Ukiokoka unakuwa mtu wa namna gani?
09 Feb 2025
Ukiokoka unakuwa ni mtu wa namna Gani?
Amani Ernest Kyamba.
Hili somo linaenda kujibu maswali mengi kama yafuatayo:
~wengine hawajaokoka mbona wanafanikiwa?
#wengine wapo kanisani wanasali hawaishi kiroho lakini wanafanikiwa kwenye kazi zao
~wengine wanatoa zaka na sadaka ila hawafanikiwi.
hayo maswali ni sample tu ya viwakilishi vingi vya maisha ya wokovu ambayo YESU Kristo anataka tuishi. lakini zaidi Mimi nagusia mahusiano yetu ya kiroho na YESU Kristo ambaye ndiye ukamilifu wa Sheria (pendo ndilo linaikamilisha Sheria)
#mithali 3:5 kuokoka ni kuvua mwili, Roho na akili chini (za zamani) na kupokea vipya.
Ni kumwabudu MUNGU pamoja na wale wenye uhai nanne na wazee ishirini na wanne jinsi wanavyodondosha taji zao na utukufu wao mbele za MUNGU ufunuo 4:10-11 kwamba wenyewe wanabaki hawana taji Wala utukufu wowote ule . basi na wokovu halisi ni kwamba unavua vyote vya kibinadamu (akili, plani za kibinadamu na vyote) unakuwa huna kitu unabaki mkiwa Tena ili MUNGU aanze kuumba vipya vya rohoni mwanzo 1:1-2. maana MUNGU hawezi kujenga mahali penye uchafu (yaani palipo na vitu vyako mwanadamu) anajenga mahali palipo ukiwa (yaani uvue Kila kitu na vyote vya kibinadamu hatimaye uwe huna kituka bisaaa). ko kuokoka ni kukiri kwamba wewe huwezi jambo lolote na kwamba kwa kuwa huwezi unamwitaji MUNGU akuwezeshe na kukusaidia.
#wengine Sasa wameokoka ila Bado wanajiona wanaweza na Bado wanategemea akili zao na Mali zao na sura zao na muonekano yao na sauti zao na walivyonavyo. hapo Inamaanisha Bado hawajaokoka kwa upendo Bali wameokoka kwa Sheria. maana Sheria mambo ya mwilini, na upendo ni Mambo ya rohoni.
#Ukiokoka unakuwa kama kichaa asiye na akili kwa kuwa akili Yako ya asili unaitupa mbali.
Yaani ni kukiri kwamba wewe si wa thamani yaani ni wa chini mno na kuhitaji kwamba MUNGU yeye ndo akuwezeshe na yeye ndo awe thamani Yako kwamba pasipo yeye wewe hauna thamani.
"KAMA UNA YESU KWELI PIGA HESABU KWAMBA JE UKIMKOSA, THAMANI GANI ITABAKI KWAKO?"
KAMA IPO THAMANI ITAKAYOBAKI KWAKO UJUE BADO HUJAKAMILIKA KATIKA PENDO LA YESU Jiulize je umeacha vyote ukamfuata YESU Kristo kwamba akikuacha ni kweli unakuwa hauna chochote? Kama sivyo endelea kupambana upendo wako ukamilike kamili kamilifu.
#akili ya kidunia na ki mfumo wa kiulimwengu unaitupa afu unazama ili uipate akili mpya na fahamu mpya ya mbinguni.
#unapewa akili teule (imani) na fahamu na maisha mateule. kama ya Wana wa Israel walivyokuwa wanaishi kiteule tofauti na mataifa yote.
Unabalikiwa kwa imani na matendo mapya yaani ya kale yamepita Sasa yamekuwa mapya. ufunuo 21:1 Sheria za asili za utafutaji zinasema kujibidiisha na shughuli za Dunia ndo kunakupa maisha ya juu na ya kitajiri.
#lakini Sheria mpya ya rohoni inajieleza wazi kabisa kwenye kitabu Cha mathayo 6:24-33.
Wapo wengine wanatoa na kufanya mambo ya baraka ila hawabarikiwi kwa Nini? Kwa kuwa Bado hawajavua akili za zamani. yaani wanataka kuishi maisha mapya kwa akili za zamani.
#formula ya MUNGU ni dhahiri, Tena ipo wazi.
Tunadhani mwili utatufanya kumuona ROHO, akati Sheria ya MUNGU ya wokovu ROHO ikiwa njema, basi itadhihirisha mambo makuu mwilini. yaani wokovu unaanzia rohoni kuja mwilini na si mwilini kwendo rohoni.
Wokovu wa Wana wa Israel ulikuwa mgumu kwa kuwa walianza na wokovu wa mwilini ndo maana kamwe hawakuingia rohoni, lakini YESU alileta wokovu unaonzia rohoni kwa MUNGU na kudhihirika mwilini.
#sisi tunadhania Sheria ndo itakayotufanya sisi kumwona MUNGU. tukawaulize Wana wa Israel wa kipindi Cha Musa walikuwa na Sheria lakini je iliwapa Nini?
Iliwapa laana, kifo cha kizazi kilichotoka misri ambapo waliotoka misri wakafika kanaani walikuwa ni Yoshua na kalebu tu wengine wote walikufa jangwani walikuwa Joshua na kalebu na kizazi Cha vijana wa Israel pekee ndo walifika kanaani. pamoja na kwamba walikuwa na Sheria lakini Sheria Ile ile ndo uliowafanya Wana wa Israel kutoona nchi ya ahadi kwa kuwa ni Sheria ambayo halikuwa na upendo ndani yake.
,na mateso mengi kwa nchi miiba kama wafilisti na waamoni, babeli na nyingi. kwa kuwa Sheria (mwili) inalazimisha lakini upendo unafanya kwa hiyari. na YESU ndiye pendo, ko ukiona unalitaja jina la YESU Kristo na hauna upendo kwa MUNGU, unakuwa hauna YESU kwani YESU ni utimilifu wa Sheria mathayo 5:17 maana yake ni upendo yaani ni Sheria ya kupenda isiyotupinga Bali inayotuaokoa je wewe wokovu unakupinga? Ni mzigo kwako? Jiulize ndugu yangu.
YESU alichagua mitume kumi na wawili akaanza kuwapa semina nzito ya upendo mpaka wakafikia mahali wamejitoa na kuacha vyote kwa ajili ya YESU. akawapima akawauliza wakamjibu sawasawa ya alivyotarajia yohana 6:67-68, mathayo 19:27-29 baada ya kuwafundisha na kuona wamekamilishwa katika pendo (ambalo ndilo ROHO) Tena ndilo neno akaenda kwa baba kwa ajili ya kuwapa msaidizi ambaye ndiye ROHO MTAKATIFU.
#matendo 2:1 walikusanyika si kwa Sababu ya Sheria kwamba YESU aliwaambia msiachane. ila walikusanyika kwa Sababu walimpenda YESU Kristo wakayapenda na maneno ya YESU na kuyathamini.
#Walikusanyika kusanyiko la upendo na si kusanyiko la Sheria.
#upendo ndo unaleta kiu Tena ndo unaleta uhai na zaidi upendo ndio unaomvuta ROHO mtakatifu ashuke kwa udhihirisho mkuu wa ajabu mno.
#sasa sisi tunafeli kwa kuwa tunamwita ROHO MTAKATIFU kwa Sheria (kwa kuwa tu tumemwamini YESU Kristo) akati yeye anashuka kwa mtu aliyempenda YESU Kristo na neno la YESU lote.
#ko kilichomfanya ROHO MTAKATIFU ashuke kwa wanafunzi ilikuwa ni upendo ambao waliuwekeza kwa YESU KRISTO.
UTASEMAJE UNAMPENDA MUNGU AKATI HUYASIKILIZI MANENO YAKE. NA UTASEMAJE UNAYASIKILIZA MANENO YA MUNGU WAKATI HUMPENDI MUNGU? jiulize na jipe jibu mwenyewe.
Ukikamilishwa katika pendo inamaana tayar akili na mfumo wa zamani unakuwa umefishwa na Sasa unakuwa mpya.
Ina maana hautafanikiwa kwa mfumo wa mwili Bali utafanikiwa kwa mfumo wa ROHO sasa. kwa kuwa zaka utatoa kwa kupenda na sadaka utatoa kwa kupenda hivyo BWANA atabariki shughuli zako kwa mfano ambao aliwabariki Wana wa Israel.
Ko ukiona hujishughulishi na mambo ya rohoni kwa ukamilifu na ukawa na amani tu basi ujue kuwa Bado akili Yako na mfumo wa maisha Yako ni wa zamani, yaani unaishi kwenye laana ya mwanadamu. utapanda mara moja na kuvuna mara moja, lakini ukiingia kwa MUNGU utapanda mara moja utavuna mara mia Moja ni ajabu!! Lakini si ajabu kwa kuwa wewe mwenyewe ni wa ajabu kwa kuwa hata uloye naye ni wa ajabu mno!!.
Unataka kuwa wa ajabu basi mpende BWANA MUNGU wako kwa moyo wote akili zote mwili wote nguvu zote roho yote na vyote. hapo utakuwa wa ajabu maana upendo una nguvu kuliko mauti (Sheria) maana dhambi ilitambulikana kwa njia ya Sheria warumi 7:5-7.
#sheria tunaitii kwa kujilazimisha, lakini upendo unafanya tuitii Sheria kwa furaha kama jinsi Wana wa Israel walivyoweka agano na MUNGU la furaha kwamba watamfuata kwa kuwa walimpenda mno.
#je wewe unafanya mambo ya MUNGU kwa namna Gani? Kama ni kwa kujilazimisha ujue kabisa utafanya usilopenda kufanya. ni laana hiyo!!
#nenda kwenye neema ambayo ni upendo ndugu yangu. yaani upendo unaishinda mauti kabisa kabisa.
#wengine wataanza kusema kwamba ufalme wa MUNGU utatekwa na wenye nguvu, kwamba nguvu ni kujilazimisha, la!! Nguvu si kujilazimisha Bali ni kufanya kwa upendo maan upendo una nguvu basi na sisi tutairithi mbingu si kwa kujilazimisha Bali kwa nguvu ya kupenda na kuamua na kujikana kuanza kumfuata YESU hapo ndiyo akili mpya na ndiyo mfumo mpya aliouleta YESU si kushindana na mwili Bali ni kuushinda mwili kwa kupitia upendo.
Swali la tatu pale mwanzo litakuja kama somo lingine tutendelea nalo barikiwa sana mtumishi wa MUNGU
This is a SOGH
Amani Ernest Kyamba
Let's do GOD'S work together 💪
SOGH team...
Comments
Post a Comment