Ukuta wa moto


​14 Sep 2024

Kibali Cha kukua/je UKUTA wa moto unakufaaa?

​Ni sawa na simulizi Moja inahusu mtu mwenye silaha za kushinda ila hajajipanga kushinda...yaani katika vita na utumwa uliokuwapo kwa maeneo kutumikishwa na wavamizi yeye alikuwa na silaha Kali sana ambazo yakini zingeweza kuwapa hao wenzake uhuru lakini yeye akaona Bora utumwa kuliko kujitoa kwa ajili ya wengine.  

​*Tunakuja kuona jinsi watu wamevaa silaha zote ila sio utayari,, utayari tunauunda sisi na MUNGU akiuona anatufungia kwa miguu,, anatuvisha Sasa ili miguu yetu ipate kibali Cha kuanza vita.  

​*apandaye Wala amwagiliaye maji SI kitu Bali akuzaye. 1 korinto 3:7 tumapandwa na watumishi wa MUNGU katika shamba la MUNGU kupitia neno la injili..maji tunamwagiliwa kwa mafundisho ya ualimu na maisha ndani ya wokovu...  

​Ni sawa ila je Nini kitakacho mkuza mtu 1 korinto 3:8 baada ya kukamilika kwa matunzo ya mmea basi suala la roho ya mtu kukua linabaki kuwa la mtu mwenyewe na MUNGU wa mbinguni.kama ilivyo kwa mpandaji na mwagiliaji..  

​*Wengi wataniambia siku Ile bwana je hatukufanya kazi Yako lakini YESU alikuwa anaangalia utakatifu na utayari.. Wala sio kazi..maana hatujakuwepo kumsaidia Mathayo 7:21-23,, #ukianzia mathayo 7:1-21 tunaona kuwa kibali Cha kukua kiroho na kimwili kinaundwa na utakatifu.  

​*Wale walijifanya kondoo,, na yamkini walijiona kondoo lakini kazi zao zilikuwa mbovu kama za shetani.kwa kuwa zililenga kuwatenga wengine na MUNGU kwa mafarakano, masengenyo na mapotoshi,, ko kumbe unaweza ikawa umeajiriwa na shetani kufanya kazi inayoitwa ya MUNGU japo siyo..  

​efeso 6:15... Kumbe utayari ni silaha na pia ndo kibali Cha kuingia katika vita,, na pia utayari ndo kibali Cha kukua,,,wengi walikataliwa kwa Sababu hawakuwa na utayari,,kwa kuwa misingi ya kazi zao ilikuwa dhaifu na siyo ya MUNGU either wanataka Mali, wanajionyesha, wanataka wawapate watu na ulimwengu kupitia huduma, ni siasa, ni ushawaishi.. Watu wangu (sio watumishi wangu) ndo wanaangamia kwa kukosa maarifa ya rohoni wanafanya kazi yangu bila bila Mimi..ko mwishowe wataonekana waizi na wabaya kama shetani.  

​*Ili uwe na UKUTA wa moto lazima tuanze wako wa kuonyesha kuwa unataka UKUTA wa moto.  

​*YESU aliwafanya wanafunzi wake waunde nadharia ya mambo ya rohoni (waliwezakujua jinsi namna utakatifu ulivyo) ambayo mbeleni yalithibitishwa na ROHO.  

​*Sasa lazima tujue ili tuajiriwe kwa ajila za rohoni katika vitendo ni lazima kujua nadharia za rohoni.  

​*Sasa wengi wetu tunataka au tunajithibirisha wenyewe bila MUNGU kuwa na sisi..hapo ni kukataliwa..  

​Hatua za kuitwa mtumishi wa MUNGU.mwajiliwa/ mtenda kazi

​*Kuteuliwa,, kati ya wengi,,kwa Nini MUNGU alimteua Musa kusimama kuwaokoa Wana wa Israel,, ni kwa Sababu Musa huyo ndiye alionyesha jinsi gani anajali kuhusu ndugu zake kiasi Cha kuwasaidia kwa namna tofauti,,,kumbe kuitwa mteule kuna gharama kubwa sana,,hata sisi tuwe waajiriwa wa MUNGU kina gharama la sivyo tutakuwa tunamsaidia tu..jambo ambalo sio zuri.  

​*Kuunda UKUTA wangu (agano na MUNGU) (kuapa kiapo cha utakatifu.kama akina mitume waliomnea pepo kwa nadharia waliyojifınza kutoka kwa YESU lakini mda haukuwastahili pale mpaka walipokamilishwa na roho baada ya upendo wao kukamilishwa katika ROHO MTAKATIFU...  

​*Upendo na matendo mema bila msingi wa ROHO MTAKATIFU ni Bure lazima ili uwe na haki ya kuhesabiwa haki uwe mwenye haki unayeoshi kwa imani(UKUTA wa moto) maana imani inakupa tumaini na ushuhuda wa kuyatenda yakupasayo ili umuone MUNGU kwa kuwa imani ni uhakika wa yatarajiwayo,,la sivyo MUNGU hatakuhesabu kuwa mtumishi wake. tuumbe msingi kwa ajili ya upendo na utakatifu tulio nao ili uwe sehemu ya kazi iliyotuleta hapa duniani..  

​*Hapo kwa uweza wa MUNGU ndipo UKUTA wa moto (imani itajengeka).  

​Kwa Nini tunashindwa kuwa na UKUTA wa moto?

Ni kwa Sababu tunataka kujengwa bila kuteuliwa/kuitwa na MUNGU kwanza,, bila kuteuliwa ina maana tupo babeli afu tunataka tuinue malango juu ya malango? yaani tupo utumwani afu uwe huru,, haiwezekani,,ni sawa n kujenga nyumba ndani ya nyumba afu useme yangu hii..si sawa..  

​Let's do GOD'S work together

SOGH Team

​This is a SOGH

Amani Ernest kyamba  


Comments

Popular posts from this blog

Kuweza kulitendea kazi neno la MUNGU

Mwamuzi(short notes)

Je kwa nini namna ile?