Posts

Usijiulize ulize

 hint: MUNGU alimwambia Musa awahesabu Wana wa Israel hesabu 1:2.lakini si kwamba MUNGU alikuwa hajui idadi.wala sio kwamba Musa alikuwa hajui kwamba MUNGU anajua idadi ya Wana wa Israel. MUNGU anajua hata idadi ya nywele, kwenye kichwa Cha Kila mtu hapa duniani mathayo 10:30. Kwa Nini alimwambia Musa ahesabu wale watu.ni kwa Sababu ni MUNGU.anataka kupima utii na uwezo wetu wakulitendea kazi neno lake.ndo maana hata kwenye masomo yaliyopita kumhusu Adam na Hawa jinsi walivyowekewa ule wa ujuzi wa mema na mabaya.ulikuwa ni Sheria inayopima uwezo wa mwanadamu kulitii na kulisikiliza neno la MUNGU.        ili kwamba endapo wakiitii Sheria(wangesikiliza neno la MUNGU) basi wangekuwa na Uhuru na ukamilifu siku zote lakini pale tu walipokula ilimaanisha Sheria Ile ikawapinga ikawazuia.          Tukisoma vizuri tunakuja kugundua kuwa adamu na Hawa Wala hawakujua kwa Nini MUNGU aliwaambia wasile Lile tunda.lakini kwa kuwa ilikuwa ni neno la MUN...

PART 01:HATUA ZA UKUAJI

 Mwandishi:Amani Ernest kyamba. SOGH Team.          MUNGU wa mbinguni alipoanza kuumba mbingu na nchi,dunia ilikuwa ukiwa,tena utupu tena giza lilitanda juu ya vilindi vya maji.MUNGU akaanza somo la uumbaji kwamba yeye awezaye yote angeweza kuijaza Dunia yote kwa siku moja au wakati mmoja tu.angeweza kuumba vyote kwani yeye anaweza vyote.akatoa somo kwetu kwamba katika kujenga,Mda ni kipengele cha muhimu zaidi.          Pia katika technology ya ufundi wa ujenzi wa nyumba.mtu anaweza kuwa na gharama nzima na maandalizi mazuri ya ujenzi,lakini akiwapelekesha mafundi wake wamalize ujenzi mzima wa nyumba kwa wiki moja.inawezekana.lakino asilimia za uimara wa nyumba hiyo unakuwa mdogo sana .na labda yajapotokea mafuriko,pepo,na mabadiliko ya Hali ya hewa,hiyo nyumba itaanguka,au yaweza kuanguka hata kabla haijamaliziwa kujengwa. Yote hiyo inasababishwa na ujenzi kutokuwa na hatua.         MUNGU angeweza kuumba wanadam...

B: kuweza kulitendea kazi neno la MUNGU

 Mwalimu:Amani Ernest kyamba  Mathayo 13:1 Njia na Mwamba.. Roho mtakatifu ni jumla ya mazingira yote ya kuifanya mbegu ikue.  Neno likikaa kwa mtu ambaye Hana  wokovu wa YESU Kristo ni kama upuuzi.ndo maana ataonekana kuwa haelewi kwa kuwa Mwamba hauna msingi wa kujenga nyumba...ko atalipokea kwa furaha kama Wana wa Israel walivyofanya( au kama mfano wa mbegu katika udongo) lakini yalipokuja majaribu kulipima neno yakawashinda kwa kuwa walikuwa hawana msingi unaojenga thamani ya NENO LA MUNGU.ko wakawa hawaoni thamani ndiyo maana maneno ya MUNGU wenyewe waliyachukulia kama ya MSA ko hawakuweza kubadilika.ko waliyashika lakini hayakuwa msaada kwao wakati wa shida ..ko Wana wa Israel walipandwa neno juu ya miamba .. ko kumbe udongo ni msingi// ko Mwamba ni sehemu haina udongo mwingi ko Ina maana hakuna msingi imara na ndio maana pepo na mafuriko yalipokuja kuleta majaribu mtu alidondoka kwa kuwa matunda ya neno yalikuwa mateta...na hayakuwi Tena .. Mzizi ni roho wa MU...

Unalinda?, Unajenga?.

 This is a SOGH:Amani Ernest Kyamba    Maana ukisipofanya na MUNGU inakuwa Bure kabisa zaburi 127:1-2. (Jambo la kwanza kabisa katika kuunda chemichemi ya uzima ndani ya mioyo yetu ni kugeuza Nia zetu ovu na kuhamisha kuwa na Nia safi kabisa..       ili kuujenga wokovu imara kama ilivyoandikwa kwenye mathayo 7:24-26 nafasi kuu ambayo mwanadamu inampasa aifanye ni kujenga na kulinda.                 kwanza kabisa tujifunze kutoka kwa Nehemia aliyekuwa anajenga mji wa yerusalemu jambo ambalo lilikuwa ni mapenzi ya MUNGU kwamba ule mji wa yerusalemu ujengwe upya kama jinsi wokovu wetu ilivyo kwamba tukiokoka ya kale yote yapite na hatimaye yawe mapya.  nehemia alikuwa ana lengo Moja tu la kujenga Kuta za yerusalemu akawa ameomba na ruhusa Toka kwa mfalme artashasta ili akaujenge mji wa baba zake. ni jambo kuu ambalo MUNGU alikuwa analihitaji kutimia kutoka kwa watumishi wake Nehemia na wale hamsini elfu. basi wale w...

Part 01: imani na akili

 Mwalimu:Amani Ernest Kyamba  SOGH Team   Ni mwendelezo wa maelezo yaliyopo kwenye somo la ubatizo,utatu mtakatifu,na sabato.na hili neno la MUNGU zuri la kiroho kabisa litatusaidia kushinda na kushinda zaidi ya kushinda.katika hili,kama tulivyojifunza kwenye masomo yaliyopita namna ya muunganiko kati ya sheria na neema,sasa tunaenda kujifunza Tena kuhusu akili na imani.     Karibu sana mtumishi mwenzangu.twende pamoja.      Kwanza kabisa nitoe ushuhuda unaoambatana na shukrani kubwa sana kwa MUNGU.kwa kuwa mwaka 2024, mwezi wa tatu niliumwa ugonjwa mbaya sana unaitwa malaria 🦟.       Ulianza kama maumivu ya kichwa ambayo yalianza kama utani, siku ya kwanza nikajipa moyo kwamba nikinywa maji afu nikilala nitapona asubuhi yake.kesho yake ugonjwa ukawa zaidi nikajikaza nikaenda na kazini Tena lakini kichwa kilikuwa kinauma sana,sijawahi umwa kichwa kwa namna ile. nakumbuka hiyo siku nikalala chumbani hapo kwa pastor maana nilijihisi ...

Part 02:KIVULI CHA YAJAYO

 Kabla haujasoma ujumbe huu,itapendeza ukisoma sehemu ya kwanza ya hili somo linaitwa KIVULI CHA YAJAYO. Unaweza kulisoma kabla ya hii part 02 ili tuweze kupata ujumbe uliokamilika zaidi. Kwanza nimalizie somo lililopita kwa kitu kimoja.   Ufalme wa MUNGU(wokovu) utashuka kwetu pale tu kwanza tukikubali udhaifu na kuhitaji msaada.udhaifu ni Sheria ya torati.ko kamwe hatutastahili agano la wokovu kama hatujakubali kufuata Sheria ya MUNGU kwanza na kushindwa...(Tunajifunza zaidi) Luka 17:20-21 Tunaona kuwa ufalme wa MUNGU ulikuwa katika Israel kwanza kutokana na uwepo wa torati(Sheria). ufalme inamaanisha utawala ko inamaanisha kwamba ukianza kujitahidi kuzifuata Sheria za MUNGU Kuna dalili kwamba unatawaliwa na MUNGU.ko inamaanisha kwamba lazima tuzifuate Sheria za MUNGU kwanza hapo ndipo ufalme(utawala) wa MUNGU utakuwa kwetu. Mathayo 21:43 lakini YESU anakuja kusema Tena kwamba ufalme wa MUNGU utaondolewa kwenu kwa kuwa hamzai matunda ya kifalme na watapewa watu wengine..hii ...

Part 01:KIVULI CHA YAJAYO

 My name:Amani Ernest Kyamba  SOGH Team  Let's do GOD'S work together  Kwenye Lile somo lililopita la "KWA NINI UMEOKOKA" tulizungumzia watu waliopambana na ya chini wakashindwa basi nilibakisha mfano mmoja wa mtu aliyeshindana na Nuru akaishinda yakobo alipambana na MUNGU wa mbinguni aliposhinda akapata baraka kubwa kuliko wote duniani.mshinde MUNGU uteke ufalme wake maana ufalme wa MUNGU unapatikana kwa nguvu na kuuteka. Na siyo kuwa na lengo la kushindana na ulimwengu.maana YESU alishinda ulimwengu sio kwa kushindana nao Bali kwa kutoa mfano wa kujitoa kikamilifu mbele za MUNGU.ndipo akaishinda. part 01: PALIPO NA UDHAIFU PANA NGUVU Lengo la haya masomo ni kuwafumbua  wakristo waanze kuona mambo ya rohoni kujua walipotoka walipo na wanapokwenda..maana watu wengine wanasema wametoka mbali huku kumbe walipo ndo waliipotoka hapo walipo ukiwa hivyo basi maana yake mtu unakuwa kipofu yaani usiyeona chochote.YESU.kristo anataka tuone, kwamba macho yafumbuke tujue t...