Umba sababu njema

UMBA SABABU NJEMA 12 Feb 2026 Mwalimu: Amani Ernest Kyamba SOGH team Let's do GOD'S work together. YESU alipokuwa anasulubiwa pale msalabani, shetani pamoja na wanadamu waliona wanamuua YESU. Kwamba ndo mwisho wa mwokozi, wakati huo YESU alikuwa anaumba sababu njema kuwa analitimiza andiko, na pia anamaliza kazi iliyomleta kwani alizaliwa ili afe kwa kusulubiwa kwa ajili yetu. Shetani aliyajua maandiko, ko labda naye angekuwa kipaumbele kuzuia YESU asisulubiwe lakini shetani ndo akasapoti kwani na yeye shetani yupo kwenye uwepo wa MUNGU, anafanya kazi ya MUNGU japo hapati thawabu kwa sababu ya makosa aliyoyafanya. Hata na sisi tukiwa tunafanya matendo ya uzima, kwa kujifariji kama sauli alivyojifariji kuwa heri ng'ombe na vinono visife kuliko kufa, Eti Bwana ana njaa ya sadaka. Sauli alihisi kuwa MUNGU ni masikini na anahitaji vitu vyake, kumbe MUNGU anahitaji utii wake. Tukiwa kama "sauli na shetani" basi tutafanya mambo yapasayo thawabu ila hatutapata thawabu kwani tayari mioyo yetu ina kiburi kwa MUNGU aonaye sirini. Watu wengi wamekuwa na mtazamo uliopotiliza kumhusu shetani hata wakafikia Kumthaminisha shetani kuliko MUNGU kwa hofu zao na maisha yao ya duniani yalivyo. Sisemi kuwa shetani si mpinzani, nachomaanisha ni kwamba shetani ni mpinzani aliyeshindwa. Yaani maadamu tunaye YESU na tunamtii, basi imeandikwa kuwa tutampinga shetani naye atatukimbia (Yakobo 4:7). Ina maana kuwa shetani anamshinda mtu asiye na nguvu, kwani yeye hana nguvu akikutana na mwenye nguvu ambaye ni YESU. Yesu alimchagua Yuda Iskariote akijua fika kuwa huyu ndiye atakayemsaliti. Ko YESU alikuwa anaandaa mazingira ya neno la MUNGU kutimizwa. Ko hata na sisi haijarishi mambo gani yatatupata, lazima moyoni tuwe tunaandaa nafasi ya MUNGU (neno) kudhihirika kwetu. Wajapoona giza sisi tunaona nuru, waonapo uharibifu sisi tunaona uzima, yaani maadamu tuna Kristo tunaumba sababu njema haijarishi tunapitia jambo gani. Shetani alitamani kumuua YESU tangu YESU akiwa mtoto mchanga kwa kupitia Herode, lakini mipango yake haikufanikiwa. Zaidi zaidi utabiri wa neno la MUNGU ndo ukawa unatimizwa kuwa "Nalimwita kutoka Misri" (Mathayo 2:15) na "Sauti ilisikika Rama" (Yeremia 31:15). Ko shetani alibuni mbinu lakini akayaishi mapenzi ya MUNGU. Ko ni aina ya mtumishi wa MUNGU aliyekataliwa. Ndo maana katika Ufunuo inazungumza habari kuwa shetani atafungwa kisha ataachiliwa ili ayadanganye mataifa na atafanya hivyo, akakusanya kama Gogu na Magogu sawasawa na neno la MUNGU. Tunasema shetani anaijua Biblia (neno) lakini tofauti na sisi watumishi wa MUNGU wa kweli ni kwamba yeye analijua neno ila kwa kuwa alikataa nuru kwa kumwasi MUNGU, amegeuza kibao; kwamba kwenye kila neno jema la MUNGU anapata sababu mbaya kwani fahamu zake hazina nuru. "Analijua neno la MUNGU kigizagiza". Wapo wengi sana ambao neno la MUNGU linawapoteza wanapotea. Badala ya kujengwa na neno wao wanapotea mbali na neno la MUNGU. Wanalijua neno kama Wagalaia wasio na akili (Wagalatia 3:1). Hii ni aina moja na shetani ndo maana watu wa namna hiyo wanakuja kuwa mashetani katika wanadamu—"sababu mbaya katika neno jema la MUNGU". Wanaanza kutafiti neno ili watengeneze upotoshaji kwani wao na shetani wote ni mashetani (wapinzani). Pamoja na kwamba shetani anaijua Biblia mwanzo, basi alichonyimwa ni kuifasiri. Ndo maana anapotaka kuharibu, MUNGU anaumba sababu njema ya kujenga ko shetani anakuwa ni "mshindwaji siku zote". Hakuna jambo shetani atafanya kwa watu kama halijaruhusiwa na MUNGU. Shetani alimgusa Ayubu kwa kibali cha MUNGU. Shetani alimharibu YESU sio kwa sababu yeye shetani alitaka ila ni kwa sababu ROHO wa MUNGU alitaka. Ndo maana Mathayo 4:1 na Luka 4:1 inasema kuwa YESU alipandishwa na ROHO nyikani ili ajaribiwe na ibilisi. Ikimaanisha kuwa kabla shetani hajamjaribu YESU tayari YESU alijua kuwa sasa ni muda wa kujaribiwa kwani ana ROHO. Na shetani alitamani sana kumjaribu YESU lakini wakati wake ulikuwa bado ko akazuiwa na moto wa MUNGU mpaka aliporuhusiwa na pia akashindwa. Kama alivyoshindwa kwa Ayubu, akashindwa kwa YESU. Pilato akaambiwa na YESU kuwa hata mamlaka ya wewe kunihukumu mimi umepewa kutoka juu (Yohana 19:11). Ko kwa mtumishi wa MUNGU kila jambo analopitia inampasa kujua kuwa kibali cha jambo hilo kimetoka juu. Ko ni kuendelea kunyenyekea chini ya mkono wa MUNGU kama YESU alivyojinyenyekeza kama kondoo akiushuhudia wema na upendo wa MUNGU katika mapito ya msalaba. Je, sisi tunapopitia magumu tunaona nini? Tunanung'unika au tunanyenyekea kumwomba MUNGU kuhusu tunayopitia? Watu wengi tunanung'unika na kuamua kumkufuru MUNGU na kumtukana kama wale watu wa Ufunuo walivyofanya baada ya mapigo yale kuwa makubwa kwao. Kunung'unika na kutukana na kukata tamaa ni kuonyesha kuwa MUNGU si sahihi kwenye maamuzi ya maisha yetu, wakati MUNGU hakosei hata mara moja. Hili linamchukiza MUNGU ndo maana manung'uniko (Adamu) na fikra zetu chafu (shetani) na pia mtazamo wa kujitetea wa Sauli. YESU alipoanza kazi ya MUNGU Biblia inaonyesha kuwa wakati mwingi Mafarisayo na Wayahudi walijaribu kutaka kumwua ila YESU alijua kuwa wakati wake ulikuwa bado. Walishika mawe ila hawakumbonda. Walimbeba ili wakamtupe, YESU akapita katikati yao akaenda zake Kapernaumu. Yote ni kwa kuwa wakati wake ulikuwa bado. Sisi hatujui wakati ko wanaposhika mawe tunaona kubondwa, wanapotubeba kututupa tunaona mauti badala ya kuona uzima. Neno la MUNGU ndilo linalotambulisha nyakati tunazopitia. Ko tukiona hatujui wakati ni jambo la kujiuliza kuwa je, tuna uhakika kuwa tuna MUNGU? Ukifika wakati MUNGU atatuambia tu kwani hakuna jambo MUNGU anafanya pasipo kuwafunulia watu wake. Ndo maana mke wa Ayubu aliona Ayubu ameachwa na MUNGU ila Ayubu akasema "je tupate mema kwa MUNGU tusipate na mabaya?" Ayubu alijua kuwa hata ubaya wa MUNGU ni mwema. Yaani MUNGU ana ubaya mwema. Lakini vipi shetani? Yeye ana wema mbaya, kwa kuwa hata njia pana ni njema na kutamanisha kwa macho, ila mwisho wake ni upotevuni. Ila njia ya MUNGU imesonga, waionao kuwa ni njema ni wachache mno, na mwisho wake ni uzimani. Ni sahihi kabisa kuwa ulikuwa ni ubaya unaomkuta Ayubu, lakini Ayubu alipotulia kwa BWANA tunakuja kuona kuwa YESU aligeuza uteka wa Ayubu akawa mara mbili ya utajiri wake wa kwanza. MUNGU alifanya njia pasipo njia. Ko hata na sisi tunapopitia mabaya wakati tuna Kristo, tufurahi kwa kuwa mwisho wetu ni mwema. Na MUNGU anatazama mwisho wa jambo na si mwanzo wa jambo. Ko tusione ubaya tuone wema, tusione mabaya tuone mema; ndivyo MUNGU anavyotaka tufanye. YESU akasema "heri ninyi watakapowashutumu kwa ajili yangu, furahini na kushangilia kwani thawabu yenu ni kubwa mbinguni". Anamaanisha kuwa tunayoyapitia si kitu lakini tunayoyachuchumilia yana maana zaidi. Ko tunapopitia magumu tumaini letu la imani lisimame kwani ahadi za MUNGU zipo na zimesimama imara kwa ajili yetu. MUNGU ametanguliza ahadi zake kwetu mbele zaidi ya ukuu wa jina lake. Jinsi gani MUNGU ni mwaminifu kwetu!! Wanafunzi wa YESU walipopigwa na kupitia shida ngumu kwa sababu ya ushuhuda wa YESU walifurahi mno na kushangilia. Maana walijua hiyo ni njia ya wanapopaendea ambapo pana utukufu, hawakukasirika hata kidogo ila walipenda adha. Maana ndo point/marks zao zinaongezeka kupitia shida zao kutokana na injili (Warumi 8:35-39). YESU naye anasulubiwa, yeye anaona anatimiza andiko, anatimiza malengo ya MUNGU. Wayahudi na shetani wale wamefungwa fahamu wanaona ndo wanamshinda YESU na kumwua, wanafurahia na kumdhihaki. YESU anaona kutukuzwa kwake katika ulimwengu; jina lake kuwa kuu zaidi ya yote mbinguni na duniani na kuzimu na ulimwenguni mwote, anaona kuketi katika mkono wa kuume wa MUNGU, japo adui na Wayahudi wanaona kushindwa kwa YESU. Yeye YESU anaona ushindi mnono. Mwishoni wanamwanganika YESU. Wakati YESU yupo msalabani kwa furaha ya ushindi akakumbuka kuwa kuna andiko halijatimizwa!! Akasema "naona kiu" (Yohana 19:28), lengo la kuongea hivyo ni kwamba aendelee kukamilisha neno. Tena akasema "imekwisha" (Yohana 19:30), sawasawa na neno la MUNGU kwa vinywa vya manabii, akafa akazikwa akafufuka akatukuzwa. YESU akawaombea msamaha waliomsulubisha wote, kwa kuwa hawajui walitendalo. YESU alijua fika kuwa kweli hawajui walitendalo. Sisi je, tunapopitia magumu, tunaanza kulaani watu? Na kusema unamnyima mtumishi wa MUNGU?, rais anapingana na dini?, serikali inafunga wanaosali?, mtumishi ameuawa?. Tunalaani na kuwaombea mabaya wakati ndo muda wa kumshukuru MUNGU kwa ajili ya yote maana yanayotokea yalishatabiriwa kuwa yatatokea katika zama hizi. Ko hao watendao mabaya hayo kwetu wanaongozwa na kipofu mkuu (shetani) (limbuko la uovu), sio wao ko ni wa kuwaombea hao na kumkemea adui aliyepo ndani yao ili baadaye waje kujua kuwa walichofanya walikosea watubu, wasamehewe waende kwa Baba. YESU alipomwona Petro kuwa anatetea kusulubiwa kwake hakumkemea Petro bali alimkemea shetani ndani ya Petro (Mathayo 16:23). YESU alipowaombea toba watu wale, ilikuwa anafungua mlango wa injili kwao. Ndo maana wengi katika waliomsulubisha waliokoka baadaye. (Alimchukia shetani ila alimpenda Petro, alimchukia shetani ila aliwapenda waliomsulubisha kwani anasulubishwa kwa ajili yao). Sasa inashangaza sisi tunaowafungia watu wasiokoke kwa sababu ya tabia zao zilizotukera. Ni ishara kuwa hatujui mamlaka yetu kwamba tunalofunga linafungwa vivyohivyo na linalofunguliwa na sisi linafunguka. Ko tunajikuta baada ya kuwa mawakala wa wokovu tunakuwa wapinzani wa wokovu. Ko mwishowe tutakataliwa (Mathayo 7:22). Sababu za kukataliwa ni nyingi ikiwapo na hii watumishi wa MUNGU. YESU alimwombea msamaha hata Yuda Iskariote maana yeye YESU ndo alitwaa tonge akatumbumbwila akampa Yuda, Yuda akala, lile tonge lilikuwa na shetani. Ko ili shetani amwingie Yuda shetani akamwomba YESU aingie kupitia tonge ili unabii utimie (ndo maana nasema shetani ni mtumishi wa MUNGU aliyelaaniwa, anatimiza mapenzi ya MUNGU kwa namna tofauti na watumishi wa MUNGU halisi). Kama jinsi alivyomwomba MUNGU ili aingie kuharibu mali za Ayubu, pia alimwomba YESU, maana mwanzo hakuwepo kwa Yuda kwani Yuda Iskariote alikuwa na wigo wa moto. Baada ya maombi hayo ya shetani na kwa kuwa wakati ulikuwa umetimia YESU akampa ruhusa shetani ya kumwingia Yuda, akamchukua pamoja na tonge, akamfinyanga, akamlisha Yuda tonge (shetani). Ndo maana Biblia inasema Yuda alipokula tonge lile shetani akamwingia Yuda (Yohana 13:27). YESU hakuishia hapo kwani alipomruhusu shetani kuingia ndani ya Yuda, YESU akamwambia shetani "uyatendayo yatende upesi". Ile kauli ilienda moja kwa moja kwa shetani aliyekuwepo ndani ya Yuda. Ni kwamba hata shetani naye alisubiri amri ya YESU ili kuanza kazi. Jinsi gani MUNGU ni mkuu mno!! Basi shetani (Yuda) akaenda akaanza kazi (lakini ni kwa kibali kutoka kwa YESU). Ko baadaye YESU aliwaombea msamaha watu wote waliomsulubisha yeye Imanueli, kwani shetani ndo alikuwa ndani yao. YESU aliwapenda watu. Ndo maana watu wote aliwaombea msamaha halafu baadaye akaenda kumshinda shetani, kuzimu na mauti. Sisi tunaanza kuchukia watu, badala ya kumchukia shetani aliye ndani ya watu hao. Ndo maana Petro alipomwambia YESU kuwa "tutakusaidia hautakamatwa" YESU hakumwona Petro, alimwona shetani, akamkemea shetani moja kwa moja, akamsamehe Petro. YESU angekuwa kama sisi angemkemea Petro na kumfukuza. YESU hataki hata mmoja apotee bali wote wafikie toba. Sisi tunageuza tunataka wanaopotea wapotee ila wasiopotea wasipotee ko tunafanya matabaka. Kama wana wa Israel walivyojitenga na mataifa mengine na kuwaona kama uchafu. Tunawatenga huku sisi hatujakamilika ndo maana Matendo 28:28 inasema kuwa kwa kuwa wokovu mmeshindwa kuutunza huku mkijipa haki katika mapungufu yenu, basi wokovu huo utaenda kwa mnaowadhani kuwa ni wachafu (mataifa). Na pia nyie mpo katika hatihati ya kunyang'anywa. Ndo maana kuna kauli inasema "makahaba watawatangulia mbinguni". Tunasema waovu kumbe na sisi ni waovu, sasa MUNGU anatunyang'anya ili wale tunaowadharau watuonyeshe jinsi gani huu wokovu ni wa thamani. MUNGU alifanya hivyo kwa Waisraeli na mataifa, na bado kwa waliookoka na ambao hawajaokoka. Ko shika sana ulichonacho... Unaweza kuongezea mfano wa Yusufu na ndugu zake (wana wa Yakobo) katika kitabu cha Mwanzo. Yusufu alikuwa ameota ndoto ya kuwa mtawala. Nduguze wakamchukia sana ikichangizwa pia na kwamba baba yake (Yakobo) alimpenda sana. Nduguze wakamchukia wakamtupa shimoni, wakadanganya kwa baba yao kuwa amekufa. Wakaona si vyema kumuacha shimoni wakaamua kumuuza kwa Waishmaeli waliokuwa wanaenda Misri. Yote ni kwa sababu ya chuki zao. Yusufu akaenda kule akawa mtumwa wa Potifa, akapata kibali akapendeza kwa mke wa Potifa. Yusufu hakuhesabu heshima ya Potifa kuwa sababu ya kuzini na mke wa bosi wake (Potifa), basi akakwepa jaribu, akashutumiwa uongo na mke wa Potifa akaenda jela. Akasahauliwa na yule mnyweshaji—hakulaumu!! Hadi ulipofika wakati aliotafsiri ndoto ya Farao akawa mkuu wa pili baada ya Farao. Yote aliyofanyiwa, yote aliyopitia, yeye aliumba sababu njema kuwa ni njia kuelekea utukufu ambao alionyeshwa na MUNGU kupitia ndoto kipindi hicho yeye ni mdogo. Ko hakutunza wala kuonyesha chuki kwa yale aliyoyapitia, alijua kuwa mabaya yote hayo ni njia ya kuufikia wakati wa BWANA. Ndo maana hakuwachukia ndugu zake, aliwapenda ila hakuwaamini; alipowaamini akaudhihirisha upendo wake kwao aliouficha kwa muda mrefu. Sisi tungechukia ndugu, tusingewapa nafasi yoyote kwa yale waliyofanya. Ubinadamu huu!! Lakini Yusufu alienda kwenye neno la MUNGU la kuwapenda wanaowaudhi na kuwaombea. Kwani pasipo ubaya wao asingefika katika ndoto yake. Ko hata na sisi ili tufike mahali pa ndoto zetu za mwilini na rohoni, inapasa tujifunze kunyenyekea chini ya mkono wa YESU ili yeye atufikishe kwa wakati wake. Barikiwa sana!! Mwalimu: Amani Ernest Kyamba SOGH team Let's do GOD'S work together.

Comments

Popular posts from this blog

Kuweza kulitendea kazi neno la MUNGU

Mwamuzi(short notes)

Je kwa nini namna ile?