Uvuvio
22 Jan 2025
Uvuvio
Fellow SOGH: Amani Ernest Kyamba.
Maombi sahihi ni kuomba uvuvio. uvuvio ni kama vile kuchukua kibali kwa yanayoenda kufanyika.
#YESU aliwavuvia (alitamka) ROHO mtakatifu wanafunzi wake (Hadi sisi). yaani alipotamka ni kwamba aliweka muhuri kwamba tukikidhi maandalio ya moyo kumpokea ROHO MTAKATIFU ni haki yetu kuongozwa naye ROHO MTAKATIFU.
Fellow SOGH: Amani Ernest Kyamba.
#ko hata uamsho hatitaomba uamsho lakini kabla ya matendo ya uamsho tunavuvia kupitia jina la YESU Kristo kwamba yanayoenda kutendeka yapate kibali mbele za hayo matendo ya uamsho.
#sulemani alivuvia hekalu alilojenga kwa ajili ya BWANA. Na uvuvio wa sulemani ukatimizwa kwani ndo ikawa hivyo 1 falme 8:22-61. pale ni kwamba sulemani alikuwa anavuvia hekalu la BWANA.
Uvuvio unaleta uhalali. ko hata sisi tunanung'unika kwamba huduma zetu hazikui ni kwakuwa hatujavuvia ukuaji. kwamba tunapoanza vitendo vya kukuza huduma (kupanda na kumwagilia basi akuzaye ambaye ni MUNGU mwenyewe atende kwa namna ya ajabu kukua.
#zaburi 127:1-2 ko BWANA MUNGU asipoulinda mji walindao ni Bure. ko twaweza kuifanya (kuulinda mji lakini ikawa Bure maana BWANA alindaye hayupo hapo) ko wengi tunafanya matendo ya uamsho lakini hatuamki kwa kuwa hatujauvuvia uamsho kwenye maisha yetu.
yaani hatujatamkia (hatujatambua) ko tunakuwa tunafanya halali lakini si kwa namna ifaayo maana kuvuvia kunaumba imani ya unakoelekea. ko hata mwalimu wetu mkuu YESU Kristo aliwavuvia wanafunzi wake (sisi sote) habari za roho ili kuanza kuwaunganisha wanafunzi wake na ROHO mtakatifu kabla hawajampokea.
ko uvuvio ndio unaotuunganisha na tunachoomba ambacho ni haki yetu.
#kama wasemavyo et ajira "connection" basi katika malengo yetu uvuvio ndo connection yenyewe.
Amen!!
#this is a SOGH.
let's do GOD'S work together
Kyamba.E.A.
SOGH team..
Comments
Post a Comment