Usijidharau
31 Aug 2024
Hili ni part 02 ya somo linaloitwa "usijiamini".
Usijidharau kwa Hali Yako ya sasa, sisi wote ni sawa./wito wa MUNGU.
This is a SOGH
Amani Ernest Kyamba
Gharama tuliyonayo kuyapata maisha ndo hiyo hiyo ambayo tajiri anayo kuyapoteza maisha yake. Luka 18:20-23 yule tajiri aliifuata Sheria alijitoa kwelikweli lakini Kuna mahali pamoja tu hakujitoa (Mali yake halikuwa imeokoka). YESU akamwambia kwamba ili ukidhi viwango vya kumfwata YESU ni lazima kwanza uuze ulivyonavyo yule mtu akahuzunika kwa kuwa alikuwa na Mali nyingi (endapo zingekuwa chache angetoa kwa urahisi kabisa lakini wingi wa Mali ndio ukaongeza wingi wa ugumu wa kumfuata YESU.
#na YESU akasema ni rahisi ngamia kupitia kwenye tundu la sindano kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa MUNGU.
*Mjane sadaka yake ilikubaliwa kwa Sababu ya ukamilifu wa moyo wake kwa MUNGU. kwa kuwa sadaka ya kwanza inayohalalisha sadaka zingine zote ni utakatifu.
*Wale matajiri walitoa vingi vyenye maana lakini hawakuwa watakatifu, wao walitoa kuonyesha na kuongeza cv ya utoaji kwa watu.
*Lakini yule mjane mzee alitoa kiasi kidogo sana ambacho hakina maana mbele za watu lakini alitoa kwa Sababu alimpenda MUNGU na kumuamini kuwa atampa kingine na hicho ndicho kilichomfanya YESU amsifu yule mjane.
#basi na sisi tusijidharau kwa uchache wa tulivyonavyo mbele za MUNGU, Bali tujiimarishe kwa moyo mkunjufu na mtakatifu hapo MUNGU atatubariki kwa kuwa yeye haangalii wingi wa vitu Bali anaangalia utayari wa moyo wako.
#huwezi kumthibitisha MUNGU kwa kile ulichonacho, Bali unamthibitisha MUNGU kwa kile unachokitoa. (Maana ya kutoa hapa ni kujitoa wewe mwenyewe kwanza ndipo utoe na ulichonacho) .
*Wito wa MUNGU hauchagui mtu kwa Hali yake, Bali unachagua mtu kwa utayari wake. Mfano: Musa alikuwa mzito wa ulimi, Daudi alikuwa mchungaji mdogo wa kondoo, Petro alikuwa mvuvi, lakini wote walitumika na MUNGU kwa namna ya ajabu.
#usijione huwezi kwa kuwa huna elimu, huna pesa, huna muonekano, au huna kipaji Fulani, MUNGU anapokuita anajua mapungufu yako na yeye ndiye atakayekamilisha hayo mapungufu.
#elimu, pesa, na vyeo ni mambo ya mwilini tu ambayo mwanadamu anayatumia kumpima mwanadamu mwenzake, lakini MUNGU anapima roho na kweli.
#ukiwa na MUNGU wewe ni wengi kuliko wale wasio na MUNGU. Basi jiamini na uanze kufanya kile ambacho MUNGU ameweka ndani ya moyo wako hata kama kinaonekana kidogo kwa sasa.
*Kazi ya MUNGU haihitaji watu wenye uwezo mkubwa, inahitaji watu wenye utayari mkubwa kwa MUNGU. mfano Daudi, sulemani.
#ko namaanisha kwamba MUNGU hahitaji kitu Wala utegemezi wa kitu ila ni kwamba MUNGU anahitaji moyo wa MUNGU tu. ilimradi una moyo na una utayari na umeitwa na umeunda msukumo wa kazi ya MUNGU, haijalishi upoje, una Hali Gani, maadamu ni MUNGU wa mbinguni lazima kazi ifanyike.
#mwingine atasema msukumo analeta MUNGU jambo ambalo siyo. msukumo unaundwa na mtu, na pia uhitaji unaundwa na mtu (maandalio) ila jawabu (wito) unatoka kwa MUNGU mwenyewe.
#ndo maana YESU aliwavuvia wanafunzi wake ROHO MTAKATIFU yohana 20:22 na aliwapa maneno yote yamhusuyo msaidizi kwa lengo la kwamba wanafunzi wajue umuhimu wa huyo waunde uhitaji na utayari ili wampokee ko kiu inatoka kwetu sisi kupitia maneno ya MUNGU tunayojifunza. hata Mimi nimeandika Lile somo kuhusu vipofu wa aina tatu ili kwamba watu wajue upofu ni Nini na wajue kuona ni kupi na faida zake basi hoja yenye nguvu zinazoambatana na kiu zikifika kwa MUNGU tunapokea tunayoyao hakika. huwezi kuona kama huna hoja ya kuona. ndo maana YESU Kristo alipokuwa amekuja duniani aliuliza "Mnataka niwafanyie nini?" ili watu watoe hoja zao za uhitaji.
Mungu alibariki neno lake. Amen.
A.E. Kyamba from SOGH team
Comments
Post a Comment