Part 03:kugeuza nia

MAUTI IMO SUFURIANI


2 falme 4:40

Je udhaifu wako ni nani anautumia kuwa chombo.uhitaji wako na tamaa Yako Ina asili ipi?

Wale manabii kipindi Cha Elisha walikuwa na njaa wakakusanya chakula chenye mauti?.

Kila mtu hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe

Ko tusikubali mahitaji na kiu yetu itupeleke gizani/ kwenye mauti.

Hata siku Moja MUNGU hamjaribu mtu.

#lakini mwanadamu ndiyo kwanza anayeanza na tamaa.hiyo tamaa ndiyo inayomfanya MUNGU au shetani aingilie kati

#yohana anasema tujithibitishe na tuthibitishe kwamba roho inayotuogoza kwenye tamaa tuliyo nayo ni ipi?

Mbaya au nzuri?

#maana wale Wana wa manabii walikuwa na lengo zuri tu la kula chakula lakini adui akataka awaharibu kupitia tanaa yetu.

#tunaanza kwa misingi mizuri alafu tunajenga nyumba mbaya(wokovu).

Kwa kuwa hakika Kuna kuwa Kuna mahali tuliruhusu na ushauli wa shetani kwenye maisha yetu 2 nyakati 10:13.

#rehoboamu alichagua njia mbaya ya vijana badala ya kufuata njia ya matendo.

#ko tunajifunza kuwa lengo la Rehoboam lilikuwa ni kujenga mausiano mazuri na Israel lakini ushauri wa vijana ulikuwa ni shetani.

#wakati mwingine sisi tunaomba mambo fulani ya kimungu lakini yanayokuja yanakuwa si ya  MUNGU kwakuwa ni sawa na mtu analengo la kwenda kaskazini alafu anapitia njia uelekeo wa kusini.ko tunajikuta katika ugumu mkubwa mno kuzifikia baraka za MUNGU za rohoni kwa kuwa tumepita katika njia ya shetani katika kumtafuta MUNGU.

#shetani anataka chakula akitie sumu kiwe mauti.ko chakula ni haja zetu ko wakati mwingine tunashindwa kutambua kuwa je haja zetu zinahusiana na MUNGU au la!!.

#tunashindwa kujua kuwa je Kuna mauti humu ili tuikwepe?.

#wana wa manabii walitambua wakapiga kelele "mauti imo sufuriani" kutambua kwao ndipo kulimpa MUNGU nafasi ya kuingilia kati ili wasiuliwe na njaa kwa kula chakula chenye mauti.

#na sisi tujapopita kwenye bonde la uvuli wa mauti hatitaogopa maadamu tumetambua tupo wapi Basi tukimwita BWANA, hakika atashuka  kutushindia..la tusipotambua tupo wapi MUNGU atakosa nafasi ya kujitwalia utukufu kupitia uhitaji wetu kwa kuwa baada ya kushinda hatutajua tulikuwa kwenye mashindano,na hatutajua ni jinsi Gani MUNGU ametupigania.yeye MUNGU anataka ajitukuze kwa mtu anayemtukuza kwa kujua jinsi Gani yupo na uhitaji.

#yohana na Yakobo waliomba kuketi kuume na kushoto katika ufalme wa YESU jambo ni kiu sahihi lakini halikuwa la ROHO,kwani lilisababishwa na tamaa za wao kuwa watu wakubwa kuliko mitume wengine.yeye YESU akawaambia Hilo linalo kwa waliowekewa tayari(na wao wakiwemo)

Maombi ambayo yanaombwa pasipo kutambua haki ni batili.na haki inathibitishwa kwa imani.

#yakikosa haki adui anaweza akaingilia na kutuharibu kabisa.

#tanguliza haki(utakatifu) kwanza kabla ya maombi.ukitanguliza maombi kwanza shetani anaweza akasaidia kukujibu hatimaye ukazaa mauti

#ko kuzijaribu hizo ROHO ni kujijaribu mwenyewe kuwa upoje mbele za unayemwomba? Ukiwa na haki shetani ni adui wa haki hatakugusa hata kidogo.hataingilia haki yako

#wana wa manabii walianza wao ndipo wakamruhusu MUNGU(neema iliwabeba hawakufa na mauti iliyo kwenye chakula)

#ukianza wewe pekee unampa na nafasi shetani ya kuyaharibu maombi na haja Yako.

#mruhusu MUNGU aanze kwanza.adui hatakugusa hakika.hautaona nguvu ya mauti ya kuweza kukuangusha.

#ujapokanyaga nge na nyoka/ukitambua kabisa kuwa hao na wakanyaga ni nge na nyoka/ hakika hawatakudhuru na utampa MUNGU utukufu hakika

Barikiwa sana fellow SOGH 

Mwalimu:Amani Ernest kyamba

SOGH TEAM 

let's do GOD'S work together.


Comments

Popular posts from this blog

A.Kuweza kulitendea kazi neno la MUNGU

Je kwa nini namna ile?

Mwamuzi(short notes)