Yule pepo akamtia kifafa
15 Sep 2024
Yule Pepo akamtia kifafa akamtoka
Luka 9:41
Marko 1:25
Marko 9:25
Lengo la Pepo kumtia kifafa yule mtu ni kupima uponyaji wa yule mtu kwamba mtu ajione mtumwa akati yupo huru.
#pepo alitoka Pepo ni kama nguruwe. tukifuga uovu ni mfano wa kufuga nguruwe. nguruwe ni mchafu sana, na ndiye anayezalisha uchafu kwenye zizi lake. kazi ya YESU unapoomba ni kuondoa chanzo Cha uchafu ambao ndio Pepo, lakini ukiondoa nguruwe Bado zizi litabaki chafu ko itaonesha kwamba hapa palikuwako na nguruwe.
#kuondoa huo uchafu ni kuanza mahusiano na MUNGU uchafu Baki wote utaondoka.
#wengine wanaondoa uchafu huku nguruwe Bado IPO, hapo itakuwa ni kuteseka, maana Bado chanzo kipo kinatusumbua.
Fellow SOGH Amani Ernest Kyamba.
#watu wameokoka na wanateseka na matendo ya Giza, lakini hawana Pepo na wanajishihudia kabisa kuwa hawana pepo, lakini wanateseka na tamaa na dhambi, ni kwa Sababu uchafu uliobaki hausafishwi, Bado wanaendelea kuufuga ndani ko Bado matunda ya utumwa yamebaki maishani mwao.
#pepo kumtoka mtu ni jambo la mamlaka ya MUNGU wa mbinguni ila kusafishwa na kufanywa safi ni mkataba kati ya MUNGU na mwanadamu.
#wengi wetu hatuna mkataba wa kufanywa safi.
#anapotoka shetani kwenye maisha yetu anaacha uchafu, huo ni sisi kusafishwa.
#ndo maana YESU alisema "Kila pando lisilopandwa na baba hakika litang'olewa" mpandaji wa pando (magugu) hakuwepo lakini pando lilibaki, Sasa YESU anataka tung'owe mapando hayo na mauchafu na maagano Baki ili kwamba tuwe safi. mathayo 15:13. Kwenye mahali hapo tunaona YESU alikuwa anawaambia wanafunzi kuhusu habari za mafarisayo jinsi Gani wanalipotosha neno na Wanamwabudu MUNGU, lakini shida ni kwamba Wanamwabudu Bure kwa kuwa misingi Yao ya imani imejengwa katika mwanadamu badala ya MUNGU.
#hawakuwa wanajiita watumishi wa shetani, lakini matunda waliyonayo yalikuwa ni ya Giza, japo habari za mtu unaozaa hayo matunda hazikusemwa pale. mti unaozaa matunda mabaya ni Pepo/ROHO chafu tunauweka mioyoni matunda tunayatunza yakiiva yanadondoka mfano wa maembe yaliyoiva yanavyo dondoka. tukimruhusu YESU aingie maishani mwetu anakuja kuukata mti/kufukuza Pepo lakini matunda mabaya yanaweza kuwa yamebaki mioyoni mwetu yalidondoka. yeye YESU hapandi mti mwema kwetu mpaka ule uchafu wa Giza na WA Pepo uondolewe, maana mbolea ya mti mzuri uzaao matunda ya roho sio uovu lakini wema ndio unaozaa wema mathayo 25:29. Na wema hauchanganyikanyi na ubaya.
ko ili ije mbolea mpya ya kukuza mti uzaao matunda ya roho wagalatia 5:19, hiyo mbolea ni ROHO mtakatifu. ili aje ni lazima aukute moyo kuwa upo safi, ili ule mti wa uzima ukuzwe katika ROHO mtakatifu.
#sasa sisi wakati mwingi tunafeli katika habari za rohoni kwa kuwa Bado tumetunza na tumeuacha ule uchafu aliouzalisha/alioupanda shetani (Gugu) katikati ya maisha yetu.
Fellow SOGH Amani Ernest Kyamba
tusome vizuri kabisa ili tuelewe vizuri
Tukisoma mathayo 5:8 katika lile hotuba ya mlimani YESU anasema heri wenye moyo safi maana hao watamwona MUNGU.
#inamaanisha kwamba ili tumwone MUNGU maishani mwetu ni lazima sharti la kwanza tuwe na mioyo safi.
#ina maana kwamba tukiwa na uchafu mioyoni tunakuwa Bado hatuna nafasi ya kumwona MUNGU maishani mwetu japo tunaye Tena yupo Tena ndo anatuongoza. kama nilivyozungumzia habari ya aina ya vipofu zile tatu ambazo ni wale waliopo nuruni lakini macho hayaoni, wale waliopo gizani na macho Yao yanaona (mafarisayo wa injili), na wale waliopo gizani na Tena hawaoni (watenda dhambi).
#aina inayozungumziwa hapo kwenye kitabu Cha mathayo 5:8 ni hiyo ya walio nuruni ila ni vipofu. kinachotufanya tuwe vipofu kwamba tusimwone MUNGU japo tunaye ni ule uchafu ambao tunao ndani ya mioyo yetu ambao adui aliuacha akauanda kama magugu, ule ndo unatupa upofu.
Kwa mfano katika Luka 18:34 inasema kwamba YESU aliwaambia wanafunzi wake kwa habari ya kuteswa kwake lakini wakati huo alitambua kabisa kuwa ulikuwa ni wakati fahamu zao zilikuwa zimefumbwa wasielewe neno. ni kama mbegu iliyopandwa alafu Bado haijachipua juu ya ardhi, ko tunaweza tukawa tumejaaliwa kuyajua mafumbo ya MUNGU lakini yakawa Bado hayajafumbuliwa kwa kuwa Bado ni aina ya vipofu.
#tunakuwepo nuruni na tunafaidika na Nuru (MUNGU) tunalima tunavuna (kufanya kazi ya MUNGU), tunatoka jasho (kutakaswa), tunatambua na tunatofautisha kati ya Nuru na Giza. tupo nuruni ko joto la jua/Nuru linatupiga tunajua ni Nuru hii na usiku tunautambua (uvuli wa mauti) kama neno lisemavyo tujapopita katika bonde la uvuli wa mauti hatutaogopa.
#joto la jua ni majaribu tunayopitia yanayolipima neno, na sisi kwa kuwa tuna neno tunaharibiwa kwa Hilo neno kama mbegu iliyopandwa na mpanzi. ko joto linatupata linapima wokovu wetu.
Fellow SOGH: Amani Ernest Kyamba
#lakini sehemu Gani inakuja kuonesha upofu?
Jua tubalihisi kwa joto (majaribu tunayopitia ndani ya wokovu) upofu unaonekana kwa kuwa Bado hatujaona kipengele Cha Nuru (mwanga) kutoka kwa MUNGU.
#Yesu ni chanzo cha Nuru na joto. tunaona joto tu lakini Nuru inayotupa tumaini hatuoni kwa kuwa Bado ni vipofu.
#nuru inaleta tumaini la mambo yajayo.
#kwa kuwa tupo gizani hatuoni yajayo, tunashindwa kuukomboa na KUUTAMBUA wakati.
#kama ilivyo kwa mimea kwamba inahitaji Nuru ili kijitengenezea chakula (mwanga na sio joto) tunapokea malighafi neno kutoka kwa watumishi wa MUNGU lakini tunashindwa kulifanya neno la MUNGU kuwa bidhaa yenye thamani kwa kuwa ni vipofu Bado sisi. kwa kuwa ili neno tunalifundishwa liwe kamili, ukamilifu huo unapimwa katika kulitendea kazi neno la MUNGU.
#hatuna bidhaa tunakuwa na wokovu malighafi yaani usio na thamani kwa kuwa tu vipofu sisi.
#mwanga ndio unaosababisha mimea kukua ko tutambue kuwa Nuru ndiyo inayothababisha sisi kukua. ko kwani tunaganda hatukui kiroho ni kwa Sababu sisi ni vipofu hatuoni, na joto linalokuja kutupima linatuunguza kwa kuwa Nuru ndo uhai, ko joto linahitaji Nuru ili liwe na thamani kwetu, likiwa peke yake tutaongua sisi.
#yaani majaribu yatatuangusha tukisipokuwa macho. mpaka tuione Nuru na YESU ndiye Nuru inang'aa Gizani na Wala Giza halikuiweza.
#na ili tuone Cha kwanza ni kusafisha ndani ya mioyo yetu sisi ambao ni wajibu wetu sisi, kuweka tayari mambo ya nyumba zetu sisi kama Hezekiah. kuomba msaada wa ROHO mtakatifu asafishe mioyo yetu iwe safi ili tuione Nuru nayo Nuru ituweke huru katika jina la YESU Kristo amen!!
Note::: kinachotusafisha ndani ya mioyo yetu sisi ni neno, neno linatuweka huru mbali na uchafu na YESU ndiye neno. sio kumwamini tu kunakotufanya YESU kuja kutufanya safi, Bali ni kumtambua na kumpokea maana alikuja akakaa kwetu kama sisi alivyokaa kwetu lakini wale hawakumtambua (hawakujua thamani ya YESU maishani mwao). tutambue thamani ya Nuru, tutatambua thamani ya kuona, hivyo tutapeleka hoja yenye nguvu kwa ROHO kwamba tunataka kuona, YESU ataona kweli tunahitaji kwa kuwa tumejua kuwa kuona ni Haki yetu. tukiomba vitu sio haki yetu hatutapewa, tutambue haki tuishi nayo kwa imani hapo tutaomba na tutajua tunaloliomba ameeeenn!!!
Mkataba wako wewe na MUNGU wa kusafishwa ule uchafu wote (maana kusafishwa ni nipe nikupe) utaendelezwa na somo la kwanini hatumwoni MUNGU.
This is a SOGH
Let's do GOD'S work together
Kyamba.E.A
Blessed you all.
Comments
Post a Comment