SOGH Team: nani unayemuangalia?
Tunajenga nia kwa ajili ya nani?
SOGH Team
Amani Ernest Kyamba.
Let's do GOD'S work together.
Note: Hili somo nimetumia reference ya cgm (christ gospel messenger) iliyopo kanisa la EAGT. Mimi nasali EAGT saza songwe kwa Daudi Before mbeyeye (true pastor).
Hii haionyeshi mapungufu ya kanisani kwetu, ila nikaona nijifunze zaidi kupitia hali ambayo nadhani wengi wanaipitia kiroho na kimwili.
#sisi tupo vizuri zaidi na tunapambana ili tuione mbingu pamoja na viongozi wetu wa kiroho (mchungaji na wazee wetu wa kanisa).
Nimeona ni vyema nitumie mfano wa mazingira yangu ili hatimaye wote tuwe vizuri kabisa.
Mara nyingi tunafanya mambo ya rohoni kwa kutumia reference fulani, yaani tuna copy. Jambo ambalo siyo. Tusiwape wanadamu wenzetu hali ya kwamba tunakopi kila kitu toka kwao kwa kuwa yale yalikuwa ni wakati ule (kwa mwanadamu) japo MUNGU ni yule yule.
#kwa mfano nilisikia mfano kutoka kwa kaka kwamba CGM ya zamani ilikuwa moto tofauti na sasa. Ni sawa na ni kweli lakini hatuwezi kufanya mbinu ya zamani kuifufua CGM; ilikuwa ni nzuri kufikiria hivyo lakini halikuwa sahihi kusema kwa kuwa usahihi ni huu hapa: maana vitu vyote ni safi lakini sio vyote vifaavyo. Vyote ni vizuri lakini si vifaavyo maana kufaa kwa kitu kunatokana na wakati sahihi alionao mwokozi YESU Kristo pekee. (1 Korinto 10:23, 1 Korinto 6:12) .
YESU Kristo mwokozi wetu alivyokuwa anaponya vipofu alikuwa anabadilisha namna za uponyaji. Kwa kuwa MUNGU hazoeleki, na MUNGU sio formula ila mambo yake ndiyo formula na pia amri. Ko tutafuata mambo yake na neno lake ipasavyo lakini sio kwa kujirudia kama zamani ile. Tunamwomba MUNGU kuwa je BWANA YESU kwa sasa tunataka kufufuka mazima maana tunasema zamani na wakati huo zamani ilikuwa ko iliisha vibaya ko kumbe hatukuamka kihalali sana bali tuliamshana sisi kwa sisi na sio wewe uliyetuamsha ndo maana tukafa.
#basi BWANA YESU tunaomba nafasi mpya na hali mpya ya uamsho na uvuvio mpya usioisha kama maji ya uhai na uzima na yaliyohai jinsi tunavyokunywa yanatupa uhai na uzima milele. #maana mwanzoni huko hatukunywa maji ya uzima tulikunywa yetu!! Na tumwombe MUNGU katika nafasi zote tunazoziomba ziwe mpya na siyo mbinu za zamani bali mpya kwelikweli. Kwa kuwa wewe MUNGU huzoeleki wala huchunguziki maana ni wa ajabu ajabu kuu.
#ko twaweza anza kujilinganisha na CGM za makanisa mengine ni sawa ila si sawa kama tunataka tuwe kama wao. Maana hata wao wanaweza kuwa wanajaribu kuwa kama YESU mwenyewe ndo maana wanakuwa bora. (Mathayo 10:24) Ko kama wakristo na watumishi wengine wanavyojaribu kuwa bora basi na sisi tuwe bora na mwalimu wa kutufanya sisi kuwa bora awe ni YESU. Hapo tutakuwa na nafasi ya kuwa kama YESU, au pungufu ya YESU kidogo maana mwanafunzi hampiti mwalimu wake; bali akijitahidi aweza kuwa sawa na mwalimu wake. Je, sisi mwalimu wetu ni nani?
Utashangaa ni makanisa mengine na moto wao ndo mwalimu wetu au jinsi hali zetu za zamani tulizozikubali na kuzipenda sana ndizo zinazokuwa reference za maisha yetu ya sasa. Jambo ambalo siyo. Nakumbuka nilipokuwa naumwa nilikumbuka jinsi nilivyokuwa mzima jana yake tu. Nilipopona nilikuwa mzima lakini tayari kunakuwa na hali mpya ya kukumbuka ugonjwa na alama ya ugonjwa inabaki. Ko hata kidonda kikipona kunabaki kovu. Ko tunatengeneza mazingira mapya ya kuishi na kovu la zamani maana tushaumia tayari.
Ko tusitegemee uzima na ulinganisho wa watumishi wengine bali tumtegemee MUNGU upya kwa nafasi mpya na maono mapya hapo ndipo tutafika mbali. Tujinyenyekeshe kwa MUNGU kwa kujitoa kwa yote tuliyonayo kwa wakati huu sasa maana kwa mwanadamu wakati ni mmoja tu ndiyo sasa. Tutegemee jambo jipya na sio kama umoja wetu wa zamani, au hali zetu za zamani, ukristo wa zamani; tumruhusu bwana YESU ndani ya mioyo yetu kupokea nafasi mpya peeee!!.
#ko tukiweka ulinganisho na wengine ina maana tunataka kuwa kama wao ko wanakuwa ni kama waalimu wetu. Na wakati huo hatujajua kuwa wao mwalimu wao ni nani, na wao je wema waalimu wanaiga hatujui?? Na kwa kuwa ndoto ya mwanafunzi ni kuwa kama mwalimu wake basi tunajikuta tunakaa mbali na YESU kabisa. Maana tunakuwa wanafunzi wa wanafunzi wa wanafunzi... wa YESU. YESU anakuwa mbali ndo maana hatufikii hatua ya kufanana naye maana tunawafuata wanaowafuata wanaomfuata YESU.
Wakati formula ya kumfuata YESU ni moja (1 Korinto 4:15): ijapokuwa tuna waalimu na wainjilisti na waimbaji wengi ikiwapo na mimi miongoni mwao hata wawe kumi elfu, bado tuna baba mmoja hapa aliyebeba maono yetu na aliyetuzaa sisi kwa neno la YESU Kristo lililopo ndani yake. Naye ni mchungaji wetu hapa Daudi Before Mbeyeye na kwa wewe mwingine unayelisikia neno hili kwa mchungaji wako na mzao wako aliyekuzaa kwa injili. Aliyekuzaa katika ROHO kwa kupitia mwokozi na BABA mkuu ambaye ni YESU Kristo. #wale mitume walikuwa na neema kuu sana maana aliyewazaa ni Kristo mwenyewe directly tofauti na sisi ambao ni indirect. Neema ya ajabu.
#wengine wataanza kusema neema hiyo ndo iliyowafanya wao wawe tofauti na sisi. Hapana!!. Kwa kuwa pamoja na kwamba tumezaliwa kwa neno la watumishi wa MUNGU, bado si wao waliotuvuta sisi na kutufanya tuamini bali ni Kristo ametuvuta. Maana afanyaye yote hayo ni yeye YESU Kristo mwenyewe ko sisi tupo sawa kabisa na watumishi wa MUNGU, wale mitume kwa kuwa wote tumechaguliwa na Kristo japo ni kwa njia tofauti. Ko tuna mamlaka moja, nafasi moja, tumaini moja, lengo moja (Efeso 4:1), Bwana mmoja, mbingu moja.
#ko kama tumezaliwa na YESU kupitia watumishi wake je si sahihi kuwaheshimu hao?. 1 Korinto 11:1 lazima tuwafuate na kuwasikiliza na kuwapenda na kuwaheshimu watumishi wa MUNGU kama na sisi tunavyopenda kuheshimiwa hasa waliotuzaa. Sihalalishi kuwasikiliza waliozaa kwa upotofu ila maadamu umemuamini YESU, basi unaliamini neno lake na una Roho wa MUNGU unayo nafasi ya kutambua kuwa upo wapi. Paulo alisema vile kwa kuwa wengi wapo maeneo sahihi lakini papara na kukosa heshima kwa MUNGU na kwa watumishi wake wanachukuliwa na tamaa zao kwenda kutafuta wanachohitaji.
TUJIFUNZE KWA BABA KAMILI NA HALISI NA WA KWELI YUPOJE? NAYE NI YESU KRISTO MWENYEWE MWOKOZI WETU.
#je baba wa kuheshimiwa ni yupi? Paulo alikuwa na haki ya kutamka vile kwa Wakorinto kama vile na baba yangu wa kiroho alivyo na haki. Ko kumfuata BABA aliyekuzaa si kufungwa na kumezeshwa na yeye kama wababa wengine wanavyofanya. Ukiona una baba anakufunga uwe chini ya mafundisho yake na kukuteka na mafundisho ya awali ya ulimwengu (Wakolosai 2:8, Wakolosai 2:20), huyo ni kipofu na anataka akutumbulize shimoni (Mathayo 15:14). Anafanya kazi ya uwakala wa shetani japo ni mtumishi wa MUNGU.
#anawafunga kwenye mafundisho na mifumo ya mwili. Tusome Wagalatia 5:16-21. Ni kwa kuwa mabaya yote ni matendo yatokanayo na mwili ko akawafundisha kwa kuchukia uovu kwa kujihesabia haki, kuwachukia waovu na wanaoonekana wakosaji. Hiyo ndiyo chuki, adui wa upendo. Anasema chukia na farakana na wazinzi... Namshukuru pastor wangu anasema simchukii mtu ila naichukia dhambi iliyo kwa mtu. Ko kwa matendo mpende kwa lengo la kumbadilisha mtu maana upendo upo zaidi ya dhambi.
Tujifunze kwa mchungaji mkuu wa kweli na halisi YESU je alisemaje kuhusu watenda dhambi (Luka 5:27-32). Mafarisayo ni mfano wa wachungaji wenye haki zao na sio haki ya MUNGU. YESU alikuja kuonyesha jinsi gani mtu anapata haki mbele za MUNGU kwamba sio kwa kujitenga na waovu bali ni kujitenga na uovu. Tunaukimbia uovu na sio waovu. Maana uovu hauna nafasi mbinguni ila waovu wana nafasi ya kuuacha uovu na kuwa safi. Kama ilivyo sawa na neno la YESU kwamba wenye afya hawahitaji tabibu (doctor) bali walio hawawezi. Doctor anapomtibu mtu atampa dawa kali, na sindano zenye maumivu lakini kwa gharama za kupona mgonjwa hana budi kukubali.
#ko hata sisi kwa gharama zozote kama watu wa MUNGU tunapasa kuondoa nafasi za ugonjwa ndani ya watu kwa namna yoyote hata yawe ya kuambukiza kama korona (tutavaa barakoa na gloves - uongozi wa ROHO MTAKATIFU) lakini mpaka wapone na sio kuwatenga na kuwaacha wafe kwa mauti eti kwa kujiweka safi. Hiyo ni tabia yenye asili ya kishetani.
Anayefundisha wema wa sheria tu kama serikali inavyokemea matendo mabaya tu, huyo siyo wa kumfuata maana kanisani ni mahali pa kiroho. Hatupo chini ya sheria tupo kwenye neema ko tunatenda wema si kwa kuwa ni wema bali kwa kuwa ni haki yetu kutenda. Manabii wa uongo kwa kuwa hawatoi mambo ya roho kama ROHO atakavyo ila hukataza kama mwili na sheria zitakavyo... wanawafunga watu kufanya mema pasipo kuwa na YESU (upendo/haki).
Mathayo 5:17 YESU hakuja kuitangua torati bali alikuja kuitimiliza. Sheria pasipo YESU Kristo ni udhaifu na utumwa. Alifundisha pastor wangu Mbeyeye kwamba kuzaliwa mara ya pili yaani katika roho ni kugeuza nia toka ndani. Maamuzi ya ndani na kupokea haki ya kutenda mema... na sio kuwa na sheria bali YESU Kristo na ROHO Mtakatifu ambaye ni utimilifu wa sheria. Tunakuwa tunafanya mema sio kwa ajili ya kupata utukufu au kujihesabia haki, bali ni kwa kuwa ni haki yetu kufanya kwa kuwa tayari tumempokea YESU.
#ko ukiona mchungaji anataka kuwa yeye pekee ndo wa rohoni na ategemewe yeye, huyo siyo wa rohoni. Hata manabii wa uongo wanataka wategemewe peke yao, ushetani huo mbaya sana. #ishara nyingine ukiona mtumishi wa MUNGU amekufa afu na huduma aliyoianzisha imekufa huyo alikuwa ni wa uongo. YESU mchungaji wa kweli alipokufa ilikuwa ni nafasi ya wanafunzi wake kufanya kazi kubwa zaidi (Yohana 14:12). Alikuwa anawaandaa wanafunzi wake kuishi bila yeye katika mwili bali na yeye katika ROHO. Watumishi wanaojipa sifa wao tu na YESU hayumo ndani ya watu wakifa, hiyo ni sifa ya shetani.
Mifano ya huduma za kimungu ni kama huduma ya Ibrahim ikarithiwa na Isaka kisha Yakobo (Israel). Pia huduma ya Musa kwenda kwa Yoshua. Huduma ya Daudi ya kujenga hekalu iliendelezwa na Sulemani. Pia huduma ya Eliya Mtishbi ilienda mara mbili na kwa utukufu zaidi kwa Elisha. Mchungaji mzuri anatoa nafasi ya kukua kwa huduma za watu hata ikiwa kubwa kuliko yake. Bado si kwamba itachukua utukufu wake bali itaukuza zaidi utukufu kwa MUNGU.
Hata na mimi na wewe tuna nafasi. Namshukuru pastor wangu mzuri alisema anatamani kupata hata mmoja mwenye huduma hata mara 10 zaidi atafurahi kweli kweli. Yoshua, Sulemani na Elisha walirithi kwa utii na kujinyenyekeza. Ko wasiweke plan ya kumzidi pastor kwani hiyo ni zawadi ya MUNGU. Cha kufanya ni sisi kunyenyekea chini ya mkono wa MUNGU mwenyewe yeye ndo atoaye jibu.
HUDUMA YA KIROHO NI IPI?
Sifa za huduma za mwilini zilikuwa na mwakilishi mmoja tu wa kumwona MUNGU kwa ajili ya watu (Musa, Eliya, n.k.). Wale walichaguliwa tangu tumboni (Yeremia 1:5) bila kuwa na haki binafsi ya kuwa wateule. Kipindi kile neema ya MUNGU ilikuwa ni kwa mtu mmoja mmoja tu na kwa taifa moja tu. Sasa neema ya MUNGU si ya mtu mmoja mmoja bali ni neema ya wanadamu wote.
Inashangaza wenye huduma kuu wanaifanya huduma yao kuwa kuu na kujipa haki kuliko wengine, hiyo ni roho ya giza. Kama watumishi wa MUNGU tusijipe haki na kujiona bora kwani neema iliyotuokoa si yetu bali ni neema ya wote. Tujivunie mali binafsi ambayo tumezaa sisi wenyewe (matunda ya wokovu). Wanaopewa wokovu wasiozaa matunda ni kukatwa na kuchomwa moto (Mathayo 3:10, Luka 13:6-9). Kitu cha kujivunia ni kwamba tunazaa matunda ya rohoni (Wagalatia 5:22) maana hiyo inamaanisha majina yetu yameandikwa mbinguni (Luka 10:20).
Haki haithibitishwi na matendo yanayopimwa na watu bali na MUNGU mwenyewe (Wagalatia 3:11). Haki inapatikana kwa kujinyenyekeza na kujishusha kama mtoza ushuru. YESU alikaa na waovu ili awapate, alivaa mwili mdhaifu ili awapate walio dhaifu. Nguvu ya YESU ilitumika kuwapata wasio na nguvu lakini sisi haki yetu wakati mwingine inawatenga wasio na haki.
Thamani kuu ya mti inakuja pale matunda yanapotoka. Adui anaweza kujigeuza kuwa malaika wa nuru (1 Korinto 11:14) akatimiza sheria ya neema lakini akashindwa kuzaa matunda ya roho. Haki yetu tunaipata kwa njia ya imani (kuishi katika ROHO na utakatifu) na kuweka kipaumbele kwa MUNGU kwanza.
Huduma halisi ya MUNGU haisimami peke yake. Ili usimame ni lazima usimame na wenzake (Mithali 18:1). Sasa tunasimama wengi, tunabebana sisi kwa sisi ili wote tumwone MUNGU na wote tufike mbinguni. Zamani ROHO alikuwa kwa watu maalumu tu, sasa ni wa wote. Alikuwa anashuka kwa waliokuwa wateule tangu kuzaliwa, lakini sasa yeye ndo anatufanya wateule tukikidhi viwango kwa kumwamini na kumpenda. Kwa sasa sisi wote ni special mbele za MUNGU.
Amani Ernest kyamba
SOGH Team
#let's do GOD'S work together.
yapo masomo mengine zaidi,kujifunza zaidi.maana hakuna ukomo wa kujifunza rohoni na mwilini pia
link: soghteam.blogspot.com
Comments
Post a Comment