Usijiamini


04/02/2026

Usijiamini mwanadamu. (Ufarisayo na jinsi ya kuushinda)

​#Samsoni alijiamini akaamka kama ilivyo kuwa ada kumbe hayupo kwenye mfumo.

#farisayo alijiamini sana mbele za MUNGU kuliko mtoza ushuru na mtoza ushuru ndo aliyehesabiwa haki zaidi kuliko farisayo.

#wale watu walikuwa wanasema BWANA, BWANA hatukufanya unabii kwa jina lako,na kwa jina lako kutoa Pepo na huduma. kilicho wafanya wapotee ni kujiamini kwao kutokana na ishara yaani kuziamini ishara kuliko MUNGU. na sisi tunajiamini sana kutokana na tunavyoonekana kwa watu (ishara za utakatifu) tunasahau kuwa je tunaonekanaje kwa MUNGU wa mbinguni?.

#kilichomfanya shetani awe mwasi kule mbinguni ni kwa Sababu alijiamini sana kwamba yeye na wazo lake ni Bora sana.

#kilichomfanya nabii yule afe pale ni kwa kuwa hakujiamini kuwa neno la lililomwambia kuwa asile af yeye akala kwa neno la yule nabii mzee. i falme 13:1-30.

#je ni kwamba MUNGU alitaka yule nabii kijana afe? Hapana, ila alothibitisha jinsi watu tunavyoaminiana sisi zaidi ya jinsi tunavyomwamini MUNGU. upendo na imani ni vipengele viwili vinavyoenda kwa mfumo tofauti:: umpende mtu ndipo umpende MUNGU zaidi ya mtu, lakini imani ni kwamba umwamini MUNGU kwanza na zaidi ndipo uamini na watu.

#wakati mwingine tunamzuia MUNGU kusema na kudhihirisha mambo makubwa na magumu tusiyoyajua kwa kuwa anapokuja ndani yetu kusakama anakuta tayari tuna mafundisho na upana wa kibinadamu ambao tumeuwekeza tayari, ili yeye apande lazima aukute usafi wa shamba, anakuta Kuta zetu tulizoziweka maishani mwetu, imani zetu, matarajio yetu. akute tupo tayari sio kusikia tu bali na kufanya atakavyo yeye.

#kama yule nabii kijana alivyokuwa tayari kutoa maneno ya ushuhuda wa MUNGU kwa mfalme lakini hakutambua jinsi Gani neno la MUNGU halibadiliki akafuata ubinadamu wa MUNGU kupitia kwa mwanadamu ambaye ni nabii mzee (maana alidhani kwamba neno la MUNGU linabadilika badilika), badala ya kutambua ni nini maana ya neno la MUNGU (kwamba halibadiliki). ko MUNGU alikuwa anampima nabii yule kijana kwamba anamuonaje yeye, akakuta kumbe nabii yule aliwekeza kutoa neno kwa wengine lakini alisahau kujengwa na neno. ni sawa na mafundi ujenzi wanajengea wengine ila wao kwao hawajengi wanaona uvivu kwa kuwa hawapati faida yeyote ko hata watumishi wengine wamewekeza kujenga wengine kwa kuwa wanapata faida ya heshima na utukufu kwa watu ila wenyewe wamejisahau kabisa kwa kuwa wanadhani kuwa kujijenga wenyewe kwa neno hakuleti utukufu kwa watu, wanasahau kuwa kuwafanya wengine wamwone MUNGU, sio thawabu kubwa mpaka wao binafsi wawe wamemwona lasivyo inakuwa ni siasa tu.

#neno la MUNGU ni Moja na linakata kuwili kwa nabii na kwa mfalme lakini nabii alifeli kwa kuwa alidhani neno la MUNGU linakata kimoja tu, kujiamini kunzaiba kipengele cha kujijenga binafsi unakuwa mtu wa kuwasaidia wenzako wajengwe ila wewe unabaki hujajengwa. na mbinguni hautaenda kwa ulivyowaimarisha wenzio bali utaenda kwa jinsi ulivyojiimarisha wewe binafsi na tena zaidi kwa jinsi unavyowaimarisha wenzio.

Mafarisayo noa walikazana kuonekana watumishi wa MUNGU kwa watu baada ya kuonekana watumishi wa MUNGU kwa MUNGU. ko wapo kuwatumikia watu na sio MUNGU na thawabu yao washaipata kwa watu tayari.

Nabii yule alikufa kwa kuwa alijiamini na kijitia moyo kwamba kwa kuwa amefanya mapenzi ya MUNGU basi neno la kutokula na kunywa (kuutunza utakatifu) linapungua makali, hata sisi kwa sababu tunaomba na kufunga tunajitia moyo kuwa tuna neema kubwa, tunasahau neno la mungu ni kali vilevile na halitanguki, yaye anataka ujenge uku unalinda, tukijenga tu pekee bado ni mafarisayo sisi, na tukilinda tu badoni mafarisayo maana tuna matendo yasiyo ya imani na pendo 1 korinto 13:1.

​Somo hili halijaisha,mda sio mrefu nitapakia somo ambalo ni part 02 inayoitwa "USIJIDHARAU" ili tujengeke zaidi.

Amani Ernest kyamba

#SOGH team 

Comments

Popular posts from this blog

Kuweza kulitendea kazi neno la MUNGU

Mwamuzi(short notes)

Je kwa nini namna ile?