17, ili katika udhaifu alioutwaa atupe nguvu na uwezo wa  kuushinda udhaifu.na hatimaye kuleta utukufu kwa MUNGU wa mbinguni.

#Ohoooo hapo tunajifunza kuwa ili tuwe na nguvu na kumpa MUNGU utukufu lazima kuwe na udhaifu.

udhaifu ndio uliomtukuza YESU Kristo akaenda akaketi mkono wa kiume wa MUNGU, kwa kuwa ukimtukuza MUNGU basi na yeye atakutukuza wewe.yohana 13:31.

     Udhaifu ni Nini basi? Udhaifu ni kiu ya kuhitaji msaada kutoka kwa MUNGU.udhaifu ni uhitaji,ni kukiri kushindwa na kuuhitaji msaada wa MUNGU.

   udhaifu ni umasikini wa roho mathayo 5:3.ni uhitaji wa kumwona MUNGU.

Warumi 8:26 hakuna ROHO MTAKATIFU pasipo udhaifu.

       Ko kazi ya roho ni kutusaidia katika udhaifu wetu kwamba tuushinde.sasa watu wanatamani roho mtakatifu lakini hawana udhaifu ili ROHO mtakatifu aje awasaidie.kama ambavyo Huwa nasema kwamba msaidizi hatakuja kwako kama hujaitaji msaada.ko hapo tunajifunza kuwa mara nyingi tunamzuia ROHO MTAKATIFU asifanye kazi ndani yetu kwa kuwa tunataka  kushughulika na madhaifu yetu wenyewe.hapo ROHO wa MUNGU huondoka.kwa kuwa hatuhitaji msaada.


Je sisi tuna udhaifu?????.

Tusonge mbele!!.



KWA KUANZA NA TOFAUTI KATI YA AGANO JIPYA LA WOKOVU NA TORATI YA MUSA.

Kabla ya wokovu kuwepo/YESU kushuka duniani torati ilikuwa ni kiongozi kwa watu wa MUNGU kumwona MUNGU.torati ni sheria.wanadamu waliongozwa na Sheria ili kumwona MUNGU kama vile nchi zetu zinavyoongozwa na katiba ya nchi ili kuongoza amani ya watu.lakini torati ilikuwa na udhaifu ambao ndio ulipelekea neema ya kweli ishuke kupitia YESU Kristo.ko udhaifu wa torati katika kuwafanya watu wamwone MUNGU ndo ulipelekea utimilifu na nguvu ya neema.

#ko kushindwa kwa torati ndo kulisababisha kuja kwa neema..maana torati ni katiba ya wanadamu kutoka kwa MUNGU kwa kuwa utendaji na utimizaji wa torati ulikuwa ni wa mwilini zaidi,torati ni ya rohoni ila ilibidi itimizwe katika mwili.lakini neema ni ya rohoni na utimizaji wa neema inabidi uwe wa rohoni zaidi.

#ufalme wa MUNGU(wokovu) utashuka kwetu pale tu kwanza tukikubali udhaifu na kuhitaji msaada.udhaifu ni Sheria ya torati.ko kamwe hatutastahili agano la wokovu kama hatujakubali kufuata Sheria ya MUNGU kwanza na kushindwa...(Tunajifunza zaidi)


Luka 17:20-21.

Tunaona kuwa ufalme wa MUNGU ulikuwa katika Israel kwanza kutokana na uwepo wa torati(Sheria). ufalme inamaanisha utawala ko inamaanisha kwamba ukianza kujitahidi kuzifuata Sheria za MUNGU Kuna dalili kwamba unatawaliwa na MUNGU.ko inamaanisha kwamba lazima tuzifuate Sheria za MUNGU kwanza hapo ndipo ufalme(utawala) wa MUNGU utakuwa kwetu.

        Mathayo 21:43; lakini YESU anakuja kusema Tena kwamba ufalme wa MUNGU utaondolewa kwenu kwa kuwa hamzai matunda ya kifalme na watapewa watu wengine..hii ni ole!!.(Tutaendelea zaidi)

          #ko hapo tunakuja kujifunza kuwa Sheria ndiyo inayoshusha ufalme wa mbinguni rohoni mwetu lakini neema ndiyo inayosababisha ufalme wa MUNGU kuzama matunda maishani mwetu. Ko tunaona kidogo kuwa kwa Nini biblia Ina maagano yote mawili japo moja ni kuukuu lakini yote yapo kwa kuwa yote Bado yanafanya kazi katika wokovu wetu.na MUNGU anayatumia yote katika kutufanya sisi kuwa watumishi wake.

Turudi nyuma kidogo. Luka 8:18;Ili upate wokovu lazima uwe na Sheria kwanza.la sivyo wokovu haukustahili.

#kwa kuwa utimilifu wa wokovu inaundwa katika udhaifu wa Sheria,yaani hakuna neema pasipo Sheria ndo maana adamu na Hawa walipewa neema alafu na Sheria kwani Sheria Ile ndo iliyopim 

a uaminifu wao kwa MUNGU....


JE NAMNA GANI SHERIA INALETA UDHAIFU NA NEEMA INALETA NGUVU?.

       Mwanadamu wa kwanza aliumbwa katika Hali ya nguvu na ushindi tu(wema) maana udhaifu ni uovu.

Kujua wema ni nguvu lakini kujua mema na mabaya kunakotokana na mpango wa MUNGU ni nguvu,na kujua mema na mabaya kunakotokana na ushawishi wa mwovu ni udhaifu.

#sisi ni dhaifu kwa kuwa ni ushawishi wa shetani kulipinga neno la MUNGU ndio uliotufanya sisi kuwa hivi Leo tulivyo.kwa kuwa shetani ana madhabahu ya uovu basi mwanadamu akajiungamanisha na shetani kwa kutolitii na kumuasi MUNGU.na ndo maana uovu ukawa unamaamuzi zaidi kuliko wema katika mwili.

basi mwili ukawa una asili ya kuyapinga mambo ya MUNGU.

        kwa kuwa wanadamu wakawa tayari dhaifu kama Dunia ya kipindi Cha nuhu jinsi ilivyokuwa mbaya,ya sodoma na Gomora nayo ikawa mbaya..kwa kuwa asili ya mwanadamu ilifanana na ya shetani.

Ko ikawa ili MUNGU aanze kuwapata watu akaanza na jamii ndogo ya watu(Wana wa Israel) kama alivyoanza na watu wawili wa Dunia kuijaza Dunia basi alianza mpango wa wokovu kupitia watu wachache na neema ya MUNGU ikawajia Wana wa Israel.

#jambo la kwanza kabisa ni kumfanya mwanadamu atambue udhaifu wake kupitia sheria.kwa kuwa Sheria ndiyo inayotambulisha dhambi.warumi 7:7. Na kwa kuwa mwanzo kwa kuwa mwanadamu hakujua udhaifu wake basi aliyafanya mambo maovu kama mema kwake.alijitia Haki katika uovu na akaona udhaifu wake ni nguvu jambo ambalo silo.

#Dhambi ilijulikana ila haikutambulikana kama dhambi kwa watu ko torati ilikuja kuunda udhaifu ili katika huo wanadamu wapate nguvu.

#Kupitia torati mwanadamu akajua kuwa Kuna MUNGU.kama Israel walivyojua kuhusu MUNGU.walipojaribu kumtii na kumfuata MUNGU wakashindwa kwa kuwa nguvu ya dhambi iliwatawala kwa kuwa walimsikiliza shetani mwanzoni..basi Israel wakatambua jinsi gani ilivyo kumtafuta MUNGU wa mbinguni.kutambua ugumu huo ndiko kulikounda uhitaji wa kumtafuta MUNGU.yaani ukijitoa sadaka mwili wako kwa kujikana kwa namna ya Sheria kumfuata MUNGU basi unastahili kupokea neema ambayo ndiyo nguvu ko unaurudia ukamilifu.matendo 1:8.

Ko kumbe KUUTAMBUA udhaifu kwa vitendo ndiyo nafasi inayotupa sisi nguvu ya vitendo ambayo ndiyo roho mtakatifu.

#je sisi tuna nguvu ya kushinda?

Conclusion:tunaweza tukawa hatuna nguvu ya kushinda kwa kuwa hatujafuata taratibu za MUNGU wetu mwenyewe za kujikana kwanza ndipo kumfuata kwa kuwa kuokoka kwanza ni Sheria ila kuuishi wokovu ni neema na nguvu inahitajika.

Warumi 10:9 kumkiri YESU Kristo na kuamini ni Sheria uitwe umeokoka kwanza lakini kwa mda ukishaokoka tu basi ni lazima ujikane katika kuishi Sheria ya MUNGU ambayo ni neno lake  ambalo linasisitiza  kuomba,kutenda mema,kutolipa ubaya kwa ubaya,kuwasamehe wengine,kuwa watu wa toba,kuombea wengine,kutafakari neno la MUNGU,kusaidia masikini na wasiojiweza na mengi ambayo yameandikwa katika agano la wokovu.ni lazima yatimilizwe kama Sheria kwa maandalio ya moyo ambayo ni ya mwanadamu huku tukilisubiria jawabu la MUNGU kwetu ambalo ni kuitwa watakatifu na yeye na kutakaswa..lakini Sheria ya kwanza ni kujitahidi sisi wenyewe katika kumtafuta MUNGU ambaye ndiye nguvu maana kwa hivyo tunakuwa tunaashiria kuwa sisi tumeshindwa ndo maana tunahitaji nguvu.

      Sisi hatuna nguvu kwa kuwa hatujakiri udhaifu ko nguvu haitustahili.kwa kuwa tumejipa nguvu wenyewe ko nguvu ya MUNGU iliyo halisi tunaikosa.basi ni lazima tuamue kumtafuta MUNGU kwa bidii kwa Kila Hali kwa kujikana na kutoa miili yetu(udhaifu) wetu kuwa dhabihu ili MUNGU atupe nguvu ya kushinda na zaidi ya kushinda.

#tulikuwa wa dhambi mambo ya MUNGU yalikuwa upuuzi kwetu tulipookoka yakawa na maana..yalikuwa na maana kwa kuwa tuliunda hamu ya kuyavuna mambo ya rohoni.

#maana kupitia mafundisho ya wokovu timeujua udhaifu wetu basi maamuzi ya kuipata nguvu yanahitaji kujikana na kujitenga  mbali na uovu...huku neema ikidhihirishwa kwa kuwa tuna roho mtakatifu wa kututetea na tuna namna ya kujaza nguvu siku baada ya siku kwa kuwa watu wa maombi kwa bidii kumuomba MUNGU huku tukiongozwa na ROHO.hapo ni kwamba tayari tutakuwa tumeshapata nguvu.neno linafunua madhaifu roho  anajaza nguvu tunajaa na tunakamilika. 

        Kupenda nguvu ndo msingi Wa kuushinda udhaifu. Basi angalia Nuru ya MUNGU juu ili ikumulike utambue udhaifu uushinde Wala utakatifu wako usiupate kwa kujilinganisha na wanadamu bali kwa kuupata kupitia MUNGU wa mbinguni kwa haki kwa njia ya imani.


............HAPO SAWA........ MUNGU alibariki neno lake amen.


Hili somo ni utambulisho wa msingi wa wokovu wetu.kutakuwa na somo part 02 ya KIVULI CHA YAJAYO.

ambalo ndio litakamilisha somo hili kabisa. Tumuombe MUNGU atupe kibali tujifunze na sehemu hiyo ya pili.usiwaze kama umehisi mkanganyiko.ninajiandaa vizuri kwa ajili ya somo la part 02.

MUNGU akubariki kwa sababu umevumilia kusoma somo hili refu sana pamoja na kwamba una mb(data bundle) na ungeweza kufanya chochote kwenye simu.

Ni hatua njema sana na hakika utapata baraka kutoka kwa BWANA kwa hicho kitendo


Amen!!



 Teacher:Amani Ernest kyamba

 from SOGH TEAM

Let's do GOD'S work together....

































Comments

Popular posts from this blog

A.Kuweza kulitendea kazi neno la MUNGU

Je kwa nini namna ile?

Mwamuzi(short notes)